top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Mangwella S, MD

24 Juni 2021 19:12:45

Kinyesi kigumu kama cha mbuzi
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Kinyesi kigumu kama cha mbuzi

Kupata kinyesi cha mbuzi ni hali inayotokea endapo mtu anapata kinyesi kidogo na kigumu kinachofanana na goroli zilizotengena au zilizoshikana au kinyesi chenye manundu manundu katika kipande kimoja kama inavyoonekana kwenye picha. Kupata kinyesi cha mbuzi kwa binadamu ni dalili ya konstipeshen.


Konstipeshen ni tatizo ambazo linalowapata watu wengi na pia huweza kuwa sugu kama lisipochukuliwa hatua.


Kuna matibabu ya hospitali na nyumbani ambayo unaweza kuyafanya kwa ili kujitibu mweyewe. Tiba asilia pia zipo kwa tatizo hili na zinafanya kazi vizuri.


Kinyesi cha mbuzi kinatokeaje?


Kupata kinyesi cha mbuzi hutokea pale endapo kinyesi kinagawanyika kuwa vipande vidogo vidogo vinavyotoka kama goroli wakati wa kujisaidia haja kubwa. Mgawanyiko huu wa kinyesi unatokea wakatiwa wa mmeng’enyo wa chakula kwenye utumbo au kwenye njia ya kutolea haja kubwa kabla ya kutoka nje na huambatana na kukenyaili kusukuma kitoke nje.


Visababishi


Kwa kawaida binadamu huenda haja kubwa mara tatu kwa siku au mara moja kila baada ya siku tatu, watu wenaopata haja kubwa mara chache zaidi ya kawaida, kinyesi huwa na muda mrefu wa kufyonzwa maji na hivyo kuwa kigumu zaidi na kutoka kwa shida. Visababishi vya kuchelewa kupata kinyesi kwa wakati huongozwa na ukosefu wa nyuzinyuzi kwenye vyakula na matatizo mengine ambayo ni;


 • Matumiziya ya dawa zinazosababisha haja ngumu kama dawa za kutibu sonona au matumizi ya dawa za kutibu haja ngumu kwa wingi

 • Hofu au wasiwasi uliopitilzia

 • Magonjwa ya mfumo wa fahamu kama demenshia, majeraha kweye mishipa ya kuthibiti misuli ya haja kubwa kutokana na ajali ya uti wa mgongo n.k

 • Ugonjwa wa sindromu ya iritabo baweli

 • Magonjwa sugu kama kisukari, haipothairoidizimu na saratani ya utumbo mpana

 • Maisha ya kuka muda mmwingi

 • Kula chakula kigumu kisicho na maji maji

 • Kutokunywa maji ya kutosha


Dalili


Baadhi ya dalili zinazoambatana na kinyesi kigumu kama cha mbuzi ni;


 • Maumivu wakati wa kujisaidia

 • Kukenya wakati wa kujisaidia

 • Kutumia vidole kitoa kinyesi kwenye njia ya haja kubwa

 • Kugandamiza tumbo kwa mikono ili kusaidia kusukuma kinyesi

 • Hisia za kujisadia kinyesi kikubwa zaidi njia ya haja kubwa

 • Hisia za kubaki kwa kinyesi kwenye kifuko cha kutuza kinyesi baada ya kujisaidia

 • Kupata hamu ya haja kubwa chini ya mara tatu kwa wiki


Uchunguzi


Tatizo la kupitisha haja ngumu kama ya mbuzi mara nyingi huwa halihitaji kufanyiwa vipimo. Daktari wako atatafuta kisababishi kwa kukuuliza maswali mbalimbali kisha kukufanyia uchunguzi wa awali wa mwili haswa tumbo na njia ya haja kubwa.


Endapo kuna dalili zinazoashiria tatizo jingine mbali na haja ngumu kama yalivyooanishwa kwenye visababishi, vipimo vitafanyika kulingana na kisabishi alivyoshuku na vinaweza kuwa;


 • Vipimo vya maabara mfano kupima damu kuangalia kiwango cha homoni ya thyroid na kalisiamu

 • Vipimo cha ultrasound

 • Kipimo cha CT scan

 • Kipimo cha bariamu

 • Kipimo cha endoscopy kuangalia ndani ya tumbo na utumbo

 • Kipimo cha uwezo wa misuli ya njia ya haja kubwa


Matibabu


Matibabu mara nyingi hulenga kuondoa kisababishi. Makala hii imeelezea matibabu ya kisababishi kikuu yaani konstipesheni. Matibabu ya konsipesheni yanalenga kulainisha haja kubwa kufanya ili iweze kupita hirahisi wakati wa kujisaidia


Matibabu lishe na kubadilisha mtindo wa maisha ni;

Haja ngumu huweza kutibiwa kwa dawa au tiba ya kubadilisha mazoea ya maisha.


