Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Peter A, MD
18 Aprili 2020 09:28:12
Kupoteza uzito
Kupungua uzito/kupoteza uzito katika tiba na afya ya mwili huchangiwa kiujumla kwa kupungua kwa maji, tishu za adipozi, misuli, madini, tendoni na tishu za konectivu mwilini.
Mtu anaweza kupungua uzito kwa kudhamilia yeye mwenyewe au kutokana na magonjwa na hali mbalimbali mwilini. Wakati mwingine sababu za kupungua uzito huwa hazifahamiki. Sababu zisizofahamika zinazosababisha kupungua uzito huweza kusababisha ugonjwa unaoitwa kacheksia, ugonjwa huu huambatana na matatizo mengi mwilini.
Kupungua uzito kwa kudhamilia hupunguza hatari kubwa ya kupata magonjwa yasiyo ya kuambukizwa mfano kisukari na magonjwa ya moyo. Tafiti zinaonyesha pia kuwa hata kwa watu wenye magonjwa ya kisukari na moyo, hupata afadhari na kurejea karibu na hali ya awali kiafya wanapopunguza uzito. Ni vema kushauriwa na daktari mbobezi wa mambo ya uzito ili kuwa na matokeo mazuri zaidi ya kiafya.
Ni njia ipi sahihi ya kujua uzito sahihi unaotakiwa kuwa nao?
Je inatosha tu kupima uzito na kusema kuwa umepungua? Hapana kupungua uzito kwa kupima uzito tu hakutoshi, kuna njia nzuri ya kujua kiwango sahihi cha uzito unachotakiwa kuwa nacho. Kipimo hiko huitwa kipimo cha kiwango cha bazo metaboliki- BMI
BMI- Hupatikana kwa kupima uzito katika Kilo na kugawanywa kwa skwea ya urefu wako katika mita.
BMI= (Uwiano wa uzito kwa urefu) gawanya kwa (Urefu mara Urefu katika mita)
Makundi ya BMI
BMI chini ya 18.5
Uzito kidogo kuliko kawaida(haushauriwi kiafya)
BMI kuanzia 18.5-24.9
Ni uzito unaoshauriwa kiafya
BMI kuanzia 25-29.9
Ni uzito kupita kiasi pia huwa na hatari ya kawaida katika afya
BMI kuanzia 30 na Kuendelea
Ni uzito mkubwa kupita kiasi na hufahamika kama ugonjwa wa obeziti.
Nini huambatana na uzito mdogo kupita kiasi?
Tabia ya kuvunjika mifupa kirahisi
Matatizo ya nywele, ngozi na meno
Kuumwa mara kwa mara
Kuhisi kuchoka muda wote
Kupungukiwa damu
Kupata mzunguko wa hedhi usiokuwa na mpangilio
Kujifungua kabla ya wakati(mtoto njiti)
Kuwa na ulemavu au ukuaji mdogo
Kutokuwa kiakili vizuri kwa watoto
Kudumaa kwa umbo na akili kwa Watoto
Ugumba kwa mwanaume na mwanamke
Matatizo ya homoni mwilini(kutowiana kwa homoni)
Kudhoofika kwa mfumo wa kingi mwilini hivyo kupata magonjwa kirahisi
Vihatarishi
Historia ya kifamilia ya kuwa na uzito kidogo
Mfumo wa umeng’enyaji kwenda kwa kasi zaidi
Mazoezi ya mara kwa mara
Magonjwa sugu na ya muda mrefu mfano kuhara kwa muda mrefu, Saratani mbalimbali, Ugonjwa wa UKIMWI na Kisukari
Magonjwa ya akili
Mambo muhimu
Kuongeza ulaji wavyakula- vyakula vyenye protini na wanga kwa wingi kama jibini na siagi ,kuongeza Blueband kwenye chakula
Kula milo midogo mara kwa mara- Watu wengi huwa na uzito mdogo kutokana na kushindwa kula chakula kingi kwa muda mrefu hivyo watu hawa wanapaswa kula kidogo kidogo na mara kwa mara kwa siku. Hata hivyo pata ushauri wa daktarin ili usipate matatizo yanayoambatana na kula mara kwa mara.
Kuongeza vyakula vya zaida kwenye mlo kama maziwa, siagi na Blueband
Zingatia mlo kamili unaoshauriwa kiafya- soma Zaidi kuhusu Makala za mlo kamili kwenye tovuti hii.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023 20:02:52
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1.MedicalNewToday.Underweight.https://www.medicalnewstoday.com/articles/321612. Imechukuliwa 17/4/2020
2.NHS.Underweight.https://www.nhs.uk/live-well/healthy-weight/advice-for-underweight-adults/. Imechukuliwa 17/4/2020
3.MayoClinic.UnderWeight.https://www.mayoclinic.org/healthy-lifestyle/nutrition-and-healthy-eating/expert-answers/underweight/faq-20058429. Imechukuliwa 17/4/2020
4.Harrison Principles of Internal Medicine ISBN NI 9781259644030 Written by Tinsley R Harrison ukurasa wa 430