Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Benjamin L, MD
7 Septemba 2021 10:07:49
Hedhi ya muda mrefu
Hedhi ya muda mrefu na hedhi yenye damu nyingi hufahamika kwa jina jingine la menorhajia. Licha ya kuleta wasiwasi, wanawake wengi huwa hawapati damu nyingi zaidi kiasi cha kuitwa menorhajia. Matibabu mbalimbali ya tatizo hili yapo na hutegemea kisababishi.
Dalili za hedhi yenye damu nyingi au ya muda mrefu
Dalili za headhi ya muda mrefu na ile yenye damu nyingi ni pamoja na;
Kuloanisha pedi zaidi ya moja kila saa kwa masaa kadhaa yanayofuatana
Uhitaji ya kutumia pedi zaidi ya moja ili kuzuia damu kumwagika
Uhitaji wa kuamka usiku ili kubadilisha pedi
Kutokwa na damu zaidi ya wiki moja
Kutokwa na mabonge makubwa ya damu
Kujizuiakufanya kazi kutokana na kutokwa na damu nyingi
Kupata dalili za upungufu wa damu kama uchovu na kuishiwa pumzi
Wakati gani wa kuonana na daktari
Tafuta msaada wa daktari endapo;
Damu inayotoka ni nyingi kiasi cha kuloanisha pedi moja au zaidi kwa saa kwa zaidiya masaa mawili
Kutokwa na damu katikati ya mzunguko wa hedhi
Kutokwa na damu baada ya komahedhi
Visabaishi vya damu nyingi au hedhi ya muda mrefu
Kuna sababu mbalimbali zinaweza kuchangia kupata hedhi yenye damu nyingi pamoja au ile ya muda mrefu, hata hivyo kwa baadhi ya nyakati sababu inaweza isifahamike. Baadhi ya sababu ni;
Madhaifu ya anatomia ya mfumo wa uzazi na vimbe
Kasoro za ovari na kukosekana kwa uwiano wa homon mwilini
Madhaifu ya anatomia ya mfumo wa uzazi na vimbe
Uvimbe fibroid ndani ya kizazi
Ni uvimbe unaotokea kwenye mfuko wa uzazi na usio na sifa za saratani na hutokea kwenye umri wa kubeba ujauzito. Kuwa na uvimbe aina hii huweza pelekea kupata hedhi nzito au ya muda mrefu zaidi.
Polipsi
Ni vimbe ndogo zisizo saratani zinazochomoza kama vidole katika kuta za uzazi na huweza pelea hedhi nzito au ile ya muda mrefu zaidi ya kawaida.
Adenomayosis
Hutokea endapo tezi za ukuta wa endometriam zimejipandikiza kwenye misuli ya uzazi. Hii hupelekea maumivu makali wakati wa hedhi pamoja na damu nyingi.
Saratani
Saratani ya kizazi na shingo ya kizazi inaweza pelekea kupata dalili ya hedhi yenye damu nyingi au ya muda mrefu haswa kama umeshaingia kipindi cha koma hedhi. Utapaswa kufanya kipimo cha Pap smear ili kuangalia kama una saratani hii au la.
Kupotea kwa uwiano wa homon mwilini
Kwa mwanamke mwenye mzunguko wa kawaida, kuna uwiano kati ya homon estrogen na progesterone ambao hurekebisha ujengaji wa kuta ndnai ya uzazi ambao unabomoka kila mwezi na kutoka kama damu ya hedhi. Kukosekena kwa uwiano huu husababisha kujengwa kwa kuta kubwa zaidi na hivyo kutoka kama damu nyingi au ya muda mrefu kuliko kawaida
Hali na maradhi mbalimbali yanaweza kupelekea kupotea kwa uwiano wa homon hizi kama vile, sindromu ya vifuko maji vingi kwenye ovari, obeziti, madhaifu ya ukinzani kwenye insulin na matatizo ya tezi thyroid
Kasoro za ovari
Kama ovari haitoi yai kila mwezi kwenye mzunguko wa hedhi, mwili wako hautazalisha homon progesterone kama kwenye mzunguko wa hedhi wa kawaida. Hii hupelekea kupata hedhi yenye damu nyingi au muda mrefu.
Matumizi ya njia za uzazi wa mpango
Njia za uzazi wa mapango ambazo zinaweza kupeleke akutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi au hedhi yenye damu nyingi ni kuwekewa kitanzi kisicho na homoni ndani ya uzazi
Kutokwa na damu muda mrefu au hedhi yenye damu nyingi hufahamika sana kama udhi la kutumia kitanzi kisicho na homon. Kama unapatwa na dalili hii, utabidi kubadilishiwa njia ya uzazi wa mpango.
