Maana ya Dimenshia
Imeandikwa na madaktari wa ulyclinic
Dimenshia ni jina la kundi za dalili na viashiria ambazo hujumuisha kuwa na matatizo ya kumbukumbu, fikra, kushindwa kutatua matatizo, kusahau lugha na mtazamo kubadilika. Dalili hizi hujitosheleza katika kudhuru au kuharibu ubora wa maisha ya mtu
Dimenshia sio ugonjwa na sio sehemu ya uzee, bali husababishwa na magonjwa mbalimbali yanayodhuru mishipa ya fahamu kwenye ubongo wa binaddamu yakiwemo magonjwa nje ya ubongo Magonjwa/matatizo yanayoweza kuleta dalili hizi huwa zaidi ya 60 hadi 70.
Dimeshia huwa endelevu ikimaanisha linaendelea jinsi mda unavyoenda na pia dalili huwa kali Zaidi jinsi mda unavyoenda. hii ni kwa sababu uhalibifu katika mishipa ya fahamu ya ubongo ikishatokea huwa endelevu na haizalishwi mingine tena kukabili uharibifu huo
Kuna aina mbili za Dimenshia, huweza kuwa ya kujirudia au ile endelevu
​
imechapishwa 24/10/2016
imepitiwa 24/10/2018