Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Adolf S, M.D
21 Machi 2020, 10:10:26
Dalili za Ujauzito wa Wiki moja
Mara baada ya kujamiana kwenye siku za hatari ambapo yai kutoka kwa mama tayari limeshatoka kwenye ovari, mbegu za kiume husafiri kutoka kwenye uke na kuingia kwenye shingo ya kizazi, kisha hupita kwenye kizazi na kufika kwenye mrija wa falopiani na hapo urutubishaji hutokea. Huchukua tatribani siku 20 kwa kijusi kilichofanyika baada ya urutubishaji kufika kwenye kuta za kizazi kutoka kwenye mrija huu wa falopiani.
Mwanamke anayebeba mimba ni yeyote yule mwenye afya njema na aliye katika umri wa kuzaa.
Dalili za ujauzito wa wiki moja
Homa za asubuhi
Kichechefu na kutapika
Kubadilika rangi ya Chuchu na kuwa nyeusi
Kuumwa kwa maziwa
Uchovu
Mwili kulegea
Kukojoa mara kwa mara
Kubadilika kwa mudi ya mtu
Kuvuruga kwa tumbo
Mafua
Maumivu ya kichwa
Kuchagua vyakula vya kula na kukosa hamu ya kula
Kizunguzungu
Kuzimia
Dalili zingine
Dalili nyingine amabazo huonekana baada ya wiki moja kupita ni kama ifuatavyo
Kutokuoana mzunguko wa Hedhi (kutokuona damu ya mwezi)
Tumbo Kuongezeka
Kuhisi mtoto anapocheza tumboni
Kukosa choo(konstipesheni)
Kubadilika kwa kwa rangi ya ngozi
Vipimo vya ujauzito wa wiki moja
Kutokana na ujauzito kuwa chini ya wiki kipimo kitakachoweza pima na kutoa majibu kamili ni kipimo cha picha ya ultrosound. Maana kipimo cha kupima mkojo hakiwezi kuonyesha ujauzito chini ya wiki 2.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023, 20:03:53
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1. Baker, P. & Monga, A. (2006). Obstetrics by Ten Teachers (18th Ed.). London: Hodder Arnold.
2. DeCherney, A.H. & Nathan, L. (2002). Current Obstetrics and Gynaecology (9th Ed.). McGraw Hill.
3. Hanretty, K.P. (2003). Obstetrics Illustrated (6th Ed.). London: Churchill Livingstone.
4. Oats, J., Abraham, S. (2005) Llewellyn-Jones Fundamentals of Obstetrics and Gynaecology. (8th Ed.).
Edinburgh: Mosby.
5. Parisaei, M., Shailendra, A., Dutta, R., Broadbent, J.A. (2008). Crash Course: Obstetrics and
Gynaecology. (2nd Ed.) Mosby.