Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
Dkt. Adolf S, M.D

15 Februari 2026, 06:55:11
Dalili za UTI kwa watu wazima
Mfumo wa mkojo umegawanyika katika sehemu kuu mbili, mfumo wa mkojo wa chini na mfumo wa mkojo wa juu, mfumo wa chini umetengenezwa na mrija wa urethra, kibofu cha mkojo na mirija miwili ya yureta.
Mfumo wa juu wa mkojo umeundwa na figo ambazo huchuja maji mwilini na kutengeneza mkojo.
Maambukizi mfumo wa juu ya mkojo hutokea endapo maambukizi ya mfumo wa chini wa mkojo yamesambaa na kwenda kwenye figo. Maambukizi kwenye figo huwa hatari sana kwani yanaweza kusababisha bakteria kuingia kwenye damu kwa kuwa damu nyingi hupita kwenye figo kwa ajili ya kuchujwa. Hata hivyo maambukizi ya mfumo wa juu wa mkojo huleta dalili kali na hutishia uhai wa mtu.
Kazi kubwa ya mfumo wa mkojo ni kuondoa sumu, uchafu na maji ya ziada mwilini
Ni vimelea gani husababisha uti?
Uti kwa asilimia zaidi ya 90 husababishwa na bakteria ainayeitwa ya escherichia coli ambaye hupatikana katika mfumo wa chakula. Bakteria wengine wanaoweza kusababisha uti ni pamoja na enterococcus faecalis, enterobacteriaceae na staphylococcus saprophyticus, na wakati mwingine uti inaweza kusababishwa na fangasi . Bakteria aina ya Staphylococcus Saprophyticus huleta maambukizi kwa wasichana wadogo na dalili zake huamka haraka sana.
Dalili za UTI ya mfumo wa chini wa mkojo
Hizi ndizo dalili zinazotokea mara nyingi kwa wanawake na wanaume.
Maumivu na hisia wakati wa kukojoa
Maumivu au kuungua wakati wa kukojoa
Kukojoa mara kwa mara
Hamu ya kukojoa ghafla
Mkojo kutoka kidogo kidogo kila unapokwenda chooni
Kuhisi bado una mkojo hata baada ya kukojoa
Mabadiliko ya mkojo
Harufu kali isiyo ya kawaida
Mkojo kuwa wa mawingu au mchafu
Mkojo kuwa wa njano iliyokolea
Wakati mwingine damu kidogo kwenye mkojo
Maumivu ya tumbo
Maumivu chini ya kitovu
Uzito au kubana sehemu ya nyonga
Kuchoma sehemu ya kibofu
Dalili za mwili mzima (huweza kuwepo au kukosekana)
Uchovu
Homa ndogo
Kichefuchefu kidogo
Dalili za UTI ya mfumo wa juu wa mkojo (Maambukizi ya figo)
Hii ni hali hatari zaidi na huhitaji matibabu ya haraka.
Maumivu makali
Maumivu ya mgongo upande wa mbavu (flank pain)
Maumivu ya kiuno upande mmoja au pande zote
Maumivu yanayosambaa hadi tumboni mbele
Dalili za maambukizi makali
Homa kali (zaidi ya 38°C)
Kutetemeka mwili
Baridi kali
Mapigo ya moyo kwenda kasi
Dalili za tumbo
Kichefuchefu kikali
Kutapika mara kwa mara
Kukosa hamu ya kula
Dalili za mkojo
Damu kwenye mkojo
Mkojo wenye usaha
Harufu kali sana ya mkojo
Dalili hatari zinazohitaji hospitali haraka
Homa kali na maumivu ya mgongo
Kutapika kushindwa kula au kunywa
Kuchanganyikiwa au kizunguzungu
Mapigo ya moyo kwenda kasi sana
Maumivu makali yasiyovumilika
Hizi zinaweza kuashiria maambukizi yameingia kwenye damu (sepsisi).
Maswali yaliyoulizwa mara kwa mara na majibu yake
1. Je, dalili za UTI kali ni zipi?
UTI kali (maambukizi ya figo) hutokea pale maambukizi yanapopanda kutoka kibofu hadi kwenye figo. Hii huitwa pyelonephritis na ni hali hatari.
Dalili zake ni:
Homa kali (zaidi ya 38°C)
Maumivu makali ya ubavu mmoja au yote chini kidogo ya mbavu (Maumivu ya flank)
Kutetemeka mwili (baridi kali)
Kutapika mara kwa mara
Damu kwenye mkojo
Mwili kulegea sana au kuchoka kupita kiasi
Mapigo ya moyo kwenda kasi
Ikiwa hazitatibiwa mapema, bakteria wanaweza kuingia kwenye damu na kusababisha sepsis, ambayo ni dharura ya kitabibu inayoweza kutishia maisha.
UTI kali inahitaji matibabu ya haraka hospitalini.
2. Naweza kuwa na UTI bila maumivu wakati wa kukojoa?
Ndiyo. Ingawa kuungua wakati wa kukojoa ni dalili ya kawaida ya UTI, si kila mtu hupata dalili hii.
