top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

5 Mei 2020 07:30:17

Siku ya kupata mimba- Ovulesheni
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Siku ya kupata mimba- Ovulesheni

Ovulation ni kitendo cha kutolewa kwa yai kutoka kwenye ovari, yai linapotolewa na ovari husafirishwa kwenda kwenye mji wa mimba(mfuko wa uzazi) kupitia mirija ya fallopio.


Mwanamke akiwa kweney ovulation huwa kwenye kipindi cha kupata mimba kirahisi. Kipindi hiki kinaweza kuitwa kipindi cha hatari kwa mwanamke, au kipindi cha kupata mimba.


Yai linapokuwa linasafiri kutoka kwenye ovari kwenda kwenye mji wa mimba, linaweza kukutana na mbegu za kiume(manii) endapo mtu atakuwa ameshiriki tendo la kujamiiana masaa 24 ndani ya yai kutolewa. Mara nyingi yai hurutubishwa na manii kwenye mirija ya falopio.


Mwanamke mwenye afya njema na ovari zinazofanya kazi, hutoa yai moja kila mwezi mara moja siku 12 hadi 14 kabla ya siku ya kuona damu ya hedhi kwa mwanamke mwenye mzunguko wa hedhi wa siku 28.


Mambo muhimu ya kufahamu


  • Si kila mwanamke yai hutolewa siku ya 12 hadi 14

  • Mwanamke mwenye mzunguko wa siku 28 hadi 32, yai lao hutolewa kati ya siku ya 10 hadi ya 19, asilimia kubwa sana ni siku ya 12 hadi ya 16 kabla ya kuona damu ya hedhi

  • Kwa mwanamke mwenye afya njema yai hutolewa siku ya 14

  • Kama mzunguko wako ni siku 35 basi yai hutolewa siku ya 21 na kama mzunguko wako ni siku 21 basi yai hutolewa siku ya 7.


Pia baadhi ya wanawake mizunguko yao huwa haina mpangilio maalumu hii ni kutokana na hali mbalimbali kama kutumia dawa za uzazi wa mpango na maudhi ya dawa zingine.


Wakati gani wa kujamiana ili kupata mimba?


  • Yai hurutubishwa ndani ya masaa 24 baada ya yai kutolewa endapo utajamiana

  • Si lazima ujamiane siku hiyo hiyo ya yai kutolewa ili kuweza kupata mimba

  • Kujamiiana siku mbili hadi tatu kabla ya yai kutoka huweza kupelekea mwanamke kupata mimba

  • Hivyo katika mzunguko zipo siku 6 ambazo urutubishwaji unaweza kutokea


Dalili za ovulation


  • Joto la mwili huwa juu kupita siku zingine

  • Ute ute wa kwenye uke hubadilika kutokana na homon ya Estrogen kuzalishwa kwa wingi

  • Matiti kuuma unapoyashika au kuwasha

  • Maumivu kidogo kwenye nyonga au tumbo

  • Kutokwa kwa maji kidogo kama ya kahawia hivi ukeni

  • Hamu ya mapenzi huongezeka

  • Mlango wauzazi huwa laini na hufunguka

  • Sehemu ya nje ya uke huonekana kuvimba

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

8 Oktoba 2021 04:53:35

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

bottom of page