Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Adolf Salome, MD
Dkt. Sospeter B, MD
5 Aprili 2021, 11:50:54

Aina za degedege
Degedege ni dalili inayoonesha mvurugiko katika mawasiliano ya umeme katika seli za ubongo
Hali hii huwapata watu wengi, inakadiriwa kuwa mtu mmoja kati ya kumi anaweza kupata degedege wakati wa maisha yake.
Mara nyingi degedege inapotokea kwa mtu hudumu kwa dakika chache bila kuleta madhara, na mara chache huweza kuwa dharura na kuhitaji msaada wa kitabibu wa haraka.
Degedege imegawanyika katika makundi makuu mawili ambayo ni;
Degedege la jumla (generalied seizure)
Degedege la upande mmoja (partial seizure)
Degedege la jumla
Aina hii huathiri mfumo wa mawasiliano katika pande zote za ubongo hivyo dalili za degedege hutokea katika mwili wote.
Aina za degedege la jumla
Degedege la jumla la kutoonekana
Degedege la la jumla la tonik kloniki
Degedege la jumla la kutoonekana
Sifa za degedege la jumla la kutoonekana
Kupoteza fahamu au kuduwaa mara nyingi chini ya sekunde 20 tu na kisha kurejea kwa fahamu
Hudumu kwa muda usioidi dakika moja
Huweza kumtokea mtu zaidi ya mara moja kwa siku
Japokuwa mtu hupoteza fahamu, nguvu ya misuli haiathiriwi na inapotokea muathirika huwa hadondoki chini
Degedege la jumla la toniki kloniki
Ni aina ya degedege linalotoa viashiria muda mfupi kabla ya kutokea.
Viashiria vyake;
Maumivu ya kichwa
Hisia ya uoga,
Hisia ya harufu
Hisia ya ganzi au vitu kutembea mwilini
Kuona vitu ambavyo havipo katika uhalisia nk.
Viashira huweza msaidia mgonjwa kujua kwamba degedege litampata ndani ya muda mfupi na hivyo kuchukua tahadhari kwa mfano kukaa sehemu salama.
Dalili
Kukakamaa kwa misuli
Kupiga kelele au kulia
Kupoteza fahamu
Kutokwa na povu mdomoni
Kung’ata ulimi
Kujongea kwa misuli ya mwili pasipo hiari
Kutokwa na haja kubwa au ndogo, au vyote kwa pamoja
Degedege hili hudumu kwa muda wa dakika 1 hadi 3 .Baada ya shambulio mgonjwa hubakia katika hali ya usingizi, kuwa mkali au kupata sonona.
Degedege la upande mmoja
Huathiri sehemu moja tu ya ubongo na kupelekea dalili katika sehemu moja ya mwili badala ya mwili mzima. Huchukua muda mfupi sana kama sekunde 10 mpaka 20.
Dalili
Kucheza kwa misuli sehemu za uso, shingo au mikono
Kuhisi harufu au ladha isiyo ya kawaida
Kupoteza fahamu
Aina hii hutokea kwa namna mbili ambazo ni
Dagedege la kupoteza fahamu
Degedege pasipo kupoteza fahamu
Visababishi vya degedege
Zipo sababu nyingi zinazowea kusababisha degedege kama ifuatavyo;
Kuwepo kwa jeraha katika ubongo
Kifafa
Matumizi ya madawa ya kulevya
Homa kali (kwa watoto)
Viwango visivyo vya kawaida vya sukari na sodium katika damu
Uvimbe katika ubongo
Maambukizi ya vimelea vya magonjwa katika ubongo mfano uti wa mgongo
Kiharusi
Magonjwa ya moyo
Namna ya kumsaidia mtu mwenye degedege
Malengo ya kutoa huduma ya kwanza kwa mgonjwa mwenye degedege ni kumlinda asipate madhara wakati degedege limetokea. Watu wengi hawafahamu mambo sahihi na yasiyo sahihi kuwafanyia waliopatwa na degedege kwenye eneo la tukio, kusoma makala hii itakusaidia kufahamu mambo hayo ya muhimu. Zifuatao ni njia za kumsaidia mtu mwenye aina yoyote ya degedege
Kaa nae, na kuwa mtulivu mpaka pale degedege litakapoisha, rekodi muda degedege lilipoanza na litakapoishia ili ufahamu limedumu kwa muda gani.
Muweke sehemu salama kwa kumtoa sehemu yenye hatari kama karibu na maji, moto n.k
Fahamu zitakaporejea, mueleze nini kilichotokea kwa ufupi na kumliwaza asijisikie vibaya
Mgeuze mwathirika wa degedege alalie ubavu mmoja (pozi la kupona kama ilivyo kwenye picha) kisha weka mto au kitu laini kichwani
Piga namba ya simu ya dharura kwa msaada zaidi kutoka kwa watoa huduma za dharura karibu nawe endapo degedege limedumu zaidi ya muda wa dakika 5
Unapata wapi maelezo zaidi kuhusu degedege?
Unaweza kupata maelezo zaidi kutoka kwenye linki mblimbali ndani ya tovuti hii au linki zilizoandikwa chini ya maelezo haya au kwa kuwasiliana na daktari wako.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023, 19:53:55
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1. Centre for disease control and prevention. Seizure First Aid. https://www.cdc.gov/epilepsy/about/first-aid.htm. Imechukuliwa 04.04.2021
2. Epilepsy foundation. Tonic-clonic Seizures. https://www.epilepsy.com/learn/types-seizures/tonic-clonic-seizures. Imechukuliwa 04.04.2021
3. Epilepsy society. Epilepsy auras. https://epilepsysociety.org.uk/epilepsy-auras. Imechukuliwa 04.04.2021
4. Medicine. What Is the First Aid for Seizures?. https://www.medicinenet.com/first_aid_for_seizures/article.htm. Imechukuliwa 05.04.2021
5. AJ Noble, et al. ‘Seizure First Aid Training’ for people with epilepsy who attend emergency departments, and their family and friends: study protocol for intervention development and a pilot randomised controlled trial. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4521519/. Imechukuliwa 05.04.2021
6. Bernd Pohlmann-Eden, et al. The first seizure and its management in adults and children
7. .https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC1363913/. Imechukuliwa 05.04.2021
8. Kathryn A. O'Hara. First Aid for Seizures: The Importance of Education and Appropriate Response. https://journals.sagepub.com/doi/abs/10.1177/0883073807303066. Imechukuliwa 05.04.2021
9. Seizure First Aid and Safety. https://www.epilepsy.com/living-epilepsy/seizure-first-aid-and-safety. Imechukuliwa 05.04.2021
10. Seizure First Aid. How to help someone having a seizure. https://www.epilepsy.com/sites/core/files/atoms/files/SFA%20Flier_HQ_8.5x11_PDF.pdf. Imechukuliwa 05.04.2021
11. @ULY CLINIC. Huduma ya kwanza, degedege kwa mtoto. https://www.ulyclinic.com/huduma-ya-kwanza-2/degedege-kwa-mtoto-huduma-ya-kwanza. Imechukuliwa 05.04.2021
12. @ ULY CLINIC Kifafa. https://www.ulyclinic.com/degedege. Imechukuliwa 05.04.2021