Baadhi ya watu — hasa wazee — wanaweza kupata:
Kukojoa mara kwa mara tu
Maumivu ya chini ya tumbo pekee
Uchovu au kuchanganyikiwa (kwa wazee)
Hivyo, kukosa maumivu wakati wa kukojoa hakumaanishi huna UTI.
3. UTI husababisha maumivu wapi hasa?
Mahali pa maumivu hutegemea sehemu iliyoathirika:
UTI ya kibofu (sistaitisi): maumivu chini ya kitovu
UTI ya figo: maumivu mgongoni chini ya mbavu, upande mmoja au pande zote
Maumivu ya figo huwa makali zaidi na huambatana na homa.
4. UTI inaweza kusababisha maumivu ya mgongo?
Ndiyo. Maumivu ya mgongo ni ishara kwamba maambukizi yamefika kwenye figo.
Maumivu haya:
Huwa pembeni mwa mgongo (sio katikati)
Huongezeka unapogusa eneo hilo
Huambatana na homa na kutapika
Hii si UTI ya kawaida — ni hali inayohitaji matibabu ya haraka.
5. Je, UTI husababisha harufu mbaya ya mkojo?
Ndiyo. Bakteria wanaosababisha UTI hubadilisha kemikali za mkojo na kusababisha:
Harufu kali
Harufu ya samaki
Mkojo kuwa wa mawingu au mchafu
Hata hivyo, harufu pekee bila dalili nyingine si lazima iwe UTI — inapaswa kuangaliwa pamoja na dalili nyingine.
6. Kwa nini nahisi kukojoa kila wakati lakini mkojo unatoka kidogo?
Hii hutokea kwa sababu kibofu cha mkojo huwa kimevimba na kukereketa.
Uvimbaji huu hufanya kibofu kutoa ishara ya kukojoa hata kama hakijajaa. Hivyo:
Unahisi hamu ya kukojoa ghafla
Mkojo unatoka kidogo
Hisi ya kukojoa hurudi tena muda mfupi baada ya kutoka chooni
Hii ni dalili ya kawaida ya UTI ya mfumo wa chini.
7. UTI inaweza kusababisha homa?
Ndiyo.
Homa ndogo huweza kutokea kwenye UTI ya kawaida
Homa kali huashiria maambukizi yamefika kwenye figo
Ikiwa homa inaambatana na maumivu ya mgongo au kutapika, tafuta matibabu haraka.
8. Je, damu kwenye mkojo ni dalili ya UTI?
Ndiyo. UTI inaweza kusababisha:
Damu inayoonekana wazi kwenye mkojo
Mkojo kuwa wa rangi ya pinki au kahawia
Damu kuonekana tu kwenye kipimo cha maabara
Damu hutokea kwa sababu ukuta wa kibofu huvimba na mishipa midogo kupasuka.
9. UTI inaweza kuchanganywa na PID?
Ndiyo, mara nyingi huchanganywa.
Zote husababisha:
Maumivu ya chini ya tumbo
Kukojoa mara kwa mara
Tofauti kubwa ni:
PID huambatana na maumivu wakati wa tendo la ndoa
PID huweza kuwa na uchafu ukeni
UTI huathiri zaidi dalili za mkojo
Utambuzi sahihi unahitaji uchunguzi wa kitabibu.
10. Ni lini niende hospitali haraka?
Nenda hospitali mara moja ikiwa una:
Homa kali
Maumivu ya mgongo pembeni ya mbavu
Kutapika sana
Kizunguzungu au kuchanganyikiwa
Mapigo ya moyo kwenda kasi
Kushindwa kunywa maji au kula
Hizi zinaweza kuashiria maambukizi ya figo au kuenea kwa bakteria kwenye damu (sepsisi).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeandikwa:
20 Machi 2020, 16:46:44
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1. Wein aj, et al., eds. Infections of the urinary tract. In: campbell-walsh urology. 11th ed. Philadelphia, pa.: elsevier; 2016. Https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 17.03.2020
2. Ferri ff. Urinary tract infection. In: ferri's clinical advisor 2017. Philadelphia, pa.: elsevier; 2017. Https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 17.03.2020
3. Bladder infection (urinary tract infection—uti) in adults. National institute of diabetes and digestive and kidney diseases. Https://www.niddk.nih.gov/health- information/urologic-diseases/bladder-infection-uti-in-adults. Imechukuliwa 17.03.2020
4. Urinary tract infections (utis). The american college of obstetricians and gynecologists. Https://www.acog.org/patients/faqs/urinary-tract-infections-utis. Imechukuliwa 17.03.2020
5. [Guideline] Gupta K, Hooton TM, Naber KG, et al. International clinical practice guidelines for the treatment of acute uncomplicated cystitis and pyelonephritis in women: A 2010 update by the Infectious Diseases Society of America and the European Society for Microbiology and Infectious Diseases. Clin Infect Dis. 2011 Mar. 52(5):e103-20. [Medline]. [Full Text].
6. [Guideline] Wagenlehner FM, Schmiemann G, Hoyme U, Fünfstück R, Hummers-Pradier E, Kaase M, et al. [National S3 guideline on uncomplicated urinary tract infection: recommendations for treatment and management of uncomplicated community-acquired bacterial urinary tract infections in adult patients]. Urologe A. 2011 Feb. 50(2):153-69. [Medline]. [Full Text].
