top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Adolf S, M.D

29 Machi 2020 10:16:33

Dalili za mtu aliyekufa
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Dalili za mtu aliyekufa

Ni nini maana ya kifo?

Kifo au kufa ni kusimama endelevu kwa kazi zote za kibayolojia mwilini zinazompa kiumbe uhai. Zipo sababu mbalimbali zinazosababisha kifo, ikiwa pamoja na magonjwa na ajali mbaya.


Kitiba kuna aina mbili za kifo, kifo cha sehemu zote za ubongo ikiwa pamoja na shina la ubongo, au kifo cha ubongo kisichohisisha shina la ubongo. Endapo mtu amekufa lakini shina la ubongo bado linafanya kazi mtu mtu huyu mapigo yake ya moyo na upumuaji unaweza endelea. Sehemu hii tumezungumzia kifo kikimaanisha kifo cha ubongo pamoja na shina la ubongo(brainstem)


Dalili mwili uliokufa


  • Kupotea kwa mapigo ya moyo

  • Kupotea kwa mapigo ya mishipa ya damu

  • Kusimama kw aupumuaji

  • Kutosikika kwa sauti za upumuaji

  • Kupanuka kwa pupul kusikodhuriwa na mwanga

  • Kutoonyesha ishara ya maumivu kama yakisababishwa kwenye mwili

  • Konea kupata ukungu

  • Mwili kuanza kubadilika ama kuoza

  • Kushuka kwa joto la mwili- Kuanza kuwa wa baridi kwenye miishio ya mikono na miguu(baadhi ya magonjwa husababisha kupanda kwa joto mara baada ya mtu kufa, joto hili linaweza kukaa masaa kadhaa kabla ya kuanza kushuka)


Mabadiliko yanayotokea mwilini baada ya kufa


  • Mabadiliko ya ghafla

  • Mabadiliko ya mapema

  • Mabadiliko ya muda mrefu


Mabadiliko ya ghafla

  • Kusimama kwa mfumo wa moyo na mishipa ya damu

  • Kusimama kwa mfumo wa upumuaji

  • Kupata mabadiliko kwenye konea ya macho- kuwa na ukungu, kukauka kutochezesha kope na

  • kupanuka kwa pupil kusiko dhuriwa na mwanga.

  • Kupotea kwa matendo yasiyohiari ya maungio ya mwili(refleksi)

  • Kulegea kwa mwili


Mabadiliko ya mapema

  • Mwili kuwa wa baridi kuanzia kwenye miishio ya miguu na mikono

  • Kukakamaa kwa misuli na maungio ya mwili

  • Mwili kubadilika rangi na kuwa kama ya blue ya zambarau


Mabadiliko ya muda mrefu

  • Mwili kujaa gesi na kuanza kuoza

  • Mwili kubadilishwa kutoka katika hali ya mafuta na kuwa hali ya kunata (Wax)

  • Kutuwama kwa maji sehemu ya chini mwili ulipolala- hivyo sehemu hii ya mwili huonekana kama imevimba na kubadilika rangi

  • Mwili kukauka endapo upo mazingira yaliyo na joto bila kuwa na unyevunyevu

  • Kufanyika kwa mafuvu- endapo nyama na viungo vingine vyote vimeoza

  • Kufanyika kwa fosili- fosili ni mifupa ambayo imekaa muda mrefu san ana hivyo huwa na mwonekano wa jiwe.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

19 Julai 2023 20:03:53

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1.Bailey FA, et al. Palliative care: The last hours and days of life. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 28.09.2020

2.Institute for Clinical Systems Improvement. Palliative care for adults. Bloomington, Minn: Institute for Clinical Systems Improvement. https://www.guideline.gov/summaries/summary/47629/palliative-care-for-adults. Imechukuliwa 28.09.2020

3.Miller RD. Palliative medicine. In: Miller's Anesthesia. 8th ed. Philadelphia, Pa: Saunders Elsevier; 2015. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 28.09.2020

4.Survey of Biological Factors Affecting the Determination of the Postmortem Interval pdf. Bautista, Richard. Spring 2012.

5.Michael J. Shkrum, MD etal. Forensic Pathology Trauma. ISBN: 978-1-58829-458-6 page 28,36

6.Burton, J. F. Fallacies in the signs of death. J. Forensic Sci.19:529–534, 1974.

7. Burton, J. F. The estimated time of death. Leg. Med. Annu. 1976:31–35, 1977.

8. Gonzales, T. A., Vance, M., Helpern, M., Umberger, C. J. Legal Medicine, Pathology and Toxicology. 2nd ed. Appleton Century Crofts, New York, 1954.

9. Camps, F. E. Legal Medicine. 2nd ed. John Wright and Sons, Bristol, UK, 1968.

10. Adelson, L. The Pathology of Homicide. Charles C. Thomas, Springfield, IL, 1974.

bottom of page