Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dkt. Lusenge S, MD
Dkt. Sospeter M, MD
2 Aprili 2026, 16:07:15

Mstari mweusi chini ya kitovu kwa mwanamke
Misuli ya tumbo imeunganishwa katikati ya tumbo kwa tishu ngumu unganishi zinazoitwa linea alba. Sehemu ya muunganiko wa tishu hizo huonekana mithiri ya mfereji au utepe unaopita katikati ya tumbo haswa kwa watu wanaojenga misuli ya tumbo (tazama picha chini).

Tishu unganishi hii huwa na chembe za melanini, chembe hizi hubadilika kuwa nyeusi kuitikia ongezeko la homoni melanini kwenye damu. Sababu yoyote inayopelekea ongezeko la homoni melanini kwenye damu hupelekea utepe wa linea alba kuwa mweusi na hivyo kuonekana nje kama mstari mweusi unaofahamika kama linea nigra.
Nini husababisha mstari mweusi chini ya kitovu?
Mstari mweusi chini ya kitovu husababishwa na mabadiliko ya homoni ambayo husababisha kuongezeka kwa vichochezi vya melanini ambayo huleta rangi nyeusi.Hali hii huisha pale uwiano wa homoni unapokuwa sawa.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 16:07:15
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
​
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
