top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Adolf S, MD

5 Desemba 2020, 16:39:37

Jino kuwa na rangi nyeusi
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Jino kuwa na rangi nyeusi

Jino moja au meno kuwa na rangi nyeusi haswa meno ya nyuma ni tatizo linalofahamika sana na husababishwa na sababu mbalimbali zinazofahamika kitiba.


Tabia ya kuchunguza meno


Unatabia ya kuchunguza meno yako haswa maeneo ya nyuma ya kinywa yenye jina la molar?

Kama bado na una meno ya nyuma ni vema kuyaangalia na kujenga tabia hiyo ya kukagua kinywa chako ili kuweza gundua mabadiliko yoyote mapema.


Makala hii ni mahususi kabisa kujibu ni nini kisababishi cha jino au meno ya nyuma ya kinywa (meno molar) kuwa na alama nyeusi na namna ya kutibu na kujikinga na tatizo hili.


Anatomia ya jino

Jino limetengenezwa na kuta mbalimbali, katika makala hii ni vema kufahamu kuhusiana na kuta mbili, ukuta wa juu ya jino unaofahamika kama enamel huwa na rangi nyeupe ambayo ndo rangi halisi unayoifahamu, na ukuta wa chini ya enamel unafahamika kama dentin ambao huwa na rangi ya kahawia.


Tazama picha kwa maelezo zaidi


Visabaishi


Nini husababisha meni ya nyuma kuwa meusi?

Vipo visababishi mbalimbali, vikiwemo vile vya kawaida au magonjwa. Visababishi hivyo ni;


  • Kuoza kwa meno

  • Matumizi ya tumbaku(sigara)

  • Kufanyika kwa tartar

  • Matumizi ya maji au chakula chenye madini ya fluoride kwa wingi

  • Matumizi ya dawa

  • Ugonjwa wa Celiac


Kuoza kwa meno

Tatizo hili hutokeaje?


Kiashiria kikubwa cha meno kuoza ni kuonekana kwa alama ya kahawia au nyeusi sehemu ya juu ya jino haswa katika meno ya nyuma. Meno huoza kufuatia kula vyakula vyenye wanga na sukari kwa wingi ikiwa pamoja na vinywwaji au vilezi jamii ya pombe. Vyakula hivi huwa na tabia ya kunata kwenye meno ya nyuma na hutengeneza ukuta ufahamikao kitiba kama plaque. Ukuta huu unaweza kuondolewa endapo utapiga vema mswaki meno yako kila baada ya kula na kabla ya kulala. Endapo hutafanya hivyo, ukuta huu utaharibu sehemu nyeupe ya jino na kusababisha ukuta wa chini ya enamel kwa jina la dentine uonekane na huvyo kuleta rangi ya kahawia au nyeusi.


Matumizi ya tumbaku (sigara)

Matumizi ya mazao ya tumbaku kama tumbaku na siraga hupelekea meno kubadilika rangi kwa sababu ya kuwa na kemikali ya nicotine ambayo ikikutana na meno husababisha yawe yabadilike rangi. Watumiaji wakuu wa tumbaku na sigara huwa na meno ya kahawia au meusi. Vykalua vingine pia vinaweza kusababisha meno yako kuwa meusi.


Kufanyika kwa tartar

Ukuta wa plaque uliofanyika kutokana na mabaki ya chakula na sukari katika meno huendelea kukua na kufanya ukuta mgumu zaidi wenye rangi nyeusi unaoitwa tartar ambao ni mgumu kutoka kwa kupiga mswaki kawaida.


Matumizi ya maji au chakula chenye madini ya fluoride kwa wingi

Kitiba tatizo hili hufahamika kama fluorosis husababishwa na kutumia vyakula vyenye madini mengi ya fluoride. Matumizi ya madini mengi ya fluoride husababisha meno kuonekana na alam nyeusi katika ukuta wa enemal. Ingawa meno yataonekana kama yana rangi mbaya, huna haja ya kwenda hospitali isipokuwa endapo unataka meno yako yawe meupe


Matumizi ya dawa

Kuna dawa za aina nyingi, baadhi ya dawa zinazosababisha meno kubadilika rangi ni


  • Matumizi ya dawa jamii ya tetracycline khaswa kwa watoto

  • Matumizi ya dawa ya kisukari yenye jina la Glibenclamide

  • Matumizi ya dawa ya kufafisha kinywa iitwayo chlorhexidine


Ugonjwa wa Celiac

Wagonjwa wenye ugonjwa wa celiac huwa na meno yenye ukuta dhaifu wa enamel kutokana na kutofanyika kawaida. Meno ya wagonjwa wenye tatizo la celic huwa na meno yenye rangi ya njano, nyeupe au rangi ya kahawia. Ugonjwa wa celiac ni ugonjwa unaodumu maisha yote, watu wenye tatizo hili wanaweza kupatiwa matibabu ya kurejesha rangi ya meno iwe nyeupe.


