Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
Dkt. Lugonda B, MD
31 Oktoba 2026, 15:23:37

Uume kutoa harufu mbaya: Visabaishi, Vipimo na Matibabu
Jibu kwa ufupi
Jibu kwa ufupi: Osha kila siku kwa maji ya uvuguvugu, vuta govi nyuma, kausha vizuri. Harufu pamoja na usaha, maumivu ya kukojoa au wekundu – pima magonjwa ya zinaa na sukari. Soma Kuchubuka ngozi ya uume.
Maelezo
Visababishi
Smegma – nyeupe, chini ya govi.
Balanitis – fangasi/bakteria; wekundu, kuwasha; soma Kuwashwa uume.
Gono, klamidia, trikomonasi – usaha, kuchoma kukojoa.
UTI – mkojo wenye harufu.
Govi kubana – ngumu kusafisha.
Jasho, nguo zisizopitisha hewa.
Uchunguzi na tiba
Uchunguzi; usaha kwa hadubini; mkojo.
Sukari ya damu.
Fangasi – krimu ya fangasi.
Bakteria/zinaa – antibayotiki za mwongozo; mwenza pia.
Govi kubana au balanitis inayojirudia – ushauri wa tohara.
Nini cha kufanya
Osha kila siku; sabuni isiyo na manukato pembeni.
Kausha kabla ya kuvaa.
Chupi za pamba; badilisha kila siku.
Kondomu kwa wapenzi wapya.
Mabaka – soma Mabaka kwenye uume.
Dalili za hatari
Govi kukwama nyuma, uume kuvimba – hospitali mara moja.
Homa, maumivu makali, usaha mwingi – hospitali.
Lini umwone daktari
Harufu inayoendelea licha ya usafi.
Usaha, kuchoma kukojoa – pima zinaa.
Fangasi zinazojirudia – pima kisukari.
Madoa – soma Madoa kwenye uume.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
1. Kwa nini uume hutoa harufu hata nikioga?
Smegma, fangasi au maambukizi; vuta govi nyuma ukisafisha.
2. Ni ugonjwa wa zinaa?
Si mara zote; usaha au maumivu – pima.
3. Sabuni gani?
Isiyo na manukato, au maji tu.
4. Tohara inasaidia?
Hupunguza smegma na balanitis.
5. Kisukari kinahusika?
Ndiyo, fangasi hujirudia.
6. Mwenza atibiwe?
Kwa magonjwa ya zinaa – ndiyo.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:07:23
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
Edwards SK, Bunker CB, Ziller F, van der Meijden WI. 2013 European guideline for the management of balanoposthitis. Int J STD AIDS. 2014;25(9):615–26.
Workowski KA, et al. Sexually Transmitted Infections Treatment Guidelines, 2021. MMWR Recomm Rep. 2021;70(4):1–187.
Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.

