top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

ULY CLINIC

Msongo mkali wa kupumua
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

6 Aprili 2026, 12:19:35

Msongo mkali wa kupumua

Dalili za msongo mkali wa kupumua ni zipi(ARDS)


Msongo mkali wa kupumua ni tatizo hatari la kupumua linalosababisha matumizi makubwa ya misuli ya ziada kutokana na upungufu wa oksijeni. Huambatana na kushuka kwa mbavu na kifua wakati wa kuvuta hewa na sauti ya mguno wakati wa kutoa hewa. Dalili nyingine ni kupumua kwa kasi, shida ya kupumua, jasho jingi , milio ya mapafu iliyosambaa (krako), na kikohozi chenye makohozi ya rangi ya waridi na mapovu. Upungufu mkali wa oksijeni husababisha wasiwasi, mpwito wa moyo wa kasi (tachycardia), na kuchanganyikiwa kiakili.


Muhtasari wa Masongo mkali wa Kupumua (ARDS)

  • Tatizo hatari la kupumua linalosababishwa na upungufu wa oksijeni.

  • Matumizi ya misuli ya ziada ya kupumua huongezeka, na kuna kushuka kwa mbavu na kifua wakati wa kuvuta hewa, pamoja na mguno wakati wa kutoa hewa.

  • Dalili kuu: Kupumua kwa kasi (tachypnea), kupumua kwa shida, jasho jingi, milio ya mapafu (krako), na kikohozi chenye makohozi yenye mapovu ya waridi.

  • Athari za upungufu mkali oksijeni: Wasiwasi, mpwito wa moyo wa kasi, na kuchanganyikiwa kiakili.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 15:59:23

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

​

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

ULY CLINIC

bottom of page