Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
ULY CLINIC

6 Aprili 2026, 12:23:42
Peritonitisi
Dalili za peritonitis ni zipi?
Dalili za Peritonitis (Uvimbe wa utando wa ndani wa tumbo)
Peritonitis ni hali ya dharura ya kitabibu inayotokea pale utando unaofunika viungo vya tumbo (peritoneum) unapopata maambukizi au muwasho mkali. Dalili zake hutegemea chanzo, kiwango cha maambukizi, na kama imeathiri sehemu moja tu au tumbo lote.
1. Dalili kuu za tumbo
Maumivu ya tumbo
Huja ghafla na huwa makali sana
Huongezeka mtu anapoguswa au kusogea
Mgonjwa hupendelea kukaa kimya bila kusogea (movement worsens pain)
Huwa ya sehemu moja (localized) au huenea kote tumboni (generalized)
Ukakamavu wa tumbo
Misuli ya tumbo hukaza bila hiari
Tumboni huhisika kama ubao mgumu
Inaweza kuwa:
Sehemu fulani (mfano upande wa chini kulia)
Tumboni kote (peritonitis iliyoenea)
Kujikinga kwa tumbo
Mgonjwa hukaza tumbo ili kuepuka maumivu
Daktari akibonyeza, maumivu huongezeka ghafla mkono unapoondolewa sehemu iliyobonyezwa
Kuvimba au kujaa kwa tumbo
Tumboni huonekana limepanuka
Gesi na kinyesi hushindwa kupita
Kupungua au kutokuwepo kwa sauti za utumbo
Utumbo hupooza (paralytic ileus)
Hakuna mlio wa mmeng’enyo wa chakula
2. Dalili za mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
Kichefuchefu
Kutapika
Kukosa hamu ya kula
Kukosa haja kubwa au gesi
Kuhisi tumbo limejaa sana
3. Dalili za mwili mzima
Hizi huonyesha maambukizi yameanza kuenea mwilini (sepsis):
Homa
Baridi kali
Mapigo ya moyo kwenda kasi
Kupumua haraka
Shinikizo la damu kushuka
Uchovu mkubwa au kuchanganyikiwa
Ngozi kuwa baridi au yenye jasho
4. Dalili hatari sana (dharura)
Mtu akionyesha mojawapo ya hizi anahitaji kufika au kufikishwa hospitali haraka sana:
Tumbo kuwa gumu kama jiwe
Kushindwa kusimama kwa sababu ya maumivu
Kutapika mara kwa mara au kutapika damu
Kuzimia au kuchanganyikiwa
Kupumua haraka sana
Shinikizo la damu kushuka (dalili za mshtuko wa kseptiki)
Muhtasari mfupi wa Peritonitis
Peritonitis husababisha maumivu makali ya ghafla ya tumbo yanayoambatana na ukakamavu wa misuli ya tumbo na kuuma sana unapoguswa. Mgonjwa pia hupata kichefuchefu, kutapika, tumbo kujaa, na kupotea kwa sauti za mnjongeo wa utumbo.
Kadri hali inavyozidi kuwa mbaya, hutokea homa, mapigo ya moyo kwenda kasi, kupumua haraka, na kushuka kwa shinikizo la damu — ishara kwamba maambukizi yameanza kuwa hatari kwa maisha.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 15:59:23
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
ULY CLINIC
