Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
Dkt. Salome A, MD
31 Oktoba 2026, 15:23:37

Matokeo ya kipimo cha VVU kwa mtu anayetumia vema dawa za kufubaza VVU (ART)
Jibu kwa ufupi
Jibu kwa ufupi: Kipimo cha VVU hubaki chanya – ni kawaida. Fuatilia kwa viral load. Hasi kwenye kipimo cha haraka si kupona – usiache ARV. Soma Je, mtu anayetumia ARV kwa miaka 3 anaweza kuambukiza?.
Maelezo
Vipimo
Kingamwili (haraka, kizazi cha 3/4) – hubaki chanya.
Viral load – lengo: haipimiki.
CD4 – hali ya kinga.
Kipimo hasi kwa anayetumia ART
Huweza kutokea kwa walioanza ART mapema sana.
Si kupona – virusi hujificha mwilini.
Kuacha ART huleta virusi kurudi haraka.
U=U
Viral load haipimiki kwa miezi 6+ – hakuna maambukizi kwa ngono.
Kondomu bado hukinga magonjwa mengine ya zinaa na mimba.
Soma Namna VVU vinavyoenea.
Nini cha kufanya
ARV kila siku saa ileile.
Viral load kwa ratiba ya kliniki (mara nyingi kila miezi 6–12).
Usipime VVU kuthibitisha kupona.
Dalili za hatari
Vipele vikubwa, macho kuwa ya njano, kubanwa pumzi – hospitali mara moja.
Lini umwone daktari
Viral load inapimika au imepanda.
Umesahau dozi mara nyingi.
Unafikiria kuacha ARV.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
1. Nikitumia ARV kipimo kitakuwa hasi?
Kwa kawaida hapana; hubaki chanya.
2. Kipimo hasi kinamaanisha nimepona?
Hapana.
3. Kipimo gani kinaonyesha ARV zinafanya kazi?
Viral load.
4. Naweza kuambukiza?
Viral load haipimiki – hapana kwa ngono.
5. Nipime VVU tena?
Hapana; fuatilia viral load.
6. Naweza kuacha ARV?
Hapana.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:07:19
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
World Health Organization. Consolidated guidelines on HIV prevention, testing, treatment, service delivery and monitoring. Geneva: WHO; 2021.
World Health Organization. The role of HIV viral suppression in improving individual health and reducing transmission: policy brief. Geneva: WHO; 2023.
Rodger AJ, et al. Risk of HIV transmission through condomless sex in serodifferent gay couples with the HIV-positive partner taking suppressive antiretroviral therapy (PARTNER): final results. Lancet. 2019;393(10189):2428–38.

