Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Adolf S, M.D
26 Machi 2020, 10:19:26
Dalili za saratani ya damu
Leukemia ni saratani ya damu inayoshambulia tishu zinazohusika kutengeneza damu ikiwa pamoja na urojo wa mifupa na mfumo wa limfatiki.
Leukemia mara nyingi huathiri chembe nyeupe za damu ambazo hupambana na maradhi mbalimbali. Kuathiriwa kwa chembe hizi hufanya mwili kushindwa kupambana na maradhi kutokana na kinga ya mwili kushuka baada ya shambulio hilo.
Visabishi vya saratani ya damu
Visababishi vya saratani hii havijulikani lakini zipo sababu zinazoweza kupelekea kupata saratani hii ikiwa pamoja na:
Kupigwa na mionzi mikali: Mfano baada ya kupigwa bomu la nyuklia kule Japan,Ongezeko la wagonjwa wa saratani ya leukemia iliongezeka zaidi
Kemikali za sumu: Mfano kemikali inayoitwa Benzene ya inayotumiwa viwandani huweza kusababisha saratani hii Leukemia
Virusi: Mfano kirusi cha Human T- Cell Lymphotropic Virus type 1-( HTLV-1) Epstein Bar Virus,pia kirusi cha UKIMWI huweza kusababisha saratani ya leukemia
Sababu za jini (vinasaba): Wanaume huathiriwa zaidi kuliko wanawake, pia watu wenye tatizo la sindromu ya Down’s huathiriwa zaidi
Makundi ya saratani ya damu
Leukemia kali
Leukemia sugu
Leukemia kali ya damu
Leukemia hii inaambatana na kuongezeka zaidi kwa chembechembe za damu ambazo hazijakomaa katika damu. Chembe hizi huitwa blast. Blast hujizalisha kwa wiki sanga ana pia huwa hazina uwezo wa kufnaya majukumu yake ya kinga mwilini. Ugonjwa huhitaji kutibiwa hima ili kupambana nao
Aina za leukemia kali
Leukemia kali imegawanyika kwenye makundi makuu mawili ambayo ni:
Leukemia kali aina ya Mayeloblastiki (AML)
Leukemia kali aina ya limphoblastiki (ALL)
Dalili za ujumla za saratani ya damu
Homa na kutetemeka
Uchovu wa mwili uliopitiliza na endelevu
Mwili kuwa dhaifu
Kupata maambukizi makali na mara kwa mara kuliko mtu mwingine(kuugua mara kwa mara)
Kupoteza uzito bila sababu
Kuvimba kwa tezi za limfu, Ini na bandama
Kutokwa na damu kirahisi
Kutokwa na damu puani mara kwa mara
Mvilio wa damu chini ya ngozi(hutengeneza alama nyekundu)
Kutokwa na jasho jingi haswa wakati wa usiku
Maumivu ya mifupa
Maumivu ya mifupa ukiguswa au wakati wa kutembea
Matibabu
Matibabu ya saratani ya damu (leukemia)
Kuna aina mbalimbali za matibabu ya saratani ya leukemia ambayo ni pamoja na;
Tiba ya dawa za Kemotherapi
Kemotherapi ni msingi mkubwa wa matibabu ya saratani ya leukemia. Dawa hizi ni kemikali zinazotumika kuua chembe za saratani. Mfano wa dawa ni Vincristine, Methotrexate na Cyclophosphamide.
Kwa kutegemea aina ya saratani unaweza kutumia dozi moja au dozi yenye mchanganyiko wa dawa. Dawa hizi zinaweza kuwa kwenye mfumo wa tembe au dawa za maji kwa ajili ya kuchomwa kwenye mishipa ya damu.
Tiba baiologia
Tiba hii huamuru chembe za ulinzi wa mwili kupambana na chembe za saratani.
Tiba elekezi
Tiba hii hutumia dawa zinazoenda kuvamia hatua Fulani ya uzalishaji wa chembe za saratani. Mfano wa dawa ni imatinib.
Tiba mionzi
Mionzi ya Xray hutumika kuharibu chembe ambazo ni saratani na kusimamisha kuzaliana.
Kupandikizwa tishu za stem
Tishu za stem ni tishu za urojo wa mifupa, daktari atakufanyia atakuweka tishu mpya kwenye mifupa yako ili zizalishe chembechembe nyeupe za damu zisizo na saratani.
Kabla ya kuwekewa tishu za stem, utakuwa kwenye dozi kali ya kemotherapi au mionzi ili kuua chembe zinazozalisha saratani. Utawekewa kwenye mifupa yako tishu za stem kutoka kwako mwenyewe au kwa mtu mwingine.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023, 20:03:53
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1. Davidson's Essentials of Medicine edited by J.Alaslair Innes Ukurasa wa 547-552
2. Long Cases in Clinical Medicine kimeandikwa na ABM Abdullah kurasa wa 633-638
3. What you need to know about leukemia. National Cancer Institute. http://www.cancer.gov/publications/patient-education/wyntk-leukemia. Imechukuliwa 26.03.2020
4. Leukemia. Leukemia & Lymphoma Society. http://www.lls.org/resourcecenter/freeeducationmaterials/leukemia/understandingleukemia. Imechukuliwa 26.03.2020
5. Taking time: Support for people with cancer. National Cancer Institute. http://www.cancer.gov/publications/patient-education/taking-time. Imechukuliwa 26.03.2020