 • Kula vyakula vyenye nyuzinyuzi kwa wingi kama nafaka zisizokobolewa, mboga za majani matunda kama tango n.k

 • Kunywa maji ya kutosha kufanya kinyesi kiwe laini

 • Kutumia dawa za kulainisha kinyesi ili kipite kirahisi. Dawa hizi zimetajwa kwenye makal ya ‘dawa za konstipesheni’ na ‘dawa za kuharisha’

 • Kufanya mazoezi ya kuongeza uwezo wa misuli ya sakafu ya nyonga na tundu la kupitisha kinyesi kwa wenye shida ya sakafu hii.

 • Kufanya mazoezi mengine ya viungo vya mwili au anaerobiki kama kukimbia kunakofanya utumbo usukume chakula kirahisi na hivyo upate hisia za kwenda haja

 • Kama haja ngumu ya mbuzi inasababishwa na konstipesheni, tatizo hili litaisha kwa kufanya njia zilizotajwa hapo juu, endapo visababishi ni vingine basi tatizo litaendelea na unahitaji kutafuta msaada zaidi kutoka kwa daktari wako.


Dawa za asili

Zipo dawa mbalimbali za asili kwa ajili ya kuondoa tatizo la kinyesi kigumu ambazo zinapatikana sehemu nyingi. Wasiliana na daktari wako kwa ushauri wa dawa gani ni nzuri. Hata hivyo ULY CLINIC inakushauri isiwe mazoea kutumia dawa ili kupata kinyesi laini, lengo kubadilisha mfumo wa maisha yako.


Wakati gani wa kuonana na daktari?


Endapo unapata kinyesi cha mbuzi na dalili zifuatazo unapaswa kutafuta msaada wa daktari haraka;


 • Dalili zinaongezeka jinsi siku zinavyoenda

 • Kinyesi kutokana na damu

 • Maumivu ya tumbo au homa

 • Kutojamba

 • Tumbo kujaa jinsi siku zinavyoenda

 • Kutapika vilivyomo tumboni


Wapi unaweza kupata taarifa zaidi kuhusu kinyesi kigumu?


Pata taarifa zaidi kuhusu konstipesheni kwa kubofya hapaMajina mengine ya kinyesi cha mbuzi kwa binadamu


Majina mengine yanayotumika kumaanisha kinyesi cha mbuzi kwa binadamu ni;


 • Kinyesi kigumu

 • Kinyesi kikavu

 • Kinyesi kilichotengana

 • Kinyesi kama goroli

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

13 Agosti 2023 08:59:43

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1. Mediscape. Constipation workup. https://emedicine.medscape.com/article/184704-workup. Imechukuliwa 24.05.2021

2. Mayo clinic. Constipation. https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/constipation/diagnosis-treatment/drc-20354259. Imechukuliwa 24.05.2021

3. National Digestive Diseases Information Clearinghouse Constipation. https://www.niddk.nih.gov/health-information/digestive-diseases/constipation/all-content. Imechukuliwa 24.05.2021

4. Chumpitazi CE, et al. Soap suds enemas are efficacious and safe for treating fecal impaction in children with abdominal pain. Gastroenterology. 2016;63:15.

5. Kellerman RD, et al. Constipation. In: Conn's Current Therapy 2019. Philadelphia, Pa.: Elsevier; 2019. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 24.05.2021

6. Ferri FF. Constipation. In: Ferri's Clinical Advisor 2019. Philadelphia, Pa.: Elsevier; 2019. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 24.05.2021

7. U.S. Department of Health and Human Services and U.S. Department of Agriculture . 2015-2020 Dietary Guidelines for Americans. https://health.gov/dietaryguidelines/2015/guidelines. Imechukuliwa 24.05.2021

8. Wald A. Etiology and evaluation of chronic constipation in adults. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 24.05.2021

9. Wald A. Management of chronic constipation in adults. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 24.05.2021

10. American College of Gastroenterology . Constipation and defecation problems. https://gi.org/topics/constipation-and-defection-problems/. Imechukuliwa 24.05.2021

bottom of page