Imeandikwa na ULY CLINIC
26 Februari 2021, 14:35:32
Kutapika
Ni kitendo cha kutoa nje chakula au maji maji yaliyo jikusanya tumboni kupitia mdomo au wakati mwingine kupitia pua.
Kitendo hiki kufanyika kwa haraka na kuweza ambatana na maumivu katikati ya kifua na kutanguliwa na kichefuchefu. Kutapika kunaweza kuwa ni njia ya tumbo kuondoa sumu ulinzi wa tumbo dhidi ya sumu. Dalili zanazoweza ambatana na kutapika ni kupumua kwa haraka haraka ,maumivu ya kichwa, kuharisha au mapigo ya moyo kwenda mbio. Kutapika pia kunaweza kuwa ni ishara ya hali ya ugonjwa ulio mwilini.
Visababishi
Kizungu zungu
Matumizi ya dawa za uzazi wa mpango
Kuziba kwa utumbo
Kichefuchefu
Kukua kwa bandama (spleno megali)
Kula kupita kiasi
Harufu mbaya
Ulaji wa sumu
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba' chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
7 Februari 2022, 19:33:54
Rejea za mada hii
1. Di Lorenzo C. Approach to the infant or child with nausea and vomiting. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 26.02.2021
2. Longstreth GF. Approach to the adult with nausea and vomiting. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 26.02.2021
3. .Nausea and vomiting. Merck Manual Professional Version. http://www.merckmanuals.com/professional/gastrointestinal-disorders/symptoms-of-gi-disorders/nausea-and-vomiting. Imechukuliwa 26.02.2021
4. WebMd.Vomiting.https://www.webmd.com/digestive-disorders/digestive-diseases-nausea-vomiting. Imechukuliwa 26.02.2021