top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Adolf S, MD

9 Desemba 2020 14:28:50

Funza kwenye ngozi
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Funza kwenye ngozi

Katika makala hii utajifunza kuhusu tatizo linalofahamika kitiba kama myiasis, katika makala hii limetumika kumaanisha ‘funza wa ngozi’ kwa binadamu


Myiasis ni nini


Myiasis ni tatizo linalotokea endapo ngozi imevamiwa na funza wa nzi. kuna wa aina tofauti tofauti za funza wa nzi wanaoweza kuvamia ngozi, hata hivyo funza wa nzi ambao wanavamia mara nyingi ngozi ya binadamu huitwa Dermatobia hominis (botfly wa binadamu) na Cordylobia anthropophaga (tumbu fly)


Funza wa nzi wanapoingia mwilini wanaweza kukaa sehemu moja au kusambaa na kuonekana katika maeneo mbalimbali za mwili ambayo ni;


  • Ngozi

  • Kwenye uwazi mbalimbali ndnai ya mwili

  • Nacho

  • Masikio

  • Koo

  • Pua

  • Sinus

  • Utumbo

  • Njia za mkojo

  • Damu- kwa watoto wenye umri chini ya miezi 9


Kumbuka

Si kila aina ya funza anaweza kusambaa sehemu nyingine ya mwili


Dalili


Dalili hutegemea funza alipo, dalili wa funza kwenye ngozi huwa ni;


  • Mwasho wa ngozi

  • Kuhisi kitu inatembea kwenye ngozi

  • Maumivu ya ngozi

  • Kutokwa na maji maji yaliyochanganyika na damu

  • Kuonekana kwa usaha kama vile mtu mwenye chunusi iliyo na usaha

  • Kuonekana kwa kidonda kinachokuwa taratibu na chenye maumivu


Funza huingiaje mwilini?


Funza aina ya Dermatobia hominis (botfly wa binadamu)

Nzi mwenye jina la Dermatobia hominis, hukimbiza na kumkamata mbu kisha kumwachia mayai mwilini mwake haswa katika sehemu ya tumbo la mbu ili kumsaida kusafirisha mayai hayo kwa binadamu. Mbu huyu ambaye chakula chake ni damu ya binadamu. Mbu aliyebebeshwa mayai ya nzi anapokwenda kutafuta malisho yake na kutua kwenye mwili wa binadamu, joto la binadamu hupelekea mayai ya nzi kutotolewa na kutoa funza wadogo (larvae) ambao huangukia kwenye ngozi kisha kutafuta njia ya kuingia ndani ya ngozi. Baadhi ya funza hupita kwenye kitundu cha mbu alichony’onyea damu au kwenye vitundu vingine ambavyo vimesababishwa na majeraha. Inachukua takribani wiki 5- 10 ili funza hawa kukua katika urefu wa milimita 15-25 kabla ya kutoka nje ili baadae wabadilike na kutengeneza nzi ndani ya wiki 2 hadi 4.


Funza wa Cordylobia anthropophaga (tumbu fly)

Aina hii ya nzi hutokea sanaa kwenye nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania, nzi hutu hufanana umbo na botifly wa binadamu. Hupembela kukaa kwenye kivuli lakini huruka sana mida ya asubuhi na mchana. Hupendelea harufu ya kinyesi na mkojo. Mbu wa kike hulaza mayai yake kwenye mchanga mkavu au kwenye nguo chafu zilizoanikwa kwenye kamba kukauka. Mayai hutotolewa ndani ya siku 3 na huweza kudumu kwenye nguo kwa siku 15 ili kusubiria kupata mtu ambaye mayai yatatotoleshwa na kuingia kwenye ngozi. Mara baada ya kukutana na mtu mayai hutotoleshwa na kutoa funza wadogo kisha hupenya kwenye mwili wa binadamu na kuingia kwenye ngozi. Funza huchukua takribani siku 9 hadi 14 kukua na kutoka nje ya mwili wa binadamu. Wanapotoka huwa na urefu kati ya milimita 13 hadi 15.


