Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Sospeter B, MD
24 Februari 2021, 09:43:40
Maumivu ya misuli
Maumivu ya misuli si ugonjwa bali ni hali au tatizo Fulani linaloendelea ndani ya mwili. Baadhi ya visababishi vikuu huwa ni mgandamizo, matumizi makubwa ya misuli, msongo wa misuli au ndani ya misuli.
Maumivu ya misuli yanaweza tokea kwenye misuli ya kundi moja au misuli yote ya mwilini. Maumivu yanayokuwa misuli yote ya mwili mara nyingi husababishwa na ugonjwa, madhara ya dawa au maambukizi mwilini
Visababishi
Visababishi vikuu vya maumivu ya misuli katika Makala hii vimegawanywa sehemu 5 mbalimbali ambazo ni;
Maambukizi
Magonjwa ya shambulio la kinga ya mwili
Majeraha kwenye misuli
Matumizi ya baadhi ya dawa
Madhaifu ya mfumo wa fahamu wa misuli
Maambukizi kwenye misuli
Maambukizi kwenye misuli yanaweza kutona na;
Virusi vya mafua
Ugonjwa wa lyme
Ugonjwa wa Rocky Mountain spotted fever unaosababishwa na kung’atwa na kupe
Malaria
Trichinosis
Ugonjwa wa COVID-19
Magonjwa ya shambulio la kinga ya mwili
Magonjwa haya hutokana na kinga ya mwili kushambulia mwili wako ikizani kuwa ni ugonjwa, mfano wake ni
Ugonjwa wa Myositis
Ugonjwa wa Polymyositis
Ugonjwa wa Lupus
Ugonjwa wa Multiple sclerosis
Majeraha kwenye misuli
Maumivu ya misuli yanayweza kutokea wakati unafanya mazoezi au kufanya kazi inayotumikisha misuli. Maumivu ya misuli kutokana na matumizi ya misuli hutokea masaa kadhaa baada ya kitendo cha kutumia misuli. Unaweza kupata maumivu ya misuli yanayochelewa kutokea endapo;
Umeanza kufanya mazoezi kwa mara ya kwanza
Umeongeza shughuli ingine kwenye mazoei unayofanya
Umeongeza kiwango cha mazoezi kwenye mazoezi unayofanya kama kuongeza uzito unaonyanyua, kukimbia kwa kasi zaidi n.k
Kufanya mazoezi au shughuli inayotumia misuli mara nyingi zaidi bila kuwa na mapumziko
Hata hivyo baadhi ya hali na mambo yanayoweza kupelekea kupelekea maumivu ya misuli ni pamoja na;
Majeraha kwenye misuli ya tumbo
Majeraha misuli ya nyuma ya mgongo
Kuvunjika kwa mfupa
Syndrome ya myofascial inayotokana na kutumika sana kwa misuli
Tatizo la tendinitis
Tatizo la tendinosis
Matumizi ya baadhi ya dawa
Baadhi ya dawa huweza kusababisha maumivu ya misuli ya muda mfupi au muda mrefu. dawa hizi huweza kusababisha uvimbe kwenye misuli unaotokana na mwitikio wa kinga za mwili au kuamsha hisia za mfumo wa maumivu.
Dawa zinazoweza kusababisha maumivu ya misuli ni pamoja na;
Dawa za saratani
Dawa jamii ya ACE inhibitor zinazotumika kushusha shinikizo la juu la damu kaa vile;
Benazepril (Lotensin)
Captopril.
Enalapril (Vasotec)
Fosinopril.
Lisinopril (Prinivil, Zestril)
Moexipril.
Perindopril.
Quinapril (Accupril)
Ramipril (Altace)
Trandolapril
Dawa jamii ya statins
Atorvastatin (Lipitor®)
Fluvastatin (Lescol. ®)
Lovastatin (Mevacor®)
Pravastatin (Pravachol®)
Rosuvastatin (Crestor®)
Simvastatin (Zocor®)
Madhaifu ya mfumo wa fahamu wa misuli
Magonjwa yatokanayo na madhaifu ya mfumo wa fahamu wa misuli yanayoweza kupelekea maumivu ya misuli ni pamoja na;
Ugonjwa wa amyotrophic lateral sclerosis
Ugonjwa wa kuisha kwa misuli (muscular dystrophy)
Ugonjwa wa myasthenia gravis
Ugonjwa wa spinal muscular atrophy
Visababishi vingine
Sababu zingine zinazoweza kusababisha maumivu ya misuli ni pamoja na;
Kupotea kwa usawia wa madini kwenye damu
Magonjwa ya mishipa ya damu ya pembeni
Msongo au kugandamizwa kwa misuli
Saratani kama vile saratani ya sarcoma na damu
Shinikizo la juu kwenye misuli
Sindromu ya uchovu mkali
Tatizo la Hypothyroidism
Ugonjwa wa fibromyalgia
Vipimo
Vipimo vitategemea kisababishi ambacho kimeonekana kutokana na historia ambayo daktari ataichukua kwako na uchunguzi wa awali wa kuangalia mwili wako.
