Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Peter A, MD
17 Aprili 2020 19:19:08
Kuishiwa pumzi
Hali na magonjwa mbalimbali yanaweza kusababisha tatizo la kuishiwa pumzi. Mara nyingi kuishiwa pumzi hutokana na matatizo ya moyo na mapafu, moyo na mapafu huhusika kwenye uchukuaji na usafirishaji wa hewa safi ya oksijeni kwenda kwenye tishu mbalimbali na kuondoa hewa chafu ya kaboni monoksaidi kwenye damu. Kuharibika kwa mfumo huu huleta matatizo ya kupumua kwa shida na kuishiwa pumzi
Dalili
Damu kwenye makohozi
Majeraha ya kifua
Maumivu ya kifua
Kifua kubana
Kukohozi
Kizunguzungu
Kuzimia
Kuchoka
Kuhisi mapigo ya moyo kwenda ndivyo sivyo
Kupumua kwa shida
Maumivu ya shingo
Maumivu wakati wa kuvuta hewa
Kupumua haraka haraka na kwa shida
Kutoa sauti za miruzi au filimbi wakati wa kupumua
Visababishi vya muda mfupi
Visababishi vya muda mfupi vya kuishiwa pumzi ni;
Kupata mzio mkali
Pumu
Sumu ya karbon monoksaidi
Mgandamizo kwenye moyo
Magonjwa sugu ya mapafu
Shambulio la moyo
Mapigo ya moyo kwenda ndivyo sivyo
Kuferi kwa moyo
Homa ya mapafu
Hewa kuajaa kwenye kuta za mapafu
Thrombosis ya mishipa ya damu ya mapafu
Kuishiwa damu kutokana na kupoteza damu haraka
Kuziba kwa njia za hewa katika mfumo wa upumuaji
Visababishi sugu
Kuishiwa kwa pumzi ambapo huweza kuchukua wiki hadi muda mrefu, visababishi huwa pamoja na;
Pumu ya kifua
Magonjwa sugu ya mapafu kama COPD
Kuferi kwa moyo
Uzito kupita kiasi(obeziti)
Kujaa kwa maji kwenye kuta za mapafu
Matatizo ya mapafu
Ugonjwa wa viral croup
Saratani ya mapafu
Kuvimba kwa seli zilizopo kwenye mapafu
Kuvilia kwa maji kwenye kuta za mapafu
Mapafu kuwa machakavu
Shinikizo la juu la damu kwenye mapafu
Kifua kikuu
Matatizo ya moyo
Magonjwa ya misuli ya moyo
Moyo kushindwa kufanya kazi
Kutanuka kwa kuta za moyo
Matatizo mengine
Kuishiwa damu
Matatizo ya woga na wasiwasi
Mbavu kuvunjika
Kupaliwa
Koromeo la hewa kuvimba
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023 20:02:52
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1.HealthLine.ShortnessofBreathing.https://www.healthline.com/health/what-does-shortness-of-breath-feel-like. Imechukuliwa 17/4/2020
2.MedicineNet.Shortnessofbreathing.https://www.medicinenet.com/shortness_of_breath/symptoms.htm. Imechukuliwa 17/4/2020
3.WebMd.Dyspnea.https://www.webmd.com/lung/shortness-breath-dyspnea. Imechukuliwa 17/4/2020
4.Harrison Principles of Internal Medicine ISBN NI 9781259644030 Written by Tinsley R Harrison ukurasa wa 201