Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Mangwella S, MD
29 Juni 2021, 19:11:20
Dalili za amibiasis
Amibiasis ni ugonjwa unaosababishwa na protozoa aina ya amiba mwenye jina la Entamoeba Histolytica. Kimelea huyu huambukizwa kwa njia ya kula chakula kilichochanganyika na kinyesi au majimaji ya kinyesi cha mtu mwenye maambukizi hata kama hana dalili.
Kimelea huyu huambukizwa kwa njia ya kula chakula kilichochanganyika na kinyesi au majimaji ya kinyesi cha mtu mwenye maambukizi hata kama hana dalili.
Dalili za amibiasis
Dalili za amibiasis huanza kuonekana wiki 2 hadi 4 baada ya kupata maambukizi kwenye tumbo. Baadhi ya watu wanaweza kupata dalili mapema zaidi, hata hivyo ni asilimia 10 hadi 20 ya watu hupata dalili ambazo huwa kati ya zifuatazo;
Kuharisha choo cha kawaida kunakoweza kupelekea kuharisha damu
Maumivu ya tumbo
Kubana kwa tumbo
Kichefuchefu
Kupoteza hamu ya kula
Homa
Kuna dalili zingine za amibiasis?
Ndio!
Kuna dalili nyingine za maambukizi ya amiba ambazo zinaweza kuonekana endapo vimelea hawa wamevamia sehemu nyingine mbali na tumbo.
Dalili za maambukizi ya amiba kwenye Ini
Amiba anapoingia kwenye ini husababisha kutengeneza kwa usaa na kusababisha jibu lililojaa usaha, jipu hili linaweza kuwa kubwa na kusabbabisha mwonekano wa kuvimba kwa tumbo na dalili zingine.
Ugonjwa huu huitwa jipu la amiba kwenye ini ambao huwa na dalili zingine zifuatazo;
Maumivu makali ya tumbo chini ya mbavu za kulia, ya kuchoma kama kisu na endelevu
Kukohoa
Homan a kutetemeka
Kuharisha kinyesi kisicho na damu
Kutojihisi vema na uchovu
Dalili za maambukizi ya Amiba kwenye ubongo
Maambukizi ya amiba kwenye ubongo husababisha kutungwa kwa usaha na hivyo kuleta ugonjwa unaofahamika kwa jina la jibu la amiba kwenye ubongo. Dalili zake hufanana na zile za homa ya uti wa mgongo ambazo ni dalili za awali na dalili za maambukizi makali.
Dalili za awali za maambukizi ya amiba kwenye ubongo
Maumivu makali ya kichwa
Homa
Kichefuchefu
Kutapika
Kukakamaa kwa shingo
Dalili za baadae za maambukizi ya amiba kwenye ubongo
Kubadilika kwa fahamu( kuchanganyikiwa)
Kutotambua watu anaowafahamu
Kutoweza tembea wima
Degedege
Kupooza kwa mshipa wa fahamu namba VII
Kupooza sehemu ya mwili
Wakati gani wa kuwasiliana na daktari haraka unapokuwa na amibiasis
Mara nyingi maambukizi ya amiba hutibika endapo mtu atapata matibabu mapema iwezekanavyo na vimelea hawawezi sambaa kwenda sehemu hatari za mwili kama ini ubongo au kwenye moyo. ENdapo unapata dalili zifuatazo ni vema ukatafuta msaada wa daktari kwa uchunguzi na matibabu;
Kuharisha damu au kinyesi chenye kamasi
Kuharisha kunakodumu zaidi ya wiki mbili
Maumivu ya tumbo
Homa
Kuvimba kwa tumbo
Maumivu ya tumbo upande wa kulia sehemu ya juu au chini ya mbavu upande wa kulia
Wapi unaweza kupata taarifa zaidi kuhusu amibiasis?
Pata taarifa zaidi kuhusu namna maambukizi yanavyotokea, vipimo na tiba kwenye makala nyingine za ulyclinic kuhusu 'amibiasis'
Magonjwa mengine yenye dalili kama za amibiasis
Si wakati wote unapokuwa na dalili hizo ni kwamba utakuwa unaugua amibiasisi hivyo ni vema kufahamu kwamba kuna magonjwa mengine yanayoweza kuleta dalili zilizotajwa hapo juu. Magonjwa yanayofanana na amibiasis ambayo yanaweza kuleta kuharisha na wakati mwingine kuharisha damu ni;
Shigelosis
Salmonelosis
Compylobacteriosis
Maambukizi ya enteroinvasive na enterohemorrhagic Escherichia coli
Ugonjwa wa inflamatori boweli
Iskemiki kolaitiz
Madhaifu ya mwingiliano wa arteri na vein
Daivetikulaitiz
Majina mengine ya dalili za amibasis
Amibiasisi hufahamika na watu wengine kama;
Dalili za amiba
Dalili za amoeba
Dalili za amoebiasis
Dalili za amiba kwenye tumbo
Dalili za amiba kwenye ubongo
Dalili za amiba kwenye ini
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
8 Oktoba 2021, 04:52:11
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1. JY Jackson-Akers, et al. Amebic Liver Abscess. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK430832/. Imeandikwa 29.06.2021
2. William A Petri, et al. Entamoeba histolytica brain abscess. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/23829905/. Imeandikwa 29.06.2021
3. CDC. Amebic Meningitis. https://www.cdc.gov/meningitis/amebic.html. Imeandikwa 29.06.2021
4. Amebic pericarditis . https://www.medscape.com/answers/212029-38511/what-is-amebic-pericarditis. Imeandikwa 29.06.2021
5. Amoebiasis : Diagnosis, symptoms, complications and management. https://www.aimu.us/2016/07/10/amoebiasis-diagnosis-symptoms-complications-and-management/. Imeandikwa 29.06.2021
6. William A. Petri, Jr, et al. Diagnosis and Management of Amebiasis. https://academic.oup.com/cid/article/29/5/1117/337264. Imeandikwa 29.06.2021