top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Adolf S, M.D

12 Aprili 2020 19:09:28

Kushuka kwa shinikizo la damu- Haipotensheni
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Kushuka kwa shinikizo la damu- Haipotensheni

Shinikizo la damu la chini hutokea pale endapo shinikizo la damu lipo chini ya 120/60 mmHg au kuwa chini kutoka kiwango cha kawaida ambacho mtu alikuwa nacho. Ni vema kupima shinikizo lako la damu ili kujua kwa kawaid alipo kiasi gani ili likishuka Zaidi ijulikane kuwa una shinikizo la damu la chini au juu ya kiwango chako cha kawaida.


Visababishi


Visababishi vya hsinikizo la damu la chini ni;


 • Ujauzito- kutokana na uhitaji mkubwa wa damu uliopo kati ya mama na kiumbe kilichopo tumboni.

 • Upotevu wa damu nyingi kutokana na ajali/kuumia

 • Upungufu wa maji mwilini (dihaidresheni)

 • Magonjwa ya homoni mfano ugonjwa wa addison’s, haipoglaisemia, parathairoidi na kisukari

 • Magonjwa ya moyo kama bradikadia, magonjwa ya valvu za moyo, mshituko wa moyo na kuferi kwa moyo

 • Ukosefu wa virutubisho mwilini kama vile vitamini B12 na foleti

 • Kutanuka kwa mishipa ya damu- ambapo mara nyingi husababibwa na nguvu kubwa ya msukumo wa damu kutoka kwenye moyo.

 • Maambukizi makali kwenye damu- husababisha shoku ya septiki

 • Matumizi ya dawa kama hydrochlorothiazide, prazosin, atenolol, propranolol, pramipexole, levodopa, doxepin, imipramine, sildenafil, tadalafil,


Aina


Aina za shinikizo la chini la damu ni


 • Shinikizo la damu la othostatiki

 • Shinikizo la damu la chini baada ya kula

 • Shinikizo la damu la chini linalosababishwa kuharibika kwa mfumo wa umeme wa ubongo

 • Shinikizo la chini la damu kutokana na kuharibika kwa mfumo wa neva


Shinikizo la damu la othostatiki

Hutokea endapo mtu amebadili pozi, mfano akiwa amelala na akaamka kwa ghafla, au akiwa amekaa na kuamka kwa ghafla. Mtu anashauriwa kuamka kwa hatua. Unapotaka kuamka ukiwa umelala, anza kuamka kwa kukaa kwanza sehemu uliyopo kwa dakika 3 hadi 5 kabla ya kusimama.


Shinikizo la damu la chini baada ya kula

Shinikizo la damu la chini baada ya kula kwa jina la kitiba Postprandial hypotension- hutokea mara baada ya kula chakula haswa chakula chenye wanga kwa wingi. Hutokea sana kwa wazee muda mchache baada ya kula.


Kwa kawaida, mara baada ya kula moyo huongeza mapigo na damu huelekezwa Zaidi kwenye mfumo wa chakula ili kubeba chakula kilichofyonzwa na utumbo na wakati huo baadhi ya mishipa ya damu sehemu zingine za mwili kama figo n.k husinyaa ili shinikizo la damu lisishuke. Baadhi ya watu jambo hili huwa halitokei, hivyo hupata kizunguzungu, kuzimia na kuanguka.


Watu wanaoathirika zaidi ni wale wenye matatizo shinikizo la damu la juu na magojwa ya mfumo wa neva wa automatiki mfano wagonjwa wa parkinson’s.


Shinikizo la damu la chini linalosababishwa kuharibika kwa mfumo wa umeme wa ubongo

Shinikizo la damu hushuka wakati wa kusimama kwa muda mrefu haswa kwa Watoto na vijana wadogo. Hii husababishwa na kuharibika kwa mawasilainano kati ya ubongo na moyo wakati wa kusimama kwa muda mrefu.


Shinikizo la chini la damu kutokana na kuharibika kwa mfumo wa neva

Shinikizo la chini la damu kutokana na kuharibika kwa mfumo wa neva hujulikana kwa jina jingine la sindromu ya Shy-Drager


Mishipa ya autonimiki inayofanya kazi za kurekebisha shinikizo la damu huharibiwa na hivyo dalil huambatana na shinikizo la juu la damu wakati umelala chini na shinikizo dogo unapokuwa umesimama.


Dalili


Dalili za shinikizo la chini la damu- (Haipotesheni)


 • Kizunguzungu / maumivu ya kichwa

 • Kuishiwa nguvu

 • Mwili kuwa mnyonge

 • Kuzimia

 • Kuhisi kiu sana

 • Kichefuchefu

 • Kupumua haraka haraka au kwa shida

 • Kushindwa kuwa makini

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

19 Julai 2023 20:03:35

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1.Kaufman H, et al. Mechanisms, causes and evaluation of orthostatic hypotension. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 11.04.2020

2.Understanding blood pressure readings. American Heart Association. http://www.heart.org/HEARTORG/Conditions/HighBloodPressure/AboutHighBloodPressure/Understanding-Blood-Pressure-Readings_UCM_301764_Article.jsp. Imechukuliwa 11.04.2020

3.Kaplan NM, et al. Ambulatory and home blood pressure monitoring and white coat hypertension. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 11.04.2020

4.Kaufman H, et al. Treatment of orthostatic and postprandial hypotension. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 11.04.2020

5.Hypotension. National Heart, Lung, and Blood Institute. https://www.nhlbi.nih.gov/book/export/html/4880. Imechukuliwa 11.04.2020

6.Low blood pressure. American Heart Association. http://www.heart.org/HEARTORG/Conditions/HighBloodPressure/AboutHighBloodPressure/Low-Blood-Pressure_UCM_301785_Article.jsp. Imechukuliwa 11.04.2020

bottom of page