Madhara ya ujauzito
Kuwa na hedhi moja yenye damu nyingi na iliyochelewa muda wake inaweza kuwa dalili ya mimba iliyotoka. Baadhi ya visababishi vingine vya kutokwa na damu nyingi wakati wa ujauzito ni kondo la nyuma kujipandikiza sehemu isiyo ya sahihi.
Magonjwa ya kurithi ya kuvuja damu
Magonjwa ya kuvuja damu ya kurithi kama ugonjwa wa von Willebrand's husababisha kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi. Magonjwa mengi hutokana na kukosa vigandisha damu muhimu.
Matumizi ya Dawa aina fulani
Baadhi ya dawa kama vile dawa za kuzuia michomo na za homon kama vile estrogen na progestins na dawa za kuyeyusha damu kama vile warfarin au enoxaparin zikitumiwa hupelekea kupata hedhi yenye damu nyigi au ya muda mrefu.
Hali na magonjwa mengine
Kuna baadhi ya hali na magonjwa mengine ambayo yanawezapelekea kutokwa na damu nyingi au kwa muda mrefu wakati wa hedhi kama vile magonjwa ya ini na figo
Vihatarishi
Vihatarishi vya kutokwa na damu nyingi au muda mrefu wakati wa hedhi hutegemea umri wa mtu na magonjwa. Kwa mabindi wadogo, kihatarishi hutokana na ovari kutozalisha yai haswa mwaka wa kwanza baada ya kuvunja ungo hivyo kupelekea damu nyingi kutoka
Kwa watu wazima walio umri wa kupata ujauzito na wazee, kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi mara nyingi hutokana na madhaifu au magonjwa kwenye mfumo wa uzazi kama vile fibroid, polipsi na adenomayosis. Hata hivyo matatizo mengine yanawez akuchangia pia kama vile saratani ya kizazi, madaifu ya kuvuja damu,matumizi ya dawa za kuyeyusha damu, magonjwa ya figo na ini
Utambuzi wa tatizo
Utaulizwa maswali mbalimbali kutokakwa daktari ili kufahau historia ya tatizo lako, vihatarishi ulivyonavyo kisha kufanyiwa uchunguzi wa awali wa mwili wako kabla ya kuagiza vipimo gani vifanyike. Endapo kuna uhaja wa kufanya vipimo, vipimo muhimu kufanyika ili kumsaidia daktari aweze kufahamu shida yako inasababishwa na nini na madhara yaliyojitokeza kutokanana historia ya tatizo lako ni;
Vipimo vya damu
Vinaweza kutambua kiwango cha damu ulichonacho na kama una upunfugu wa damu au la. Vipimo vingine vya damu hulenga kuangalia homon zinazozalishwa na tezi thyroid na pia kuangalia vigandisha damu
Kipimo cha Pap
Kipimo hiki huchukua tishu kutoka kwenye ukuta wa shingo ya kizazi kisha kuangaliwa na hadubini kwa lengo la kutambua kama kuna mabadiliko ya kisaratani katika tishu hizo
Kipimo cha kinyama kutoka kwenye endometriamu
Kinyama kidogo kitachukuliwa kutoka kwenye ukuta wa ndai ya kizazi kwa kipimo hiki ili kutambua kama kuna mabadiliko ya kisaratani.
Kipimo cha ultrasound
Kipimo hiki hutumia miale ya sauti kuangalia via vya uzazi kama vile kizazi, ovari na nyonga. Lengo likiwa kutambua magonjwa au uvimbe kama fibroid, saratani ya endometriam au kutambua kama una ujauzito n.k
Sonohysterografi
Utaingiziwa maji ndani ya kizazi kupitia uke kisha kufanyiwa kipimo hiki ambacho kinaweza kutambua matatizo ya kiafya kwenye mfuko wa kziazi.
Kipimo cha histeroskopi
Kipimo hiki hutumia kamera ndogo iliyo kwenye kifaa chenye mpini mwembamba unaoingizwa kuchunguza ndani ya uzazi na mirija ya uzazi kupitia uke.
Matibabu
Matibabu ya kutokwa damu nyingi au kwa muda mrefu wakati wa hedhi hutegemea kisababishi, hali yako ya kiafya na hali ya ugonjwa, uwezo wa mwili kustahimili tiba utayopatiwa, madhara ya tiba kwenye maisha yako na uhitaji wako w akupata mtoto hapo baadaye. Matibabu huhusisha dawa, upasuaji na ushauri.
