top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Adolf S, MD

5 Desemba 2020 10:26:22

Mipasuko/vidonda njia ya haja kubwa
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Mipasuko/vidonda njia ya haja kubwa

Vidonda njia ya haja kubwa au mipasuko kwenye njia ya haja kubwa katika makala hii imetumika kumaanisha tatizo linalofahamika kitiba kama anal fissure.


Anal fissure ni tatizo linalofahamika sana kitiba, hutokea kwenye umri wowote ule na kisabaishi kikuu huwa ni kupitisha haja kubwa ngumu. Haja ngumu inapopita kwenye njia ya haja kubwa husababisha njia hii kuchanika. Dalili zinazo ambatana ni maumivu pamoja na damu nyekundu kwenye kinyesi.


Tatizo hili si la kukuogopesha kwani linafahamika kisababishi na linatibika kwa matibabu ya nyuumbani ndani ya wiki mbili kwa kufuata ushauri wa kitaalamu na chakula. Endapo tatizo limeendelea kwa muda wa wiki sita, kitaalamu tatizo hili litakuwa ni sugu. Hata hivyo endapo umefanya matibabu ya nyumbani bila mafanikio kwa kipinid cha wiki mbili, unatakiwa onana na daktari wako kwa uchunguzi na tiba.


Dalili


 • Mwonekano wa kidonda au mpasuko katika mdomo wa njia ya haja kubwa

 • Mwonekano wa kipele au kiuvimbe kidogo pembezoni mwa mpasuko

 • Maumivu makali eneo la mdomo wa haja kubwa wakati wa kujisaidia haja kubwa

 • Muamivu ya njia ya haja kubwa hata baada ya ujisaidia

 • Mwonekano wa mstari wa damu kwenye kinyesi au kwenye tishu ya kujisafishia njia ya haja kubwa

 • Kutokwa na uchafu unaonuka kutoka njia ya haja kubwa

 • Kushindwa kukojoa au kukojoa mara kwa mara

 • Hisia za kuungua au kuwashwa sehemu za siri


Visababishi


Ni nini husabaisha mipasuko kwenye njia ya haja kubwa?

Mipasuko njia ya haja kubwa huchangiwa na kupitisha haja ngumu kwa asilimia zaidi ya 80. Sababu nyingine ni kuharisha kwa muda mrefu sana. Hata hivyo visababishi vingine ni;


 • Kutumia ngumu sana kusukuma kinyesi wakati wa kujisaidia

 • Ugonjw a wa cronh’s unaosababisha kuharisha kwa muda mrefu

 • Kuingiza kitu kigeni ndani ya njia ya haja kubwa

 • Kupungua kwa damu inayoenda kwenye eneo la haja kubwa

 • Kubana kwa misuli ya njia ya haja kubwa kutokana na degedege la misuri hiyo

 • Kuwa na Saratani ya njia ya haja kubwa

 • Kuwa na UKIMWI

 • Kuugua Kifua kikuu

 • Kuugua Kaswende


Vihatarishi


Vihatarishi vya kupata tatizo hili ni;


 • Kupata haja ngumu mara kwa mara

 • Kujifungua

 • Uzee

 • Kuwa na magonjwa yanayoleata kuharisha kwa muda mrefu kama magonjwa ya inflammatory bowel


Vipimo


Vipimo vya utambuzi


Ili kutambua mipasuko njia ya haja kubwa daktari wako atakuchunguza kwenye njia hiyo. Uchunguzi wa ndani ya njia ya haja kubwa pia unaweza fanyika endapo kuna uhaja kwa kuingiza kidole au kifaa maalumu (anoscope) ili kuweza kuona kama kuna shida yoyote ndani ya njia ya haja kubwa.


 • Matibabu ya hospitali

 • Matibabu ya dawa.


Mfano dawa za Nitroglycerin Ointment na Calcium Channel Blockers


Upasuaji

Endapo matibabu ya nyumbani yaliyoorodheshwa hapo juu hayajafanya kazi ndani ya wiki mbili, utahitajika kuonana na daktari wako kwa matibabu. Matibabu unayowez akufanyiwa hospitali ni;


Matibabu ya upasuaji

Hufanyika kwa wagonjwa ambao hawajapona kwa matibabu ya nyumbani . daktari atapasua na kufungua mipasuko ya njia ya haja kubwa na tatizo lako litaondoka kabisa.


