Maelezo ya majibu ya maswali mbalimbali ya kiafya

Vasograin inatibu nini?
Vasograin ni kidonge chenye mchanganyiko wa ergotamine, kafeini, paracetamol na prochlorperazine, kinachotumika kutibu shambulio la kipandauso (migraine) na baadhi ya maumivu ya kichwa ya mishipa ya damu. Hutolewa kwa cheti cha daktari. Kutumia mara nyingi huleta maumivu ya kichwa ya kudumu, na haifai kwa wajawazito, wenye magonjwa ya moyo na presha, wala wanaotumia baadhi ya ARV na antibiotiki.

Dawa za kutumia baada ya kutoa mimba
Baada ya mimba kutoka au kutolewa, dawa hutolewa kulingana na hali ya mwanamke, si kila dawa kwa kila mtu. Dawa za maumivu kama ibuprofen hufanya kazi vizuri kwa maumivu ya kizazi, na paracetamol ni mbadala; aspirini iepukwe kwa sababu huongeza damu. Antibayotiki za kinga hutolewa kwa wanaosafishwa kizazi kwa njia ya upasuaji mdogo kama kufyonza kwa mrija (MVA); kwa waliotoa mimba kwa dawa, antibayotiki hazihitajiki kwa kawaida isipokuwa kuna dalili za maambukizi.

Kuwashwa wakati wa kukojoa kwa wanawake: Sababu, Tiba na Tahadhari
Kuwashwa sehemu za siri mkojo unapogusa ngozi mara nyingi hutokana na fangasi ukeni, trikomonasi, mzio au muwasho wa sabuni, pedi zenye manukato na dawa za kuosha uke, ngozi kavu au michubuko ya kujikuna, herpes, na magonjwa ya ngozi kama lichen sclerosus. UTI kwa kawaida huleta kuchoma ndani zaidi ya kuwasha, pamoja na kukojoa mara kwa mara. Kubadilisha sabuni na kujisafisha zaidi mara nyingi huzidisha tatizo. Uchunguzi wa ute na mkojo huonyesha chanzo; tiba ya kubahatisha huchelewesha kupona.

Maumivu ya kudumu kwenye kitovu kwa mwanamke: Visababishi, Uchunguzi na Msaada wa haraka
Mfano: mwanamke wa miaka 29 mwenye maumivu ya kitovu kwa miezi 2, yanayoongezeka akibonyeza, na kitovu kuvimba kidogo baada ya kula – hii inaelekeza zaidi kwenye ngiri ya kitovu. Visababishi vya maumivu ya kitovu kwa mwanamke: ngiri ya kitovu (hasa waliojifungua au wenye uzito mkubwa – kuvimba ukisimama au kukohoa), endometriosis ya kitovu (nadra – maumivu na uvimbe wa bluu-zambarau unaoongezeka au kutoa damu wakati wa hedhi), maambukizi ya kitovu au mabaki ya urachus (uchafu, harufu), kidole tumbo cha mwanzo (maumivu huanzia kitovuni kisha kuhamia kulia chini), vidonda vya tumbo, sisti ya ovari na mimba nje ya kizazi. Vipimo ni uchunguzi wa mwili, kipimo cha mimba, mkojo na ultrasound ya tumbo na ukuta wake. Ngiri iliyokwama – ngumu, nyekundu, isiyorudi ndani na kutapika – ni dharura ya upasuaji.

Visababishi vya Maumivu ya tumbo- Wanaume: Kikokotoo
Kikokotoo hiki ni cha elimu: kinaonyesha visababishi vinavyowezekana vya maumivu ya tumbo kwa wanaume kulingana na eneo na sifa za maumivu, ili kuonyesha kwa nini daktari huhitaji historia, uchunguzi na vipimo – si kutoa utambuzi. Kwa wanaume, mbali na mfumo wa chakula na mkojo, maumivu ya tumbo la chini huweza kutoka kwenye korodani (kujisokota – dharura), ngiri, tezi dume, na kwa wazee mshipa mkubwa wa damu (aorta). Maumivu ya juu ya tumbo huweza kuwa ya moyo, hasa pamoja na jasho na kubanwa pumzi.

Muda wa kushiriki Ngono bila Kinga wakati wa kutumia Uzazi wa Mpango
Muda wa kusubiri kabla ya ngono bila kondomu hutegemea njia na siku uliyoanza (WHO 2022). Kitanzi cha shaba – kinga mara moja. Vidonge vya mchanganyiko – mara moja ukianza ndani ya siku 5 za mwanzo wa hedhi; vinginevyo siku 7 za kondomu. Vidonge vya projestini pekee – siku 2 za kondomu (mara moja ndani ya siku 5 za hedhi). Sindano ya Depo, kipandikizi na kitanzi cha homoni – mara moja ukianza ndani ya siku 7 za mwanzo wa hedhi; vinginevyo siku 7 za kondomu. Kumbuka: hakuna njia ya homoni wala kitanzi kinachokinga magonjwa ya zinaa na VVU – kondomu ndiyo hulinda.