Matibabu dawa
Dawa zinazoweza kusaidia tatizo la kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi ni;
Ibuprofen au naproxen sodium hukata damu pia kusaidia kuondoa maumivu
Tranexamic acid. Inayopaswa kutumiwa wakati wa kutokwa na damu nyingi tu basi
Vidonge vya uzazi wa mpango
Vidonge vya progesterone
Kipandikizi chenye homon levonorgestrel ambacho hupunguza ukuaji wa ukuta wa endometriam
Dawa za kuongeza damu kama una dalili za upungufu wa damu mfano madini chuma.
Matibabu ya upasuaji
Utahitaji matibabu ya upasuaji kama tatizo la kutokwa na damu muda mrefu haliweza kudhibitiwa kwa dawa. Upasuaji huo huhusisha;
Kukwanguliwa ukuta wa ndai ya kizazi
Huleta kuondoa ukuta wa ndani ya kizazi unaotengenezwa na kubomoka kila mwezi hivyo kuleta damu nyingi. Mara baada ya kukwanguliwa kizazi, damu itatoka kidogo hata hivyo utahitajika kufanyiwa upasuaji huu mara kwa mara.
Kutengeneza emboli kwenye arteri ya uterine
Kwa wanawake ambao kutokwa na damu nyingi kunatokana na uvimbe wa fibroid, ili kusinyaza fibroid inapaswa kupunguza kiwango cha damu kinachoingia kwenye uvimbe huu kwa kutumia njia hii ya kuziba mishipa ya damu inayolisha vimbe. Kifaa maalumu kitapitishwa kwenye arteri ya femoral inayopatikana kwenye paja kisha kuelekezwa kwa kutumia kamera mpaka kwenye unaopatika kwenye mshipa arteri ya uterus
Upasuaji wa ultrasound
Upasuaji huu hulenga kusinyaza vimbe za fibroid kwa kutumia miale sauti ya ultrasound. Mara zote mgonjwa huwa hajanywi sehemu yoyote ile ya mwili
Upasuaji wa kuondoa uvimbe
Upasuaji huu hulenga kukata uvimbe ndani ya kizazi na kuundoa kwa kutumia mchano kwenye tumbo au kutumia vifaa maalumu vianvyopitishwa ukeni mpaka kwenye kizazi
Kuharibu kwa ukuta wa endometriamu.
Upasuaji huu hutumia miale ya laser ili kuharibu tishu za endometriamu. Baada ya kuahribu tishu hizi unaweza usipate hedhi tena au kupat ahedhi yenye damu kidogo na mara nyingi inakuwa vigumu kupata ujauzito n ahata kama ukipat ani vigumu kukua kwa kawaida hivyo inashauriwa kutumia dawa za uzazi wa mpango mpaka wakati wa koma hedhi mara baada ya kufanyiwa upasuaji huu.
Upasuaji wa kuondoa kizazi
Upasuaji huu hulenga kuondoa chanzo cha kutokwa na damu kwa kuondoa kizazi chote. Baada ya upasuaji huu hutaweza kubeba ujauzito.
Matibabu ya magonjwa mengine
Kama tatizo la kutokwa na damu nyingi limetokana na magonjwa mengine kama madhaifu ya homon thyroid, utakapopata tiba sahihi, tatizo hilo litapotea.
Madhara
Kutokwa na damu kwa mdua mrefu huweza sababisha;
Kuishiwa damu
Kuishiwa madini chuma mwilini (Dalili za kuishiwa damu kama vile kupauka kwa ngozi, uchovu na mwili kuwa mvivu, kupumua kwa shida na kuvimba mwili
Maumivu makali
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
8 Oktoba 2021 04:52:31
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1. Cunningham FG, et al. Abnormal uterine bleeding. In: Williams Obstetrics. 24th ed. New York, N.Y.: The McGraw-Hill Companies; 2014. http://accessmedicine.mhmedical.com. Imechukuliwa 07.09.2021
2. Ferri FF. Menorrhagia. In: Ferri's Clinical Advisor 2017. Philadelphia, Pa.: Elsevier; 2017. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 07.09.2021
3. Heavy menstrual bleeding. Centers for Disease Control and Prevention. https://www.cdc.gov/ncbddd/blooddisorders/women/menorrhagia.html. Imechukuliwa 07.09.2021
4. Kaunitz AM. Approach to abnormal uterine bleeding in nonpregnant reproductive-age women. https://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 07.09.2021
7. Kaunitz AM. Management of abnormal uterine bleeding. https://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 07.09.2021
8. Radiological Society of North America MR-guided focused ultrasound for uterine fibroids. https://www.radiologyinfo.org/en/info.cfm?pg=mrgfus. Imechukuliwa 07.09.2021