Magonjwa ya ngozi
​
Soma kuhusu magonjwa ya ngozi hapa, endapo una tatizo lolote la ngozi na unahitaji ushauri na tiba popote pale ulipo wasiliana nasi hapa au pata tiba hapa
Tinea manuum ni jina la ugonjwa wa fangasi unaodhuru mikono tu na hutokea kwa nadra sana ukilinganisha na fangasi wa kanyagio wenye jina la tinea pedis.
Soriasis ni ugonjwa sugu wa ngozi unaotokana na michomo endelevu ya kinga za mwili za mtu. Ugonjwa husababisha mwonekano wa unaoeleweka wa maeneo wa wekundu, magamba(ngozi kuwa nene).
Kubanduka kwa ngozi ya kiganja cha mkono kitabibu ikifahamika kwa jina la Keratolisis eksifoliativa au jina jingine la lamela dishaidrosis ni udhaifu wa ngozi ya kiganja cha mkono inayopelekea ngozi kubanduka. Tatizo hili hujirudia mara kadhaa na huweza kuathiri vidole vya mkono, kanyagio na huamswha sana kwa watu wengi kwenye majira ya kiangazi au hali ya hewa ya ujoto.
Ngozi kukauka mara nyingi husababishwa na vitu vya kawaida kama hali ya hewa ya umoto au baridi, kuloweka ngozi kwenye maji ya moto na kukosekana kwa unyevu kwenye ngozi. Visababishi hivi vinavyojulikana huweza kutubika kwa njia ambazo mtu anaweza kuzifanya nyumbani. Hata hivyo baadhi ya watu hupata tatizo kubwa linaloogopesha na kufanya waende hospitali kuonana na daktari wa ngozi.
Ngozi kubanduka na ngozi kuwa na magamba hutokea kutokana na sababu mbalimbali zinazoendelea kwenye ngozi, sababu hizo zinaweza kuwa kwa sababu za kawaida kama vile kuchomwa na mwanga wa jua au sababu zinazotokana na magonjwa ndani ya mwili.
EPD ni aina mojawapo ya magonjwa ya ngozi ya kurithi yanayoipa ngozi mabaka yenye sura kama yai au kutokuwa na mipaka ya kueleweka na yenye rangi ya kijivu au blue iliyokolea kuelekea nyeusi. EPD huweza kutokea shingoni, usoni, na katika kiwiliwili.
Ni tatizo la ngozi ambalo husababisha ngozi iwe nyekundu(kwa watu weupe), iwashe na kupata vipele vinavyosababishwa na aleji na kitu Fulani. Tatizo hili ni miongoni mwa aina ya pumu ya ngozi lakini yenyewe husababishwa na mgusano wa ngozi na kitu Fulani.
Ulimi wa jiografia au ulimi ramani ni tatizo linalotokana na michomo ya ulimi inayoletwa na kinga za mwili na huathiri sakafu ya ulimi. Tatizo hili halina madhara yoyote kwenye ulimi wako, tafiti zinaonyesha tatizo hili huambatana pumu ya Ngozi, licheni planas na soriasisi