Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Sospeter B, MD
13 Desemba 2020 14:59:01
Vidonda kwenye uume
Kidonda/Vidonda kwenye uume huweza kusababishwa na sababu mbalimbali, unapopatwa na vipele kwenye uume usione kuwa upo mwenyewe, wasiliana na daktari kwani kuna tiba inapatikana. Makala hii ni madhumuni haswa kuelezea ni mambo au magonjwa gani yanasababisha vipele kwenye uume na dalili zake. Kusoma kuhusu dalili zaidi na tiba ingia kwenye kisababishi kimoja moja.
Visababishi
Visababishi huwa ni;
Kisonono
Maambukizi ya herpes
Saratani
Aleji ya dawa
Treponema pallidum
Haemophilus ducreyi
Magonjwa mengine
Kisonono
Sifa ya kipele cha kisonono ni,
Kipele kilichojitenga
Kisicho na maumivu
Kilichoinuka juu ya usawa wa ngozi
Sakafu isiyo na mwinuko
Matibabu
Matibabu huhusisha matumizi ya dawa za kutibu magonjwa ya zinaa
Maambukizi ya herpes
Sifa ya kipele cha herpes ni;
Kuambatana na mkusanyiko wa malengelenge madogo yenye maji
Matibabu
Matibabu huhusisha matumizi ya dawa za kupunguza uzalishaji wa kirusi huyu, hata hivyo tatizo linaweza kuondoka lenyewe pasipo kutumia dawa baada ya wiki kadhaa.
Kipele cha saratani
Sifa za vipele ni;
Kuwa na wekundu kwenye kichwa cha uume, shina na gozi
Kutoa unyevuunyevu kwenye kichwa cha uume, shina na gozi
Matibabu
Kipele cha aina hii matibabu yake hutegemea hatua ya ugonjwa, upasuaji au matumizi ya dawa za saratani huweza kuchaguliwa au kutumia njia zote kwa mbili pamoja.
Vipele kutokana aleji ya dawa
Sifa za vipele
Wekundu kwenye ngozi ya uume
Huweza kuambatana na malenge makubwa yenye maji
Hutokea siku chache au wiki kadhaa baada ya kuanza dawa
Huisha baada ya kuacha dawa
Huacha kovu lenye rangi nyeusi iliyokolea zaidi(nyeusi)
Dawa zinazoweza kupelekea kupata dalili hii ni;
Dawa jamii ya sulfonamides (trimethoprim/sulfamethoxazole
Dawa jamii ya tetracycline
Dawa jamii ya penicillins
Dawa jamii ya cephalosporins
Clindamycin
Zada za antifungal
Zada za antimalarials
Dapsone
Fluoroquinolones
Acetaminophen
acetylsalicylic acid
Ibuprofen
Indomethacin [Indocin]
Naproxen
Phenylbutazone
Anticonvulsants
Benzodiazepines
Barbiturates
Opiates
Matibabu
Matibabu huhusisha kutambua ni dawa gani inasababisha upate upele huu kisha kuacha kama utakavyoshauriwa na daktari wako.
Treponema pallidum
Vipele vya chancre hutokana na maambukizi ya kimelea anayesababisha kisonono kwa jina la Treponema pallidum
Vipele vya chancroid huwa na sifa zifuatazo;
Chenye maumivu
Kilichozama ndani
Kipele chenye mipaka iliyo na rangi ya njano
Sakavu chafu na iliyooza
Kuvimba kwenye ya maeneo ya kinena
Matibabu
Matibabu huhusisha matumizi ya dawa za kutibu magonjwa ya zinaa
Haemophilus ducreyi
Husababisha vipele ambavyo havina maumivu
Vihatarishi
Vihatarishi vya kupata upele sehemu za siri ni;
Kutofanya usafi maeneo ya siri
Kuugua ugonjwa wa kisukari
Kushiriki ngono bila kutumia kondomu na mwathirika wa magonjwa ya zinaa
Kuwa na wapenzi wengi
Kuwa kijana
Kuwa na maambukizi ya UKIMWI
Magonjwa mengine
Magonjwa mengine yanayoweza kupelekea kupata vipele kwenye uume ni pamoja na;
Balanitis xerotica obliterans
Penile lichen planus
Pearly penile papules
Contact dermatitis
Maambukizi ya fangasi
Psoriasis
Granuloma inguinale
Molluscum contagiosum
Scabies
Genital warts
Muulize daktari ni tatizo gani ulilonalo ili kuanza matibabu
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023 19:54:12
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1.American family of physician. Itchy and Painful Ulceration on the Penis https://www.aafp.org/afp/2006/0101/p133.html. Imechukuliwa 11.12.2020
2.Case Study: Postsexual Penile Ulcer as a Symptom of Diabetes. https://clinical.diabetesjournals.org/content/23/4/191. Imechukuliwa 11.12.2020
3.BMJ. Chronic penile ulcer as the first manifestation of HIV infection. https://casereports.bmj.com/content/2017/bcr-2017-221604. Imechukuliwa 11.12.2020
4.Penis sores: 12 causes and treatments. https://www.medicalnewstoday.com/articles/326583#pictures. Imechukuliwa 11.12.2020