top of page

Maelezo ya majibu ya maswali mbalimbali ya kiafya

Kinga ya kiungulia

Kiunguliwa kinaweza kukingwa kwa kutumia dawa za kupunguza uzalishaji wa tindikali, kuepuka kulala angalau masaa 2 baada ya kula, kuepuka vyakula vyenye viungo vingi n.k

Matibabu ya presha pasipo dawa

Kuna njia nyingi unaweza tumia kushusha shinikizo la damu endapo hutaki tumia dawa;
Kwa kula vyakula vyenye mboga za majani kwa wingi, matunda na mbegu. Fuata ushauri wa mlo maalumu kama ilivyoelezewa katika makala hii. Kumbuka kwenye makala hii imeelezewa taarifa za awali tu, taarifa zaidi zinapatikana kwa madaktari wa ULY CLINIC.

Matibabu ya maumivu ya koo

Maumivu ya koo ni dalili ya hisia za kuhisi maumivu, ukavu au kukwanguliwa kwa koo. Tatizo hili huwapata watu wengi duniani.

Mara nyingi maumivu ya koo husababishwa na maambukizi ya virusi na hewa kavu kwenye mazingira na mara nyingi dalili hii hupotea yenyewe bila matibabu.

Presha ya kushuka matibababu ya nyumbani

Presha ya kushuka huitwa kitiba kama hypotension, endapo una presha ya kushuka ni vema kufahamu ni nini kisababishi cha presha yako. Aina kadhaa za presha ya kushuka zinafahamika, ambazo zimezungumziwa kwenye makala hii na matibabu yake ya nyumbani ni
• Kuwa makini unapokuwa unaamka,
• Presha ya kushuka unapoamka asubuhi na mapema,
• Presha ya kushuka baada ya kula,
• Presha kushuka unapolala chali
• Presha ya kushuka kutokana na upungufu wa damu

Chakula cha mgonjwa wa saratani

Saratani ni mkusayiko wa magonjwa mengi yanayotokana na kushindwa kwa udhibiti dhidi ya uzalishaji na ukuaji wa seli mwilini. Sifa kuu ya seli za saratani ni kukua kwa haraka zaidi na kusambaa sehemu yoyote ile ya mwili.

Tiba ya kukojoa kitandani

Ili kuacha kukojoa kitandani, matumizi ya dawa haitakiwi kuwa uchaguzi wa kwanza, njia asili za kuufunza ubongo wa mtoto au mtu mzima zinatakiwa kutumika ili kuleta majibu mzuri na yanayodumu. Makala hii imezungumzia tiba isiyo dawa ya kukojoa kitandani.

bottom of page