Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Sospeter B, MD
3 Machi 2021 11:28:17
Syndrome ya Asherman
Sindromu ya asherman kwa jina jingine hufahamika kama makovu mshikamano ndani ya mfuko wa kizazi ,hutokea pale endapo makovu yametengenezwa ndani ya kiwili cha kizazi pamoja na au maeneo ya ya shingo ya uzazi. Makovu hutokea kama matokeo ya upasuaji wa kizazi au kama matokeo ya kukwanguliwa ndani ya kizazi au kuwa matokeo ya maambukizi ya baadhi ya magonjwa yanayoathiri ndani ya uzazi.
Visababishi
Makovu ndani ya kizazi hutokea awali kama matokeo ya kukwanguliwa ndani ya kizazi wakati wa kutoa mimba, wakati wa kusafisha kizazi baada ya mimba kutoka au wakati wa kutoa kondo la nyuma lililong’ang’ania baada ya kujifungua.
Wakati mwingine makovu haya huweza kutokea kama matokeo ya kutolewa sampuli kwa ajili ya kupima saratani, kutolewa uvimbe wa fibroid.
Magonjwa kama TB na Kichocho cha mkojo kinaweza kuathiri pia mji wa uazi na kusababisha makunyazi ndani ya mfuko wa kizazi.
Epidemiologia
Tatizo hili halifahamiki sana ingawa lipo, hii ni kwa sababu ya kutolifikiria, lakini huwa na dalili za kupelekea wanawake kupata hedhi au damu ya mwezi kidogo sana. Asilimia 13 ya wanawake wanaotoa mimba kwenye miezi mitatu ya kwanza hupata tatizo hili na asilimi 30 pia ya wanawake wanaokwanguliwa kizazi baada ya mimba kutoka kipindi baada ya miezi mitatu kupita hupata tatizo hili.
Wanawake wanaorudia rudia kufanya usafishaji wa kizazi kwa njia ya kukwanguliwa, huongeza hatari mara dufu ya kupata makunyanzi ndani ya mfuko wa kizazi.
Pathophysiologia
Syndrome ya Asherman hutokea pale endapo kumetokea majeraha kwenye ukuta wa endometria , ukuta wa ndani ya kizazi ambao huhusika katika kushikilia kijusi mara baada ya kuchavushwa. Majeraha huamsha chembe za mwili zinazosababisha michomo kutokea kwenye ukuta huu kisha kupona kwa kuleta makovu
Dalili
Wanawake wenye syndrome ya Asherman huweza kuwa na dalili zifuatazo;
Kupata hedhi nyepesi au kutokuona hedhi kabisa
Kuwa na hedhi ya kawaida endapo sehemu ndogo tu ya kizazi imeathiriwa
Maumivu makali wakati wa hedhi licha ya kutokupata damu ya hedhi
Kutoka kwa mimba kunakojirudia rudia
Vipimo
Vipimo cha vhicochezi
Oestrogen
Progesterone
FSH
Kipimo cha Hysterosalpingography
Kipimo hiki kinaweza kuangalia kwenye mirija na mfuko wa uzazi kwa ujumla
Matibabu
Matibabu upasuaji
Matibabu ya tatizo haya yanapaswa kufanywa na daktari wa upasuaji mzoefu kwenye tatizo hili. Matibabu huhusisha kutoa makovu yaliyokwisha tengenezwa kwa kutumia vifaa maalumu vinavyoweza. Baada ya upasuaji unaweza kuwekewa kifaa maalumu cha kuzuia kushikamana kwa kuta za kizazi na kufanyika kwa makovu zaidi.
Matibabu mengine yanafanyiwa majaribio kwa sasa ambayo baadaye yanaweza kuwa faida kwa wanawake baadaye ni matibabu ya kupandikizwa kwa chembe asilia za ukuta wa mji wa uzazi kutoka kwenye sehemu ya uzazi ambayo haijaathiriwa.
Tafiti zinafanyia kazi pia matibabu ya dawa za kuyeyusha makovu jamii ya hyaluronidase ambazo zinaonyesha kuja leta matokeo mazuri hapo baadae
Madhara
Sindromu ya Asherman's huweza pelekea;
Kujirudia kutoka kwa mimba licha ya kupata matibabu ya upasuaji na dawa
Kutokea kwa saratani ya mji wa uzazi, hatari huwa kidogo ukilinganisha na wanawake wasio na tatizo hili hata hivyo huchelewa kupata dalili kama wanawake wengine wenye kizazi kisicho na makovu
Madhara ya ujauzito kama kupata uchungu kabla ya wakati, kujifungua mtoto njiti au mwenye uzito kidogo sana, kujishikiza kwa kondo la nyuma kwenye misuli ya uzazi na kushindwa kukamilika kwa hatua ya tatu ya kujifungua kutokana na kutotoka kwa kondo la nyuma.
Kujikinga
Kujikinga dhidi ya kupata tatizo la syndrome ya Asherman ni changamoto kwa sababu mbalimbali ikiwa pamoja na matatizo mengine ambayo hayazuiliki.
Hata hivyo kinga pekee ya tatizo la syndrome ya Asherman ni kuepuka kupata mimba zisizotarajiwa kwa kutumia njia za uzazi wa mpango. Ukiepuka kupata mimba utajiondoa kwenye kihatarishi cha kutoa mimba na kisha kukwanguliwa ndani ya kizazi.
Kwa wanawake ambao ni lazima wapate matibabu ya kukwanguliwa kizazi, daktari anaweza kuweka kifaa maalumu cha kuzuia kuta za uzazi kushikamana kwa makovu yanayotengenezwa baada ya kukwanguliwa kizazi. Kifaa hiki kitahitajika kuvaliwa kwa miedhi kadha akisha kutolewa
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023 19:54:12
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1. Queckbörner S, et al. Cellular therapies for the endometrium: An update. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/30815850/.Imechukuliwa 3.03.2021
2. Guo EJ, et al. Reproductive outcomes after surgical treatment of asherman syndrome: A systematic review. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/30713131/.Imechukuliwa 3.03.2021
3. Ludwin A, et al. Ultrasound-guided repeat intrauterine balloon dilatation for prevention of adhesions. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/30677188/. Imechukuliwa 3.03.2021
4. Chikazawa K, et al. Detection of Asherman's syndrome after conservative management of placenta accreta:. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/30454053/.Imechukuliwa 3.03.2021
5. Al-Inany H. Intrauterine adhesions. An update. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/11703193/. Imechukuliwa 3.03.2021
6. Tchente NC, et al. [Asherman's syndrome : management after curettage following a postnatal placental retention and literature review]. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/30335256/.Imechukuliwa 3.03.2021
7. ASIMAKOPULOS N. TRAUMATIC INTRAUTERINE ADHESIONS. (THE FRITSCH-ASHERMAN SYNDROME). https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/14322441/.Imechukuliwa 3.03.2021
8. Young BK. A multidisciplinary approach to pregnancy loss: the pregnancy loss prevention center. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/29858908/.Imechukuliwa 3.03.2021
9. Capmas P, et al. Are synechiae a complication of laparotomic myomectomy?. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/29454580/ .Imechukuliwa 3.03.2021
10. Dreisler E,et al. Asherman's syndrome: current perspectives on diagnosis and management. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/30936754/ Imechukuliwa 3.03.2021
11. Azizi R, et al. Stem cell therapy in Asherman syndrome and thin endometrium: Stem cell- based therapy. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/29571018/.Imechukuliwa 3.03.2021
12. Zheng F, et al. Meta-analysis of the use of amniotic membrane to prevent recurrence of intrauterine adhesion after hysteroscopic adhesiolysis. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/30073656/. Imechukuliwa 3.03.2021