top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

Dkt. Mangwella S, MD

Dkt. Peter A, MD

31 Oktoba 2026, 15:23:37

Vasograin inatibu nini?

Jibu kwa ufupi


Jibu kwa ufupi: Vasograin hutibu shambulio la kipandauso likianza. Si dawa ya kila maumivu ya kichwa, na haipaswi kutumika mara nyingi kwa wiki. Tumia kwa ushauri wa daktari tu.


Maelezo


Viambato na kazi zake


  • Ergotamine – hubana mishipa ya damu iliyopanuka kichwani wakati wa kipandauso.

  • Kafeini – huongeza ufanisi wa ergotamine.

  • Paracetamol – hupunguza maumivu.

  • Prochlorperazine – hupunguza kichefuchefu na kutapika vinavyoambatana na kipandauso.


Maudhi


  • Kichefuchefu, kizunguzungu, usingizi.

  • Ganzi au kuwashwa vidole, miguu kuuma.

  • Kutumia mara nyingi – maumivu ya kichwa yanayotokana na dawa yenyewe (medication-overuse headache) na utegemezi.


Wasiotakiwa kutumia


  • Wajawazito na wanaonyonyesha.

  • Wenye magonjwa ya moyo, presha isiyodhibitiwa, magonjwa ya mishipa ya damu, ini au figo.

  • Wanaotumia ARV zenye ritonavir au cobicistat, au antibiotiki kama erythromycin na clarithromycin – mchanganyiko huu huweza kubana mishipa kupita kiasi (ergotism) na kuharibu vidole au viungo.

  • Wanaotumia dawa nyingine za kipandauso za aina ya triptan siku hiyo hiyo.


Nini cha kufanya


  • Tumia kwa cheti cha daktari na kwa maelekezo yake.

  • Mwambie daktari dawa zote unazotumia, hasa ARV na antibiotiki.

  • Kama unapata kipandauso mara nyingi (zaidi ya mara 4 kwa mwezi), uliza kuhusu dawa za kuzuia mashambulizi.

  • Andika siku za maumivu na vichochezi (usingizi mdogo, msongo, vyakula fulani) – soma Maumivu ya kichwa.


Dalili za hatari


Acha dawa na nenda hospitali mara moja ukiwa na:


  • Vidole vya mikono au miguu kuwa baridi, vyeupe au bluu, na maumivu.

  • Maumivu ya kifua.

  • Udhaifu wa upande mmoja wa mwili, kuongea kwa shida.

  • Maumivu makali ya ghafla ya kichwa – "makali kuliko yote maishani".


Lini umwone daktari


  • Unahitaji Vasograin zaidi ya siku 2 kwa wiki.

  • Maumivu ya kichwa yamebadilika au ni ya kila siku.

  • Umepata mimba ukiwa unatumia Vasograin.


Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Vasograin inatibu maumivu yoyote ya kichwa?

Hapana. Ni kwa kipandauso na baadhi ya maumivu ya mishipa ya damu.

2. Naweza kutumia Vasograin kila siku?

Hapana. Matumizi ya mara kwa mara huleta maumivu ya kichwa ya kudumu na madhara mengine.

3. Natumia ARV, naweza kutumia Vasograin?

Mwambie daktari kwanza – baadhi ya ARV zikichanganywa na ergotamine ni hatari.

4. Mjamzito anaweza kutumia Vasograin?

Hapana. Ergotamine inaweza kuharibu mimba.

5. Vasograin inapatikana bila cheti?

Inapaswa kutolewa kwa cheti cha daktari.

6. Nimetumia Vasograin na vidole vimekuwa baridi, nifanyeje?

Acha dawa na nenda hospitali mara moja.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 19:07:19

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.

  2. Mahajan A, et al. Prolonged abuse of Vasograin tablets. Indian J Priv Psychiatry. 2018;12(1):27–8.

  3. Ausband SC, Goodman PE. An unusual case of clarithromycin associated ergotism. J Emerg Med. 2001;21(4):411–3.

  4. Diener HC, et al. Pathophysiology, prevention, and treatment of medication overuse headache. Lancet Neurol. 2019;18(9):891–902.

bottom of page