Kumbuka

Endapo dalili zako hazijaisha ndani ya iwki mbili onana na daktari kwa ushauri na matibabu zaidi


Matibabu ya nyumbani

Matibabu hulenga kutibu kisababishi, hata hivyo matibabu ya mipasuko njia ya haja kubwa si makubwa na yanaweza kufanyika nyumbani kwako. Fuata ushauri ufuatao kujitibu mwenyewe nyumbani;


 • Tumia dawa za kulainisha haja kubwa ili itoke laini na kirahisi pasipo kuumiza kidonda

 • Kunywa maji ya kutosha kufanya haja yako kubwa iwe laini

 • Tumia dawa za kuongeza nyuzinyuzi ili kufanya haja kubwa itoke kirahisi

 • Kula vyakula vyenye nyuzinyuzi kwa wingi mfano mboga za majani, vyakula vya nafaka ambavyo havijakobolewa matunda kama parachichi, tango n.k

 • Kalia maji ya uvuguvugu yenye detol ili kulainisha kidonda na kuondoa miwasho na bakteria ili kuupa muda kidonda chako kupona haraka

 • Tumia mafuta yenye nitroglycerine ili kufanya mzunguko wa damu uongezeke kwenye njia ya haja kubwa na kufanya upone haraka.

 • Dawa za kuzuia miwasho za kupaka mfano dawa jamii ya hydrocortisone na cetirizine zinaweza kutumika kama kuna miwasho mingi sehemu hii

 • Tumia dawa za maumivu za kupaka mfano dawa zenye lidocaine endapo unakerwa na hali ya maumivu maeneo hayo

 • Soma zaidi makala mbalimbali kuhusu afya yako ili kuwa na ufahamu na kujikinga na magonjwa yanayozuilika


Namna ya kujikinga


 • Safisha njia ya haj akubwa kisahihi na kisha ikaushe isiwe na unyevu unyevu

 • Tumia sabuni kusafisha njia ya haja kubwa, usitumie nguvu safisha kwa utaratibu

 • Unapokuwa unasafisha njia ya haja kubwa Kenya kidogo kama unataka kutoa haja kubwa kisha shikiria hao hapo huku unasafisha kwa maji safi na sabuni

 • Kunywa maji ya kutosha kila siku katika kiwango kinachoshauriwa kiafya(soma zaidi kuhusu makal ahii kwneye tovuti hii)

 • Kula vyakula vyenye nyuzinyuzi kwa wingi mfano mboga za majani, vyakula vya nafaka ambavyo havijakobolewa na matunda

 • Fanya mazoezi katika mpangilio maalumu na kwa jinsi inavyoshauriwa kitaalamu(soma katika makala za mazoezi ndani ya tovuti hii ya ULY CLINIC)

 • Endapo una harisha, pata matibabu mara moja ili tatizo lisiwe sugu

 • Kwa watoto hakikisha unawabadilisha pampasi haraka iwezekanavyo baada ya kujisaidia

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

19 Julai 2023 19:54:47

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1. Anal Fissures. https://www.ucsfhealth.org/education/anal-fissures. Imechukuliwa 2.12.2020
2. Anal Fissures . https://my.clevelandclinic.org/health/diseases/13177-anal-fissures. Imechukuliwa 2.12.2020
3. Maged Nasr, Hussin Ezzat etal. Botulinum Toxin Injection Versus Lateral Internal Sphincterotomy in the Treatment of Chronic Anal Fissure: A Randomized Controlled Trial .https://link.springer.com/article/10.1007/s00268-010-0736-5. Imechukuliwa 2.12.2020
4. Anal Fissure Expanded Information. https://fascrs.org/patients/diseases-and-conditions/a-z/anal-fissure-expanded-information. Imechukuliwa 2.12.2020
5. Steven Schlichtemeier, etal. Anal fissure. https://www.nps.org.au/australian-prescriber/articles/anal-fissure. Imechukuliwa 2.12.2020

bottom of page