Matibabu


Matibabu huhusisha dawa au upasuaji wa kuondoa funza mwilini. Dawa hutumika kwenye funza walio kwenye maeneo ya macho, kinywa na puani. Dawa ya kunywa aina ya ivermectin hutumika sana kwa wagonjwa wenye funza kwenye maeneo yaliyotajwa hapo awali ambapo si rahisi kuwatoa kwa upasuaji au kwa madhumuni ya kupunguza uvimbe kutokana na mwitikio wa kinga za mwili.


Matibabu ya nyumbani

Kwa sababu funza hawa huishi kwa kwa kutegemea hew safi ya oksijeni kutoka kwenye mazingira, endapo utafanya mambo yafuatayo utasababisha funza watoke kwenye ngozi au kufa ndani ya ngozi.


Tumia mafuta ya taa, mafuta ya wanyama, afuta mazito, mafuta ya nywele kupaka kwenye kitundu cha funza ili akose hewa na hivyo kutafuta njia ya kutoka nje ya mwili.


Tumia uma ya kushikia wadudu endapo unayo kutoa funza ambao waliokuja karibu na ngozi. Funza wa nzi D. hominis ni wagumu kutoka kwa njia ya kutumia uma kwa sababu ya umbo lao lilivyo hivyo kiwiliwili huweza kukatikia ndani ya ngozi. Unashauriwa kuwasiliana na mtaalamu wa afya kwa msaada zaidi wa matibabu.


Namna ya kujikinga


Unaweza kujikinga na tatizo la funza hawa kwa kufanya mambo yafuatayo;


  • Kuvaa mguo za kufunika mwili ili kutokutana na nzi au mbu, kichwani inashauriwa kuvaa kofia endapo upo kwenye maeneo ambayo kuna tatizo hili

  • Kulala kwenye chandarua chenye kilichotiwa dawa ya mbu

  • Kulala kwenye kitanda badala ya kulala chini ili kuepuka kukutana na mai ya nzi huyu

  • Matumizi ya dawa za kupaka kwa ajili ya kufukuza nzi na mbu wasitue kwenye mwili wako

  • Kupiga pasi nguo zako ili kuua mayai ya nzi huyu pamoja na wadudu wengine

  • Kwa watu wenye vidonda, vidonda vinatakiw akusafishwa vema kwa dawa na pia kufunikwa na gozi ilikuia nzi kutua katika vidonda

  • Watu wenye vidonda hawatakiwi kukaa nje au kuacha milango na madirisha wazi ili nzi wasiingie ndani na kugusa vidonda

  • Hakikisha unasafisha mazingira yako kuzuia nzi na boresha mfumo wa maji taka ili kufukunza nzi kwenye mazingira yako.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

19 Julai 2023 19:54:47

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

​

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1. Myiasis treatment. https://emedicine.medscape.com/article/1491170-medication#2. Imechukuliwa 8.12.2020
2. Myiasis. https://www.cdc.gov/parasites/myiasis/index.html. Imechukuliwa 8.12.2020
3. Causal Agent. https://www.cdc.gov/parasites/myiasis/biology.html.
4. Cutaneous Myiasis . https://www.msdmanuals.com/professional/dermatologic-disorders/parasitic-skin-infections/cutaneous-myiasis. Imechukuliwa 8.12.2020
5. Myiasis in domestic cats: a global review . https://parasitesandvectors.biomedcentral.com/articles/10.1186/s13071-019-3618-1. Imechukuliwa 8.12.2020
6. Cutaneous myiasis . https://dermnetnz.org/topics/cutaneous-myiasis/. Imechukuliwa 8.12.2020
7. Krajewski A. Allen B. Hoss D. Patel C. Chandawarkar RY. Cutaneous myiasis. Journal of Plastic, Reconstructive & Aesthetic Surgery: JPRAS. 62(10):e383-6, 2009 Oct. [Case Reports. Journal Article. Review]

bottom of page