Mwandishi:
Mhariri:
ULY Clinic
25 Juni 2020 18:20:59
Dalili za kifafa
Kifafa huelezewa kuwa ni degedege la kujirudia rudiarudia, degedege hili husababisha mwili kojongesha misuli bila hiaria mithiri ya mtu aliye na pepo au kupigwa na shoti ya umeme.
Kifafa kinaweza kuwapata watu wakubwa, watoto wadogo, jinsia yeyote na katika umri wowote.
Vihatarishi vya kupata kifafa
Kukosa usingizi kwa muda mrefu
Kuwa na historia ya kifafa kwenye ukoo au familia
Msongo wa mawazo
Taa za kimurimuri mfano televisheni, Taa za Disko
Kutokunywa dawa za kifafa kama ulivyopangiwa na mtaalamu wa afya
Matumizi ya dozi kubwa ya dawa kama haloperidol,chlorpromazine
Matumizi ya pombe na dawa za kulevya kama vile kokeini
Kiwango kidogo cha sukari mwilini
Visababishi vya kifafa
Kwa watoto wachanga/wadogo
Sababu za kimaumbile
Kasoro/matatizo wakati wa kuzaliwa mfano kukosa hewa oksijeni wakati wa kuzaliwa
Homa ya Uti wa mgongo
Majeraha ya wakati wa kuzaliwa
Matatizo ya mishipa ya fahamu
Saratani au uvimbe ndani ya fuvu la kichwa
Homa kali za mara kwa mara
Kwa vijana na umri wa kati
Jeraha kichwani
Saratani ya ubongo
Magonjwa ya mfumo wa fahamu
Kwa wazee
Kiharusi
Matatizo katia mfumo wa neva
Saratani ya ubongo
Majeraha kichwani
Dalili za kifafa
Kuchanganyikiwa kwa muda
Mijongeo ya misuli ya mwili isiyo ya hiari
Kupoteza fahamu
Kutoelewa mazingira
Dalili za ukichaa kama hofu, shauku kuu
Dalili za déjà vu
Dalili zinazoambatana na kifafa
Dalili zingine zinazoambatana ni
Mkojo au kinyesi kutoka chenyewe
Kutokwana povu mdomoni
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
8 Oktoba 2021 04:52:13
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1.MOHSW (2005). Tanzania National Formulary. Dar es Salaam, Tanzania: Ministry of Health and Social Welfare.
2.Braunwald, E. & Fauci, A.S. (2001). Harrison’s Principles of Internal Medicine. McGraw Hill
3.Boom, N. A., Colledge, N.R., Walker, B.R. et al. (2006). Davidson’s Principles and Practices of Medicine. Churchill, Livingstone.
4.Fischer, J.H. (1994). The Epilepsy Counseling Guide. Fair Lawn: New Jersey