Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
ULY CLINIC

6 Aprili 2026, 12:14:12
Nimonia
Dalili na ishara za nimonia ni zipi?
Nimonia inayosababishwa na bakteria husababisha matumizi makubwa ya misuli ya ziada kwa kupumua. Kawaida, maambukizi haya huanza ghafla na homa kali pamoja na baridi kali.
Dalili na ishara zinazohusiana na nimonia ni:
Maumivu ya kifua,
Kikohozi chenye makohozi,
Kupumua kwa shida na kupumua haraka,
Mapigo ya moyo haraka (tachycardia),
Sauti ya kwikwi wakati wa kutoa pumzi
Ngozi na midomo kuwa buluu,
Kutokwa na jasho,
Sauti laini za mpasuko kwenye mapafu (Krako laini).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 15:59:23
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
ULY CLINIC
