Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
6 Mei 2020 10:02:17
Nyuropathi ya pembezoni
Ugonjwa wa neva ni matokeo ya kujeruhiwa kwa ubongo na uti wa mgongo. Majeruhi husababisha udhaifu wa neva, ganzi na maumivu hasa kwenye miishio ya mwili kama vile mikononi na miguuni hata hivyo pia sehemu mbalimbali za mwili huweza kuathiriwa.
Makala hii imezungumzia dalili za nyuropathi ya pembezoni ikimaanisha nyuropathi kwenye viungo vyua miguu na mikono na huitwa kwa lugha nyingine ya peripheral neuropathy
Mfumo wa neva hutuma taarifa kutoka kwenye ubongo na uti wa mgongo kwenda sehemu zingine za mwili kupitia kemikali zinazoitwa nyurotransmita na kupitia mishipa ya fahamu. Taarifa hizi huenda maeneo husika na zingine hurejesha ujumbe au kuleta ujumbe mpya kwenye ubongo na uti wa mgongo.
Magonjwa ya nyuropathi huweza kusababishwa na magonjwa ya uti wa yanayosababishwa na ajali , maambukizi, magonjwa ya kurithi ,sumuna kisababishi kukuu ni ugonjwa wa kisukari.
Dalili
Kuanza taratibu kuhisi ganzi ,kuhisi hali ya kuchomwa chomwa kwenye miguu au mikono ambayo husambaa kwenda kwenye vidole vya miguu na mikono
Kupata maumivu makali au ya kuchoma
Kutohisi maumivu kabisa
Kukosa uwiano wa kutembea na kuanguka
Misuli kuwa dhaifu
Kuhisi kama umevaa soki na wakati hujavaa au kuhisi kama umevaa glovu wakati hujavaa
Kupooza
Dalili za kuathiriwa kwa neva za autonomic
Kushindwa kuvumilia joto
Kutokwa sana au kutotokwa na jasho kabisa
Matatizo ya kushindwa kutoa mkojo na kupat ahaja kubwa
Kuhisi kizunguzungu
Visababishi
Magonjwa yanayoshambulia mfumo wa kinga za mwili kama baridi yabisi na Ukimwi na Ukoma
Ugonjwa wa kisukari ,Nusu ya wagonjwa hawa huwa hupata nyuropathi
Maambukizi mbalimbali kama ya bakteria na Virusi (Epstain Bar, Hepatitis), Virusi vya Ukimwi)
Magonjwa ya kurithi ya neva
Saratani mbalimbali ambazo huweza kukandamiza neva na kuzuia utendaji kazi wake.
Magonjwa mengine kama ya figo na ini
Jinsi ya kujikinga
Kula mlo kamili kutoka kwenye makundi matano ya chakula, usisahau chakula chenye mboga za majani kwa wingi na matunda huku ukiepuka vyakula vyenye Mafuta na sukari kwa wingi
Kuwa na ratiba maalumu ya mazoezi angalau dakika 30 kwa siku katika siku 3 au 4 za wiki
Jiepushe na sababu zote zinazosababisha magonjwa ya neva
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
8 Oktoba 2021 04:53:29
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1.Peripheral neuropathy fact sheet. National Institute of Neurological Disorders and Stroke. http://www.ninds.nih.gov/disorders/peripheralneuropathy/detail_peripheralneuropathy.htm. Imechukuliwa 16.04.2020
2.What is peripheral neuropathy. The Foundation for Peripheral Neuropathy. https://www.foundationforpn.org/what-is-peripheral-neuropathy/. Imechukuliwa 16.04.2020
3.Rutkove SB. Overview of polyneuropathy. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 16.04.2020
4.Feldman EL, et al. Treatment of diabetic neuropathy. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 16.04.2020
5.WebMd.PeripheralNeuropathy.https://www.webmd.com/brain/understanding-peripheral-neuropathy-basics. Imechukuliwa 16/4/2020
6.HealthLine.PeripheralNeuropathy.https://www.healthline.com/health/peripheral-neuropathy. Imechukuliwa 16/4/2020
7.Harrison Principles of Internal Medicine ISBN NI 9781259644030 Written by Tinsley R Harrison ukurasa wa 754