top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Adolf S, MD

4 Desemba 2020 07:52:34

Kuganda kwa damu
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Kuganda kwa damu

Kuganda kwa damu ni moja ua njia za ulinzi wa mwili dhidi ya majeraha yanayotokea ndani na nje ya mwili, njia hii huzuia kiwango kikubwa cha damu kupotea na kuvilia ndani ya mwili. Chembe sahani za damu pamoja na protini mbalimbali zinazohusika na ugandishaji damu hushirikiana kwa karibu iki kufanya dmau igande baada ya kupata jeraha mwilini.


Hata hivyo endapo damu inaganda pasipo majeraha au bila mpangilio, tatizo la kuganda damu hutokea na kuleta madhara makubwa mwilini. Kwenye makala hii utajifunza kuhusu tatizo la damu kunganda linalofahamika kwa jina la thrombophilia


Thrombophilia husababishwa na madhaifu ya mwili katika utengenezaji wa vigandisha damu, huweza kuwa ni tatizo la kurithiwa au kutokea baada ya kuzaliwa. Vigandisha damu ni protini mbalimbali zinazozalishwa na ini mfano wake ni Protein C, Protein S, Protein Z, prothrombin na factor V Leiden


Visababishi


VIsababishi vya damu kuganda kupita kiasi vimegawanyika katika makundi mawili, visababishi vya kuzaliwa (kurithi) na visababishi vinavyotokea baada ya kuzaliwa.


Visababishi vya kuzaliwa

Visababishi vya kuzaliwa, ni visababishi ndani ya mwili ambavyo vimerithiwa na huonekana tu pale mtu anapozaliwa endapo akipimwa. Visababishi hivyo ni ;


  • Mutation katika factor V Leiden

  • Upungufu wa antithrombin

  • Upungufu wa Protein C

  • Upungufu wa Protein S

  • Upungufu wa Protein Z

  • Mutation katika protini ya prothrombin 20210


Visababishi


Madhaifu ya kuganda kwa damu kupita kiasi ambayo huonekaa baada ya kuzaliwa na kusababisha thrombophilia ni;


  • Disseminated intravascular coagulation(DIC)- hutokea mara nyingi kwa wagonjwa wenye saratani.

  • Sindromu ya Antiphospholipid antibody- huamsha vigandisha damu kufanya kazi yake kupita kiasi.

  • Hyperhomocysteinemia- husababishwa na upungufu wa vitamin B6, vitamin B12, au folate

  • Kukaa sehemu moja kwa muda mrefu pasipo kutembea- hutokea sana kwa watu waliopooza, wanaofanya kazi za kukaa au kusafiri masafa marefu, kulala kitandani kwa muda mrefu au historia ya kufanyiwa upasuaji na mshituko wa moyo.

  • Kuferi kufanya kazi kwa moyo- husababisha damu kutosafirishwa vema kwenda sehemu zingine za mwili na hivyo kupelekea damu kuganda.

  • Kuwa na uzito mkubwa kupita kiasi au ugonjwa wa obeziti- hupelekea kuongezeka kwa shinikizo ndani ya mishipa ya vein na hivyo kusababisha damu kuwa na tabia ya kuganda.


Vihatarishi


Vihatarishi vinavyokufanya uwe na hatari kubwa zaidi ya kupata tatizo la thrombophilia au kupata madhara makubwa ya damu kuganda huwa ni;


  • Kufanya kazi zinazokufanya ukae chini kwa muda mrefu

  • Kufanyiwa upasuaji

  • Sindromu ya nephrotic

  • UKIMWI

  • Kuwekewa catheter kwenye mishipa mikuu ya damu

  • Kupatwa na Mshituko wa moyo

  • Kutumia dawa zenye estrogen kama vile dawa za uzazi wa mpango (majira) na dawa za hormonal therapy

  • Uvutaji wa sigara

  • Kuwa mjamzito

  • Kuwa na historia ya embolism ya Pulmonary

  • Historia ya tatizo hili kwa ndugu wa damu moja

  • Kupata kiharusi(stroke)

  • Kuwa na madhaifuya Factor V Leiden

  • Kuwa na matatizo ya rhythm ya moyo

  • Kuwa na moyo ulioferi

  • Kuwa na sindromu ya Antiphospholipid

  • Kuwa na tatizo Arteriosclerosis / atherosclerosis

  • Kuwa na tatizo la Deep vein thrombosis (DVT)

  • Kuwa na tatizo la Polycythemia vera

  • Kuwa na ugonjwa wa obeziti

  • Magonjwa ya mishipa ya arteri pembezoni mwa mwili

  • Ugonjwa wa COVID 19


Dalili


Dalili hutegemea sehemu iliyoathiriwa na tatizo la dmau kuganda, katika sehemu hii utajifunza kuhusu dalili ya baadhi ya maeneo;


