top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Adolf S, M.D

12 Aprili 2020 18:00:27

Usaha sehemu za siri
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Usaha sehemu za siri

Usaha ni majimaji mazito yenye rangi ya njano au ukijani yanayotokea sehemu ambayo tishu zimeathirika na maambukizi ambayo yanaweza kuwa ya bakteria, fangasi n.k. Usaha hutokana na seli nyeupe za damu zilizokufa Pamoja na serumu. Usaha hutokea pale ambapo kinga asilia ya mwili inapoitikia mapambano dhidi ya bakteria au fangasi wanaoshambulia sehemu ya mwili.


Kutokwa na usaha sehemu za siri huweza kutokea kutokana na maambukizi ya bakteria kwenye uke au fangazi mfano vaginosis au maambukizi kwenye njia ya mkojo kwa mwanaume mfano prostaitizi.


Vihatarishi


 • Maambukizi kwenye njia ya mkojo mfano UTI na payelonephraitizi ambayo hupelekea usaha kwenye figo.

 • Magonjwa ya zinaa mfano klamidia, kisonono, kaswende na trikomoniasisi

 • Upungufu wa kinga mwilini

 • Maambukizi kwenye tezi dume

 • Maambukizi sugu kwenye kibofu cha mkojo

 • Mzio au uvimbe sehemu yeyote ya kibofu cha mkojo

 • Maambukizi kutokana na mawe kwenye kibofu cha mkojo au kwenye figo

 • Saratani kwenye shingo ya kizazi, kwenye mfuko wa uzazi au kwenye ovari


Dalili


 • Maumivu makali ya kuchoma wakati wa kukojoa

 • Maumivu chini ya kitovu

 • Homa

 • Kutapika

 • Maumivu wakati wa tendo la ndoa (kujamiiana) hasa usaha utokanao na maambukizi kwenye seviksi (servisaitizi)

 • Kuvimba kwa korodani moja hasa kwa waathirika wa kisonono

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

19 Julai 2023 20:03:53

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1.Definition of pus discharge at https://www.verywellhealth.com/recovering-from-surgery-what-to-expect-3156826. Imechukuliwa11/4/2020

2.Healthline. Vaginal boils. https://www.healthline.com/health/womens-health/vaginal-boils. Imechukuliwa 11/4/2020
3. Patient. Vaginal discharge. https://patient.info/doctor/vaginal-discharge. Imechukuliwa 11/4/2020

4. Mayo clinic. Vaginal discharge. https://www.mayoclinic.org/symptoms/vaginal-discharge/basics/definition/sym-20050825. Imechukuliwa 11/4/2020

bottom of page