Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
ULY CLINIC
31 Oktoba 2026, 15:23:37
Wiki gani hedhi itarejea baada ya kutoa mimba?
Jibu kwa ufupi
Jibu kwa ufupi: Wiki 4 hadi 6 kwa wengi. Anza uzazi wa mpango mara moja – mimba inaweza kutokea kabla ya hedhi kurudi. Soma Kupata ujauzito baada ya kutoa mimba.
Maelezo
Kwa nini hedhi inaweza kuchelewa
Homoni za ujauzito huchukua muda kushuka.
Mimba kubwa zaidi – muda zaidi.
Njia iliyotumika – dawa au usafishaji.
Msongo, uchovu, ugonjwa.
Mimba mpya.
Mara chache – makovu ndani ya kizazi baada ya kusafishwa (Asherman).
Dalili kwamba mwili unarudi kawaida
Damu ya baada ya mimba kupungua na kuisha.
Ute wa kawaida wa uke kurudi.
Ute wa uovuleshaji (kama yai bichi) – soma Siku salama baada ya kutoa mimba.
Nini cha kufanya
Andika tarehe ya mimba kutoka na ya hedhi ya kwanza.
Anza uzazi wa mpango – soma Uzazi wa mpango baada ya kutoa mimba.
Pima mimba kama hedhi haijarudi wiki 6 na ulifanya tendo bila kinga.
Dalili za hatari
Nenda kituo cha afya mara moja ukiwa na:
Damu nyingi sana.
Maumivu makali ya tumbo.
Homa au uchafu wenye harufu mbaya.
Lini umwone daktari
Hedhi haijarudi wiki 6 hadi 8.
Hedhi ya kwanza ni kidogo sana au haipo kabisa baada ya kusafishwa kizazi.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
1. Hedhi hurudi lini baada ya kutoa mimba?
Kwa wengi ndani ya wiki 4 hadi 6.
2. Naweza kupata mimba kabla ya hedhi kurudi?
Ndiyo, uovuleshaji unaweza kutokea wiki 2 baadaye.
3. Hedhi ya kwanza huwa nzito?
Inaweza kuwa nzito kidogo au tofauti; hurudi kawaida mizunguko inayofuata.
4. Wiki 8 bila hedhi, nifanyeje?
Pima mimba na mwone mtoa huduma.
5. Hedhi ni kidogo sana tangu nisafishwe, ni nini?
Mara chache makovu ndani ya kizazi – mwone mtoa huduma.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 17:07:30
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.
World Health Organization. Abortion care guideline. Geneva: WHO; 2022.