Baadhi ya vipimo vinavyoweza kufanyika ni pamoja na;
Kipimo cha FBP
Kipimo cha serum electrolyte
Kipimo cha CT scan au MRI
Kipimo cha Ultrosound
Kipimo cha Discography au Myelogram
Kipimo cha Nerve block
Matibabu
Matibabu yatategemea kisababishi kilichofahamika. Daktari wako anaweza kuamua matibabu yako kulingana na hali ya mwili wako. Hata hivyo matibabu kwa ujumla huhusisha , matibabu ya dawa za maumivu ili kuondoa dalili na matibabu ya mazoezi ya maalumu ya misuli ya mwili
Matibabu ya nyumbani
Ili kuzuia kuendelea kwa maumivu ya misuli unaweza kufanya mambo yafuatayo
Pumzisha mwili wako
Kama maumivu ya misuli ni makali, fikiria kuhusu kupumzika au kupumzisha misuli ya wili wako ili kuipa muda wa kupona na kutoendelea kwa majeraha
Endapo maumivu ya misuli yametokana na mazoezi, endelea kufanya mazoezi, hii itapalekea seli za hisia za maumivu kuhisi kuzoea maumivu na kisha maumivu yatapotea
Kanda kwa kutumia barafu iliyotiwa kwenye mfuko wa plastiki eneo lenye maumivu ya misuli kwa muda wa dakika 15 hadi 20 kila baada ya masaa nane
Tumia kigandamiza misuli ili kupunguza uvimbe endapo una uvimbe kwenye misuli
Weka eneo lenye maumivu ya misuli juu ya usawa wa moyo ili kupunguza uvimbe. Mfano unaweza weka miguu juu ya mto wakati umelala n.k
Tumia dawa za maumivu kwa maumivu sugu au ya muda mrefu. Utahitaji ushauri wa daktari wako dawa gani utumie na kwa muda gani
Fanya mazoezi ya kunyoosha misuli yako pamoja na mazoezi ya kuondoa maumivu ya misuli. Utahitaji ushauri pia wa mtaalamu wa mazoezi ya misuli kuhusu mazoezi gani unatakiwa kufanya
Fanya shughuli zinazopelekea kupunguza msongo wkenye misuli na akili yako. Unaweza fanya mazoezi ya yoga au kuwa na muda wa tafakuri ya kina
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023, 19:54:12
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1.Shmerling RH. Approach to the patient with myalgia. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 24.02.2021
2.LeBlond RF, et al. The spine, pelvis and extremities. In: DeGowin's Diagnostic Examination. 10th ed. New York, N.Y.: McGraw-Hill Education; 2015. http://www.accessmedicine.com. Imechukuliwa 24.02.2021
3.Muscle cramps. Merck Manual Professional Version.http://www.merckmanuals.com/professional/neurologic-disorders/approach-to-the-neurologic-patient/muscle-cramps. Imechukuliwa 24.02.2021
4.American Academy of Orthopaedic Surgeons. Sprains, strains and other soft tissue injuries. http://orthoinfo.aaos.org/topic.cfm?topic=A00111. Imechukuliwa 24.02.2021
5.Aronson JK, ed. Angiotensin-converting enzyme inhibitors. In: Meyler's Side Effects of Drugs. 16th ed. Amsterdam, Netherlands: Elsevier; 2016. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 24.02.2021
6.Understanding Muscle Soreness – How Much is Too Much?.https://www.kidney.org/content/understanding-muscle-soreness-%E2%80%93-how-much-too-much. Imechukuliwa 24.02.2021
7.Inflammatory Myopathies Fact Sheet. https://www.ninds.nih.gov/Disorders/Patient-Caregiver-Education/Fact-Sheets/Inflammatory-Myopathies-Fact-Sheet. Imechukuliwa 24.02.2021