Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
ULY CLINIC

6 Aprili 2026, 12:23:26
Embolism ya mapafu
Dalili za embolism ya mapafu ni zipi?
Dalili na ishara za embolism ya mapafu au kifungo cha mapafu hutegemea ukubwa, idadi, na eneo la vijinga vya damu vilivyokwama, lakini ni hali hatari inayoweza kusababisha matumizi makubwa ya misuli ya ziada kwa kupumua.
Dalili kuu ni:
Kupumua kwa shida na kupumua haraka,
Maumivu ya kifua ya pleuriti au chini ya mfupa wa kidari,
Wasiwasi na mfadhaiko,
Mapigo ya moyo haraka,
Kikohozi chenye makohozi, mara nyingine chenye damu,
Homa ya kiwango cha chini,
Ngozi kuwa na rangi ya buluu), kuzimia , na uvimbe wa mishipa ya shingo (Kuvimba kwa vena jugula) ikiwa vijinga vya damu ni vikubwa,
Sauti za mapafu zilizotawanyika (krako ya kutawanyika) na MIruzi katika sehemu fulani iliyoathirika.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 15:59:23
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
ULY CLINIC