Dalili katika mfumo wa upumuaji (mapafu)

  • Kuishiwa pumzi

  • Maumivu ya kifua

  • Kutokwa jasho

  • Homa

  • Kukohoa damu

  • Mapigo ya moyo kwenda haraka sana



Dalili kwenye Miguu

  • Mguu kuwa wa moto

  • Mguu kubadilika rangi (kuwa na rangi nyekundu)

  • Kuvimba kwa mguu


Dalili kwenye moyo

  • Kuishiwa pumzi

  • Kichefuchefu

  • Maumivu ya kichwa

  • Kutokwa na jasho

  • Kutojihisi vema sehemu ya juu ya kiwiliwili

  • Maumivu ya kifua

  • Hisia za mgandamizo kwenye kifua


Kwenye ubongo

  • Kushindwa kuongea

  • Uono hafifu

  • Kupooza upande mmoja wa uso, mikono au miguu

  • Maumivu ya kichwa ya ghafla


Dalili za tumboni

  • Kutapika

  • Kuharisha

  • Maumivu makali ya tumbo



Matibabu

  • Matibabu huhusisha kuchukuliwa historia ya tatizo lako kisha kufanyiwa vipimo vya msingi ili kutambua tatizo ni nini. Vipimo vitafnayika ili kutambua kisababishi, kutathmini madhara na kutoa njia sahihi ya matibabu yako.

  • Tatizo la damu kuganda la kurithi huwa halina tiba, matibabu hulenga kuondoa dalili tu zisitokee mara nyingi ili mtu aishi maisha yenye ubora


Vipimo


  • Kipimo cha PT-INR- Prothrombin time

  • Kipimo cha Activated partial thromboplastin time (aPTT

  • Kiwango cha Fibrinogen

  • Kipimo cha Complete blood count (CBC)


Baadhi ya vipimo vya kupima matatizo ya kurithi ya kuganda kwa damu ni


  • Kipimo cha jeni ambavyo ni kipimo cha factor V Leiden na jeni ya prothrombin gene mutation

  • Kipimo cha ufanyajikazi wa Antithrombin

  • Kipimo cha ufanyajikazi wa Protein C

  • Kipimo cha ufanyajikazi wa Protein S

  • Kipimo cha kiwango cha homocysteine kipinidi hujala chakula


Endapo una historia ya vitu vifuatavyo unatakiwa fanyiwa vipomo utambuzi kugundu kama una madhaifu ya damu kuganda ndani ya mwili wako ili kufanya mikakati ya kujikinga kupata tatizo hili pia;


  • Historia ya tatizo la kuganda damu kwa ndugu wa damu kwenye familia

  • Kuganda damu kwenye umri mdogo, chini ya miaka 50

  • Kuwa na historia ya kuganda damu kwenye maneo haya, mikono, ini, utumbo, figo na ubongo

  • Kuganda damu kusikokuwa na kisababishi

  • Kuganda damu kunakojirudia

  • Historia ya kujirudia ya tatizo la damu kuganda

  • Kutokwa na mimba kunakojirudia

  • Kupata kiharusi kwenye umri mdogo


Madhara


Kupata tatizo la embolism ya pulmonari

Hutokea endapo chembe za damu iliyoganda zimesafiri na kwenda kuziba mishipa ya damu ya mapafu. Tatizo hili huwa linahitaji matibabu ya haraka na huweza kusababisha kifo kwa mgonjwa. Dalili huhusisha; maumivu ya kifua, kuishiw apumzi, maumivu ya kichwa na kizunguzungu, kikohozi kikavu au kukohoa damu na mirenda, maumivu juu ya mgongo na kuzimia.


Tatizo sugu la kutofanya kazi kwa mishipa ya miguuni inayorejesha damu kwenye moyo

Hutokea endapo tatizo la damu kuganda miguuni limejirudia rudia kwa muda mrefu. Huambatana na mabadiliko ya rangi pamoja na kuvimba kwa miguu


Kuvimba kwa mishipa ya vein iliyo karibu na ngozi

Hutokana na kuganda kwa damu kwenye mishipa ya damu iliyo karibu na ngozi, hupelekea mguu kuvimba, kuwa wa moto na kuonekana kwa mishipa ya damu.


Kiharusi na mshituko wa moyo

Hutokea pale endapo damu imeganda kwenye mishipa ya damu ya ubongo au kwenye moyo, hata hivyo tatizo linaweza kuletwa pia na chembe zilizonyofoka kwenye uvimbe ulio mbali na moyo mfano miguuni. Dalili hizi ni hatari na huweza kusabbabisha kifo.


