top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Adolf S, M.D

20 Machi 2020 16:19:42

Dalili za homa ya Ini
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Dalili za homa ya Ini

Ugonjwa unatokeaje?

Maambukizi ya virusi vya hepataitiz hupelekea michomo kwenye ini kutokana na shambulio la virusi hao kwenye chembe za ini. Shambulio hili hupelekea kutokea kwa dalili mbalimbali ambazo zimeorodheshwa kwenye mada hii.


Hii kupelekea Ini kupata shida na kuvimba na kushindwa kufanya kazi vizuri. Hii hali huitwa Homa ya Ini au hepatitis.


Aina za virusi vya homa ya Ini


Kuna Aina 5 ya Virus vya homa ya Ini na hivyo kuna aina 5 za hepataitiz inayosababishwa na virusi


  • Kirusi cha Hepataitiz A, husababisha Hepataitis A

  • Kirusi cha Hepataitiz B, husababisha Hepataitis B

  • Kirusi cha Hepataitiz C, husababisha Hepataitis C

  • Kirusi cha Hepataitiz D, husababisha Hepataitis D


Kirusi cha Hepataitiz A na E

Huambukizwa kupitia chakula, maji ambayo hayako salama kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.


Kirusi cha Hepataitiz B na C

Huambukizwa kwa kupitia damu, majimaji mfano shahawa, majimaji ukeni kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.


Dalili za homa ya virusi vya ini


Zipo katika makundi (2) mawili


  • Dalili za muda mfupi

  • Dalili za za usugu


Dalili za muda mfupi za homa ya virusi vya ini

Dalili hizi za mwanzo hutokea ndani ya miezi 6 baada ya kuambukizwa virusi vya homa ya Ini, hutokea kwa baadhi ya watu hazitokei kwa kila mtu.


  • Maumivu ya tumbo

  • Uchovu

  • Kupoteza hamu ya kula

  • Mgonjwa kupungua uzito

  • Manjano

  • Mkojo kuwa na rangi ya koka kola


Dalili za usugu

Mgonjwa mwenye maambukizi ya kudumu ya virusi vya homa ya Ini dalili huonekana pale ambapo ugonjwa umekolea mwilini, Na kadri muda unavyoenda virusi husababisha tatizo la sirosisi (ni kusinyaa) na kushindwa kufanya kazi vizuri, ugonjwa wa silosisi husababisha Ini kushindwa kufanya kazi na wagonjwa wengi wenye tatizo hili huwa na hatari ya kupata saratani ya ini baada ya miaka kadhaa.


  • Uchovu wa mwili

  • Dalili za kutokwa na mafua

  • Kutoa haja kubwa iliyopauka

  • Mkojo mweusi kama soda ya koka kola

  • Kupoteza hamu ya kula

  • Kupungua uzito bila sababu ya msingi

  • Manjano kwenye Ngozi na macho

  • Wakati mwingine manjano kwenye mate na mkojo


Dalili sugu huweza kutokea endapo mgonjwa hajapata tiba, badhi ya virusi huweza kuleta dalili sugu kama hepataitis A na B, dalili sugu hutokea endapo maambukizi ya virusi yamedumu kwa muda Zaidi ya miezi sita.


Baadhi ya dalili sugu ni;

  • Manjano endelevu

  • Kuvimba tumbo

  • Misuli kulegea

  • Mkojo uliopauka

  • Kuumia kirahisi na kutokwa na damu muda mrefu

  • Kutokwa na damu bila sababu

  • Kukanganyikiwa

  • Kupungua uzito

  • Kifo

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

19 Julai 2023 20:04:25

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

​

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1.Centers for Disease Control and Prevention. (2016). Hepatitis B and the vaccine (shot) to prevent it: Fact sheet for parents [Fact sheet]. cdc.gov/vaccines/vpd-vac/hepb/fs-parents.html. Imechukuliwa 17.03.2020
2.Cropley A, et al. (2017). The use of immunosuppression in autoimmune hepatitis: A current literature review. DOI: doi.org/10.3350/cmh.2016.0089
3.Heidelbaugh JJ, et al. (n.d.). Cirrhosis and chronic liver failure: Part II. Complications and treatment. aafp.org/afp/2006/0901/p767.html
4.Heidrich B, et al. (2013). Treatment options for hepatitis delta virus infection [Abstract]. DOI: 10.1007/s11908-012-0307-z

bottom of page