Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Adolf S, MD
26 Novemba 2020 15:35:43
Kujisaidia kinyesi chenye harufu mbaya
Haja kubwa au kinyesi kwa kawaida huwa na harufu isiyopendeza watu wengi na wakati mwingine baadhi ya watu hukataa kabisa kuangalia kinyesi kwa sababu huweza kupata kichefuchefu au kutapia. Licha ya kuwa na harufu mbaya, kinyesi kinaweza kuwa na harufu mbaya zaidi ya ile ambayo umeizoea. Makala hii imezungumzia sababu za kitaalamu za kupata kinyesi chenye harufu mbaya.
Visababishi
Harufu mbaya ya kinyesi huweza kusababishwa na sababu mbalimbali ambazo ni;
Kutofyonzwa vema kwa chakula
Maambukizi tumboni
Matumizi ya dawa aina fulani
Kuugua magonjwa mengine
Kutofyonzwa vema kwa chakula
Hutokea endapo tumbo lako limepoteza uwezo wa kufyonza chakula kilichomeng’enywa kwa kiasi kinachotakiwa na hivyo kubaki tumboni. Chakula hiki hushambuliwa na bakteria hivyo kutengeneza harufu mbaya ya kinyesi. Baadhi ya magonjwa yanayosababisha kutofyonzwa kwa chakula vema ni;
Ugonjwa wa Celiac- mtu huwa na aleji na chakula chenye ngano na huambatana na harufu mbaya ya kinyesi pamoja na dalili zingine
Ugonjwa wa Crohn’s- mtu huwa na aleji na chakula chenye ngano na huambatana na harufu mbaya ya kinyesi pamoja na dalili zingine
Ugonjwa wa Ulcerative colitis
Mwili kutostahimili chakula cha wanga
Mwili kutotostahimili chakula cha protini
Mwili kutostahimili chakula chenye lactose mfano maziwa n.k
Aleji ya chakula mfano maziwa n.k
Maambukizi tumboni
Maambukizi kwenye mfumo wa tumbo huweza kupelekea kupata harufu mbaya ya kinyesi, maambukizi yanaweza kuwa ya bakteria, virusi au vimelea.
Dalili
Dalili zingine
Kinyesi kutoa harufu mbaya kama ya kitu kilichooza
Kutoa harufu mbaya ukila vyakula aina Fulani tu
Kuharisha au kupata haja ngumu
Kutoa upepo njia ya haja kubwa wenye harufu mbaya
Maumivu ya tumbo
Kuendesha
Kutoa kinyesi chenye mafuta
Tumbo kujaa gesi
Ganzi
Misuli kukaza
Vidonda mdomoni
Mvurugiko wa tumbo
Vipele vya aleji kwenye ngozi
Matumizi ya dawa aina Fulani
Matumizi ya baadhi ya dawa hupelekea kupata choo kinachonuka na hutokea sana ukiwa una aleji nazo, baadhi ya dawa za antibayotiki huweza kuleta kinyesi kutoa harufu mbaya kwa sababu huua bakteria walinzi na kuacha bakteria wanaoozesha chakula mfano wa dawa hizo ni
Dawa baadhi jamii ya antibaotic
Matumizi ya Vitamin A, D, E na K na Multivitamin
Magonjwa mengine
Magonjwa mengine kama ugonjwa sugu wa kidole tumbo (pancreatitis), cystic fibrosis na kuwa na utumbo mfupi kutokana na kukatwa wakati wa upasuaji husababisha kutoa kinyesi kinachonuka sana.
Wakati gani wa kwenda hospitali
Ukipata kinyesi kinachotoa harufu mbaya pamoja na dalili hizi onana na daktari wako haraka;
Homa
Maumivu ya tumbo
Kupungua uzito bila sababu
Kutetemeka mwili
Damu kwenye kinyesi
Kinyesi cheusi
Kinyesi kilichopauka
Kuharisha kunakoendelea
Dalili za kuishiwa maji mwilini
Utapiamlo
Kinga
Fanya mambo yafuatayo ili ujikinge kupata harufu mbaya ya kinyesi
Epuke kutumia maziwa ambayo hayajachemshwa
Zuia kutumia vyakula ulivyo na aleji navyo au ambavyo tumbo lako halivifyonzi vema
Endapo una magonjwa yaliyotajwa hapo juu fanya hima kupata uchunguzi na matibabu
Kama una ugonjwa wa crohn’s au ulcerative colitis, epuka vyakula vinavyochokoza tumbo lako
Zuia vyakula visioze kwa kuvitunza vema kabla ya kuvipika au kuvila. Tunza vyakula kwenye jokofu, vipashe au pika na viive kabla ya kula.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023 19:54:47
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1.Chronic pancreatitis causes and symptoms. https://pancreasfoundation.org/patient-information/chronic-pancreatitis/causes-and-symptoms/ Imechukuliwa 24.11.2020
2.Milk & dairy allergy. https://acaai.org/allergies/types-allergies/food-allergy/types-food-allergy/milk-dairy-allergy. Imechukuliwa 24.11.2020
3.What is inflammatory bowel disease (IBD)?. https://www. cdc.gov/ibd/what-is-IBD.htm. Imechukuliwa 24.11.2020
4.What is celiac disease? (n.d.). https://www.celiac.org/about-celiac-disease/what-is-celiac-disease/ Imechukuliwa 24.11.2020
5.Healthline. Foul smelling stool. https://www.healthline.com/health/stools-foul-smelling#prevention. Imechukuliwa 24.11.2020
6.These 6 factors could be making your poop smell so bad!. https://timesofindia.indiatimes.com/life-style/health-fitness/health-news/six-reasons-why-your-poop-smells-so-bad/photostory/71274090.cms. Imechukuliwa 24.11.2020