top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Adolf S, M.D

22 Machi 2020, 23:04:03

Dalili za nimonia
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Dalili za nimonia

Nimonia (nyumonia) ni ugonjwa wa mapafu unaoshambulia mapafu na kupelekea kuvimba, wakati mwingine kusinyaa. Nimonia huathiri sana vifuko vya hewa viitwavyo alveoli, vifuko vya hewa vya aliveoli huweza kujaa maji na kusababisha shida katika upumuaji.


Ugonjwa huu husababishwa na maambukizi ya vimelea aina ya bakteria, virusi, fangasi na vyanzo vingine kama vumbi, gesi na madawa makali na kemikali.


Wagonjwa wengi wenye nimoni hutokana na bakteria aitwaye Streptococcus pneumoniae


Aina za nimonia


Nimonia Imegawanyika katika makundi 2 mawili;


  • Nimonia Inayoambukizwa hospitalin

  • Nimonia Inayoambukizwa kwenye jumuiya


Nimonia inayoambukizwa hospitalin


Nimonia hii utokea wakati mhusika mwambukizaji na anaye ambukizwa wako katika mazingira ya hospitalin


Na vimelea hivi hua ni sugu na hawasikii dawa.


Nimonia ya kuambukizwa kwenye jumuiya


Ni aina ya homa ya mapafu ambayo huambukizwa nje ya kituo cha afya.


Dalili za nimonia kwa ujumla


  • Maumivu ya kifua pale mgonjwa anapohema ama kukohoa

  • Kikohozi kikali chenye kohozi

  • Kuishiwa pumzi, upumuaji kua mgumu

  • Homa kali

  • Kukosa hamu ya chakula, kichefuchefu

  • Mwili kua na uchovu

  • Kuhusi kuchanganyikiwa mara nyingi hali hii hutokea kwa watu ambao wana umri zaidi ya miaka 65.


Dalili kwa Watoto Chini ya Umri wa miaka 5

Kwa Watoto chini ya Umri wa miaka mitano dalili huwa ni mtoto kuwa na homa (joto jingi mwilini), kikohozi, upumuaji wa haraka haraka na kuonekana kuwa na shida katika kupumua.


Vihatarishi vinavyopelekea kupata nimonia


  • Uvutaji sigara

  • Ukosefu wa kinga mwilini

  • Ulevi

  • Uzee

  • Magonjwa sugu

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

19 Julai 2023, 20:03:53

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

​

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

bottom of page