top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Benjamin L, MD

18 Novemba 2021 06:06:58

Dalili za utapiamlo
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Dalili za utapiamlo

Utapiamlo ni hali inayotokana na utumiaji wa lishe yenye virutubisho ambavyo havitoshi au lishe iliyozidi, inayopelekea athari kwa afya ya mtoto.


Tatizo hili husababisha athari katika ukuaji wa mwili na akili ya mtoto. Watoto walio chini ya umri wa miaka 5 huathirika zaidi.


Aina za utapiamlo

Upungufu wa lishe yenye virutubisho umegaganyika katika makundi mawili nayo ni Nyongea na Unyafuzi (kwashako). Hali hizi zinaweza kutokea kwa pamoja lugha nyingine huitwa Marasmickwashiokor.

Nyongea ni nini?

nyongea ni hali inayowapata watoto kutokana na kupata lishe yenye upungufu wa chakula aina ya wanga/nishati(kabohaidreti).

Unyafuzi ni nini?

Unyafuzi ni hali inayotokea ikiwa kuna upungufu wa protini katika lishe kwa ajili ya mahitaji ya ujenzi wa mwili. Kwa nchi zinazoendelea watoto wengi hupata hali zote yaani unyafuzi na nyongea kutokana na umaskini, elimu duni ya lishe,magonjwa n.k.


Lishe kuzidi ni hali ya kupata lishe kupita kiasi kinachohitajika mwilini, hupelekea mwili kunenepa zaidi, na kuleta Kiribatumbo, hali hii katika nchi zinazoendelea huzania ni afya kwa mtoto kwa sababu ya kukosa ufahamu.


Visababishi.


Visababishi vya utapiamlo ni pamoja na;

  • Ukosefu wa vyakula vya wanga/nishati, protini, madini na vitamin kwa muda fulani

  • Hali ya njaa ya kudumu inayotokana na umaskini .

  • Kukosa sehemu muhimu ya lishe kama protini, nishati ,madini, vitamin kutokana na gharama za chakula cha aina fulani.

  • Kukosa sehemu muhimu ya lishe kutokana na kukosa ufahamu mzuri kuhusu lishe bora.

  • Magonjwa yaweza kuleta utapiamlo kwa muda mfupi kwa watoto, mfano homa ya matumbo, nimonia, malaria mtoto anakosa hamu ya chakula, ikiwa mtoto anahitaji lishe nzuri kwa ajlili ya ukuaji.

  • Tamaduni katika makabila huwa wanatabia ya kukataza wanawake wajawazito na watoto kula aina Fulani za chakula, tamaduni hizi zinasababisha kuzaliwa kwa watoto wenye tatizo hili.


Dalili.

Mtoto anaweza kuwa anaonekana ana afya nzuri kumbe ana tatizo hili, Dalili za utapiamlo(nyongea) kwa watoto ni;

  • Uchovu

  • Tumbo kufura

  • Ngozi kukauka

  • Mtoto kulia bila sababu

  • Mtoto kupata magonjwa ya mara kwa mara

  • Mwezo wa kudhibiti joto la mwili hupungua

  • Dalili za unyafuzi(kwashikor) ni mwili ni

  • Kuvimba mwili(miguu, uso n.k)

  • Kuchubuka kwa ngozi

  • Rangi ya ngozi kubadilika(kuongezeka au kuzidi ukilinganisha na kabla ya tatizo),

  • Kupata vidonda kwenye miguu,mapaja,viuno na nyuma ya masikio.

  • Pia watoto wengi wenye matatizo ya unyafuzi na nyongea huwa na matatizo mengine kama

  • Tatizo la macho kutokana na upungufu wa vitamin A

  • Pia huwa na upungufu wa damu


Wakati gani wa kuwasiliana na daktari?


Wasiliana na daktari mara moja ukiona mtoto ana dalili zilizoorodheshwa hapo juu kwa ajili ya vipimo na matibabu


Unawezaje kumkinga mtoto na utapiamlo?

Chakula chenye mchanganyiko wenye ubora mfano nafaka, maziwa nyama,samaki na maharagwe inaweza kupunguza tatizo. Mama anayelea mtoto anapaswa kupata elimu pia kuhusu lishe bora ili kuzuia utapiamlo kwa mtoto.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

18 Novemba 2021 06:06:58

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1. Saunders, Jet al. “Malnutrition: causes and consequences.” Clinical medicine (London, England) vol. 10,6 (2010): 624-7. doi:10.7861/clinmedicine.10-6-624

2. Elia M, editor. Guidelines for detection and management of malnutrition. Malnutrition Advisory Group, Standing Committee of BAPEN. Maidenhead: BAPEN, 2000.

3. Stratton R, et al. Disease-related malnutrition: an evidence-based approach to treatment. Oxon: Cabi Publishing, 2003.

4. Elia M, et al. How much undernutrition is there in hospitals?. Br J Nutr 2000;84:257–9.10.1017/S000711450000152

bottom of page