Matibabu ya hospitali


Yapo matibabu mbalimbali kwa ajili ya jino lililokuwa na rangi nyeusi, matibabu hayo huhusisha


Matumizi ya kalisiamu au fluoride: kuimarisha jino dhidi ya mashimo yaliyofanyika. Njia hii hutumika kwa wagonjwa ambao tatizo limefahamika mapema zaidi


Kuziba vitundu vya jino- endapo vijishimo kwenye jino havijazama ndani zaidi, njia hii hutumika kuziba vijishimo hivyo kwa kutumia madini ya siliva na porcelain.


Endapo jino lako lina shimo kubwa linalofika kwenye mzizi wa jino, utafanyiwa upasuaji wa kutoa jino hili na kisha sehemu jino lilipotolewa itazibwa na madini maalumu.


Kwa wagonjwa wenye jino/meno meusi kutokana na tartar- daktari atatumia vifaa maalumu kutoa ukuta huo ili kuondoa tatizo lako, kisha kupaka kemikali maalumu ambazo zitazuia maneo yako kubadilika rangi yake kirahisi.


Matibabu ya nyumbani


Unaweza kufanya mambo yafuatayo mwenyewe nyumbani kwa ajili ya kujitibu tatizo la meno kuwa meusi kutokana na sababu za vinywaji, chakula na uvutaji wa sigara.


  • Swaki meno yako kwa kutumia mchanganyiko wa maji na magadi soda

  • Tumia dawa ya hydrogen peroxide iliyopunguzwa makali kuswaki meno yako kila siku au kila wiki, kumbuka usimeze na sukutua kwa maji mengi mara baada ya kumaliza kuswaki meno yako

  • Tumia dawa za kufanya meni yawe meupe zinazopatikana madukani kama vile dawa za kuosha kinywa zenye hydrogen peroxide, dawa ya meno yenye sodium hypochlorite au carbamide peroxide

  • Endapo kisababishi ni tartar unahitajika kuonana na daktari wako kwa matibabu ya kitaalamu


Vyakula vinavyozuia khbadilika rangi ya meno


  • Mboga za majani kama spinachi na brokoli

  • Maziwa mgando

  • Matunda yenye nyuzinyuzi kwa wingi kama tufaa, peasi

  • Vyakula vyenye viuajisumu kama karoti, tangawizi na vitunguu swaumu

  • Vyakula kutokana na nafaka zisizokobolewa

  • Karanga


Kujikinga


Ili kujikinga na meno kuwa na rangi nyeusi fanyausafi wa kinywa chako na meno kwa kufuata mbinu sahihi za kufafisha kinywa na meno.


  • Piga mswaki kila unapomaliza kula na kabla hujalala usiku

  • Sukutua kinywa chako kwa maji safi kila siku baada ya kupiga mswaki

  • Tumia dawa ya meno yenye fluoride kila siku isipokuwa kwa watoto chini ya umri wa miezi sita

  • Usitumie vitu vyenye kemikali nicotine mfano tumbaku na sigara

  • Tusiwe na tabia ya kusaga meno yako kuepuka kuharibu ukuta wa juu wa meno yako

  • Usipende kutumia vyakula vyenye rangi isiyo asilia, sukari kwa wingi isipokuwa endapo unapiga mswaki kila unapomaliza kula

  • Usitumie vyakula asilia vyenye rangi nyeusi isipokuwa unapiga mswaki kwa dawa mara baada ya kula

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

19 Julai 2023, 19:54:47

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

​

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1. Enamel hypoplasia and its role in identification of individuals: A review of literature . https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4455163/. Imechukuliwa 3.12.2020
2. CDC. Fluorosis. https://www.cdc.gov/fluoridation/faqs/dental_fluorosis/index.htm
3. Chino CA family dentist discuss causes of black spots on teeth. https://www.brightsmilechino.com/what-causes-the-black-spots-on-teeth.html#. Imechukuliwa 3.12.2020
4. Tooth whitening what we need to know. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4058574/. Imechukuliwa 3.12.2020
5. Dental Enamel Defects and Celiac Disease. https://www.niddk.nih.gov/health-information/professionals/clinical-tools-patient-management/digestive-diseases/dental-enamel-defects-celiac-disease?dkrd=hisce0126. Imechukuliwa 3.12.2020
6. What causes discolored teeth and is there any way to cure or prevent staining? . https://now.tufts.edu/articles/what-causes-discolored-teeth-and-there-any-way-cure-or-prevent-staining. Imechukuliwa 3.12.2020

bottom of page