Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Peter A, MD
5 Novemba 2021 09:48:32
Saratani ya ulimi
Aina kadhaa za saratani zinaweza kuathiri ulimi na mara nyingi huanzia kwenye ukuta wa ngozi ya ulimi uliotengenezwa na seli za squamous. Matibabu na hatima ya saratani ya ulimi hutegemea aina ya saratani iliyoathiri ulimi. Saratani ya ulimi inayotokea sehemu za mdomo ambapo itakuwa rahisi kuonekana kwa macho huweza kutibiwa mapema mara inapoonekana na kuzuia madhara, saratani ya ulimi inayotokea nyuma karibu na koo au kwenye shina la ulimi si rahisi kuonekana na hivyo huweza kugunduliwa katika hatua za juu Zaidi wakati tatizo tayari limeshakuwa kubwa.
Dalili za saratani ya ulimi hutegemea hatua ya sawatani, baadhi yake ni;
Kidonda kwenye ulimi ambacho hakiponi
Uvimbe kwenye ulimi
Maumivu ya ulimi yanayoambatana na uvimbe au kidonda
Maumivu wakati wa kumeza chakula
Kumeza kwa shida
Mabadiliko ya sauti (kuwa na sauti kama ya farasi au sauti kukauka)
Maumivu kwenye taya
Kuhisi kitu kinakaba kwenye koo
Shida katika kumeza au kutafuna chakula
Vidonda kwenye ulimi ambavyo haviponi
Ganzi mdomonikutokwa na damu kwenye ulimi bila sababu
Uvimbe kwenye ulimi ambao hauondoki
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023 20:02:03
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada