top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY clinic

Dkt. Peter A, MD

17 Aprili 2020, 17:40:00

Dalili ya mzio
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Dalili ya mzio

Mzio hutokea wakati mfumo wa kinga za mwili unaitikia vitu vigeni vyote vinapoingia kwenye mwili, mfano sumu mbalimbali, harufu za maua na poleni au baadhi ya vyakula kwa baadhi ya watu. Mfumo huu wa kinga za mwili ni muhimu sana kwani husaidia kumlinda mtu na sumu/kemikali ambazo hazihitajiki mwilini.


Hata hivyo baadhi ya watu huwa na mzio na vitu vya kawaida kama chakula, mfano dagaa, samaki, ngano n.k ambapo watu wengine hawana aleji na hivyo vitu.


Karibia kila mtu ana aleji na kitu Fulani katika Maisha yake.


Visababishi


Aleji husababishwa na nini?


Mara kitu kigeni kinapogusa kuta za mwili wa binadamu kupitia Ngozi au mdomoni, mfumo wa kinga za mwili hutengeneza kinga zidi yake ili baadae ipate kupambana na vitu hivyo vigeni. Antibodi huitikia kwenye kitu kigeni cha namna hiyo endapo kitakuja kwa mara ya pilina kuonyesha dalili za mzio/aleji kama vile kuvimba kwa ngozi na mfumo kupumua kwa shida au kuharisha.


Ukali wa mzio hutegemea mtu na mtu, baadhi ya watu hupata mzio mkali wa anaphailatiki unaotishia Maisha yake.


Aleji nyingi huwa hazitibiki, matibabu huelekezwa kupunguza dalili dalili tu.


Dalili za mzio



Dalili za mzio hutegemea aina ya mzio na sehemu gani imeathiriwa. Mzio huweza kuathiri mfumo wa kuingiza hewa kifuani, sainazi, pua, ngozi na mfumo wa chakula. Kila sehemu huwa na dalili zake za kipekee. Mzio mkali husababisha mwitikio mkubwa wa kinga za mwili na kuleta mzio wa anafailaktiki


Dalili za mzio wa puani


Mzio wa rhinaitis (Rhinaitiz) huweza kuathiri pua na kupelekea dalili za;


  • Kupiga chafya

  • Kuwashwa kwa pua na mdomo

  • Kutokwa na maji maji puani

  • Macho kuwa mekundu au kuvimba


Dalili za mzio wa chakula


Hii huweza kusabababisha;


  • Maumivu ya mdomo

  • Kuvimba kwa ulimi, uso au kifua Pamoja na maumivu ya ulimi

  • Mzio wa anafailaksisi


Dalili za mzio kung'atwa na nyuki


Mzio wa kung'atwa na nyuki ,huweza kusabababisha;


  • Kuvimba sehemu uliyong'atwa

  • Mwili kuwasha

  • Kukohoa

  • Kifua kubana

  • Kutoa sauti wakati wa kuhema ya mlio kama filimbi

  • Kuishiwa pumzi

  • Mzio wa anafailaksisi


Dalili za mzio wa dawa


Mzio wa dawa huweza kusabababisha;


  • Ngozi kuwasha

  • Vipele na harara

  • Kuvimba uso

  • Kutoa sauti wakati wa kuhema yenye mlio kama filimbi

  • Mzio wa anafailaksisi


Dalili waanafailaksia


Baadhi ya mzio huweza kuendelea kuwa mzio wa anafailakasia, mzio huu ni mkali san ana unahitaji matibabu ya dharura. Mzio wa anafailaksia hupelekea kushuka kwa shinikizo la damu.

Dalili za mtu mwenye mzio wa anafailaksisi ni;


  • Kupoteza fahamu

  • Kushuka kwa Shinikizo la damu

  • Kutoka na vipele kwenye ngozi

  • Kizunguzungu

  • Kuhisi mapigo ya moyo

  • Mapigo ya moyo kwenda taratibu

  • Kichefuchefu na

  • Kutapika


Visababishi


Mzio wa kwenye hewa husababishwa na;

  • Poleni za maua au miti, vinyesi vya wanayama na vumbi ndani ya nyumba.

  • Baadhi ya vyakula

  • Kung'atwa na wadudu

  • Dawa mbalimbali kama dawa jamii ya Penicillin


Kinga ya mzio


Kujiepusha na mzio, kukaa mbali na visababishi na kutokula au kutumia dawa zinazosababisha mzio.

​

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

19 Julai 2023, 20:02:52

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

​

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1.MayoClinic.Allergy.https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/allergies/symptoms-causes/syc-20351497. Imechukuliwa 17/4/2020

2.HealthLine.AllergySymptoms.https://www.healthline.com/health/allergies. Imechukuliwa 17/4/2020

3.WebMd.Allergy.https://www.webmd.com/allergies/guide/allergy-symptoms-types. Imechukuliwa 17/4/2020

4.Davidson’s Essential of medicine Edited by Alastair Innes ISBN 9780702030000 Ukurasa wa 23

bottom of page