Kumbuka: Kwa watu wanaorithi tatizo la damu kuganda, dalili huwa hazionekani haraka mara baada ya kuzaliwa, tatizo huja onekana baada ya kuwa kijana mdogo, hata hivyo damu inaweza kuganda kwenye umri wowote ule.


Matibabu


Matibabu dawa

Matumizi ya dawa za kuyeyusha damu(anticoagulant) huwa ni msingi wa matibabu ya tatizo la damu kuganda kupita kiasi.


Endapo mtu ameshapata tatizo la kuganda damu mara mbili katika maisha yake anashauriwa kutumia dawa za kuyeyusha damu kama warfarin katika maisha yake yote ili kuzuia damu kuganda kwa wakati mwingine.


Tatizo la hyperhomocysteinemia hutibiwa kwa kutumia vitamin kwa kuwa hutokana na upungufu wa vitamin.


Utahitaji kufanyiwa vipimo vya damu mara kwa mara endapo unatumia dawa za kuyeyusha damu


Matibabu ya nyumbani

Fanya mambo yafuatayo kujikinga au kufanya usipate tatizo la kuganda kwa damu kupitiliza


  • Epuka kukaa sehemu moja kwa muda mrefu bila kutembea- hata kama unasafiri safari ya muda mrefu sana kwenye ndege amka na kutembea hata kuelekea maliwato ili tu ufanye mzunguko wako wa damu uongezeke.

  • Endapo unaendesha gari safari ndefu, fanya hivyo pia, simamisha gari na tembea mwendo Fulani ili kufanya mzunguko wako wa damu uwe vizuri na kuzuia damu kuganda.

  • Hakikisha baada ya upasuaji unaanza kufanya mazoezi ya kutembea ili uongeze mzunguko wa damu na kufanya upone haraka pia kuzuia kupata tatizo la damu kuganda.

  • Kunywa maji ya kutosha wakati unasafiri ili kuongeza kiwango cha maji mwilini na kuzuia damu kuganda.

  • Badili mtindo wa maisha yako, endapo una uzito mkubwa kupit akiasi, punguza uzito kwa kufanya mazoezi au kufanya diet.

  • Acha kuvuta sigara

  • Fanya mazoezi yenye mpangilio na mara tatu au nne kwa wiki

  • Dhibiti shinikizo la damu la juu kwa dawa na chakula unachokula

  • Penda kujifunza kwa kusoma Zaidi kuhusu matatizo ya mwili wako na kufahamu njia mbalimbali za kujikinga na matibabu yake.


Wakati gani wa kuonana na daktari ?


Mwone daktari wako haraka endapo unaata dalili hizi;


  • Mapigo ya moyo kwenda haraka

  • Kuvimba na kubadilika rangi kwa miguu yako kunakoambatana na maumivu na kuongezeka joto la mguu

  • Kushindwa kuongea ghafla

  • Kupoteza hisia usoni au kwenye miguu kwa ghafla

  • Kupata maumivu wakati wa kupumua au kushindwa kupumua

  • Kupata maumivu wakati wa kunyoosha bega, mkono au taya

  • Kukohoa makohozi yenye damu

  • Kuhisi kichwa chepesi na kizunguzungu

  • Kubadilika kwa uono wako ghafla


Majina mengine ya kuganda kwa damu

  • Thrombofilia

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

19 Julai 2023 19:54:47

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

​

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1. Joel L. Moake etal. Excessive Clotting. https://www.msdmanuals.com/home/blood-disorders/excessive-clotting/excessive-clotting. Imechukuliwa 4.12.2020
2. Joel L. Moake, MD etal. Overview of Blood Clotting Disorders . https://www.msdmanuals.com/home/blood-disorders/bleeding-due-to-clotting-disorders/overview-of-blood-clotting-disorders. Imechukuliwa 4.12.2020
3. Blood clots. American Society of Hematology. http://www.hematology.org/Patients/Blood-Disorders/Blood-Clots/5233.aspx. Imechukuliwa 4.12.2020
4. Your guide to preventing and treating blood clots. Agency for Healthcare Research and Quality. http://www.ahrq.gov/patients-consumers/prevention/disease/bloodclots.html. Imechukuliwa 4.12.2020
5. Understand your risk for excessive blood clotting. American Heart Association. http://www.heart.org/HEARTORG/Conditions/More/Understand-Your-Risk-for-Excessive-Blood-Clotting_UCM_448771_Article.jsp. Imechukuliwa 4.12.2020
6. What causes excessive blood clotting? National Heart, Lung, and Blood Institute. http://www.nhlbi.nih.gov/health/health-topics/topics/ebc/causes. Imechukuliwa 4.12.2020
7. Blood Clotting Disorders (Hypercoagulable States). https://my.clevelandclinic.org/health/diseases/16788-blood-clotting-disorders-hypercoagulable-states. Imechukuliwa 4.12.2020

bottom of page