Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
ULY CLINIC
14 Septemba 2023 16:40:33
Kukauka ngozi
Ngozi kukauka kwa jia jingine la kitiba hufahamika kama xerosis kyutizi mara nyingi husababishwa na sababu za kawaida kama vile hali ya hewa ya umoto au baridi, kuloweka ngozi kwenye maji ya moto na kukosekana kwa unyevu kwenye ngozi. Visababishi hivi vinavyojulikana huweza kutubika kwa njia ambazo mtu anaweza kuzifanya nyumbani. Hata hivyo baadhi ya watu hupata tatizo kubwa linaloogopesha na kufanya waende hospitali kuonana na daktari wa ngozi.
Ngozi kukauka huambatana pia na kupasuka kwa ngozi, kupata magamba, kupata ramani na miwasho haswa katika maeneo ya viganja vya mikono, mikono na miguuni
Visababishi
Zipo hali na magonjwa mbalimbali yanayoweza kupelekea ngozi kukauka, katika sehemu hii utajifunza sababu zinazosababisha kwa kaisi kukibwa.
Kuwa na magonjwa ya ngozi kama demataitizi, kontakti demataitizi, pumu ya ngozi, soriasisi
Kukaa kwenye hali ya hewa yenye unyevu kidogo
Hali ya hewa ya ujoto, kuishi mazingira yenye joto kali
Kuoga maji ya moto na kwa muda mrefu au mara kwa mara
Matumizi ya sabuni na kemikali zinazokausha ngozi
Dalili
Dalili hutegemea kisababishi na umri wako, unaweza kupata dalili zifuatazo;
Kuhisi ngozi kuvuta mara baada ya kuoga au kuogelea
Ngozi kuwa nyekundu
Ngozi kuwa na rangi ya majivu
Kupasuka kwa ngozi au kuwana michirizi
Kuwasha kwa ngozi
Kuhisi na kuona ngozi imekunjamana
Kubabuka kwa ngozi
Kutokwa na damu kwenye ngozi haswa kwenye michirizi ilozama zaidi
Ni wakati gani wa kumwona daktari?
Mwone daktari endapo:
Ngozi haijirudii kwenye hali yake ya awali licha ya kufanya juhudi za kujitibu mwenyewe
Ngozi inabadilika kuwa na rangi nyekundu
Unakosa usingizi
Unavidonda kwenye ngozi iliyokauka vitokanavyo na kujikuna au maambukizi
Ngozi imekauka au kukunjamana katika eneo kubwa la mwili
Vihatarishi
Mtu mwenye ngozi yenye mafuta au mwenye ngozi kavu asilia wote wanaweza kukumbwa na tatizo hilila ngozi kukauka na kupasuka. Vihatarihi vingine ni;
Umri mkubwa na kuzeeka. Umri zaidi ya miaka 40
Kutumia maji yenye chlorine kuoga mara kwa mara
Kufanya kazi zinazohusika kuzamisha mwili wako kwenye maji
Kuosha ngozi na vimiminika vya moto na mara kwa mara
Historia ya kuwa na magonjwa ya ngozi kama demataitizi
Hali ya hewa, kipindi cha baridi na joto ambapo hali ya hewa inakosa unyevu wa kutosha
Matibabu ya nyumbani
Badili mtindo wa maisha kwa kufanya mambo yafuatayo;
Kunywa maji ya kutosha
Chagua kilainisha ngozi kizuri. Mafuta ya Vaseline yasiyo na pafyumu ni mazuri zaidi
Usioge kwa kutumia maji ya moto
Usioge kila siku
Usioge zaidi ya dakika 10 kwa siku
Tumia sabuni za kuongeza unyevu kwenye ngozi unapooga
Paka mafuta ya kuleta unyevu wkenye ngozi mara unapomaliza kuoga
Usifanye scrubu au kusababisha miwasho kwenye maeneo ngozi imekauka
Endapo ni msimu wa masika au baridi, tumia mashine za kuongeza unyevu kwenye hewa kama ukiweza
Kinga
Kujikinga fanya mambo yaliyotajwa kwenye matibabu ya nyumbani pamoja na
Kuvaa glavu wakati unashika majimaji endapo unahatari ya kukauka mikono
Jifunike jinsi uwezavyo kwenye msimu wa baridi
Madhara
Kuamka kwa pumu ya ngozi
Kupata maambukizi kwenye ngozi haswa kwenye maeneo ambayo yamepasuka
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
14 Septemba 2023 16:40:33
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
Dry skin. https://www.healthline.com/health/dry-skin. Imechukuliwa 04.08.2020
Dry skin. (n.d.). aad.org/public/diseases/dry-sweaty-skin/dry-skin. Imechukuliwa 04.08.2020
Dry skin/itchy skin. (n.d.).my.clevelandclinic.org/health/diseases/16940-dry-skinitchy-skin. Imechukuliwa 04.08.2020
Dry skin. American Osteopathic College of Dermatology. http://www.aocd.org/page/DrySkin. Imechukuliwa 04.08.2020
Dry skin. American Academy of Dermatology. https://www.aad.org/public/diseases/dry-sweaty-skin/dry-skin. Imechukuliwa 04.08.2020
The McGraw-Hill Companies; 2012. http://www.accessmedicine.com. Imechukuliwa 04.08.2020
Fazio SB, et al. Pruritus: Overview of management. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 04.08.2020