top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Benjamin L, MD

22 Septemba 2025, 22:41:57

Vidonda mdomoni
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Vidonda mdomoni

Vidonda mdomoni (au kanka, aphthous ulcers) ni majeraha madogo yenye kina kifupi yanayojitokeza ndani ya kinywa kwenye mashavu, midomo ya ndani, ulimi au kwenye paa laini la kinywa. Havina maambukizi (hayambukizwi), hujitokea mara kwa mara kwa baadhi ya watu na mara nyingi hupona ndani ya siku 7–14 bila kuacha kovu.


Sifa za vidonda mdomoni

Vidonda hivi huwa na sifa zingine zifuatazo;

  • Haviambukizwi kama vilivyo vidonda vya homa baridi

  • Havitokei nje ya midomo, wala kwenye kona za midomo kama vilivyo vidonda vingine

  • Huwa vidogo, vyenye umbo la mduara au mviringo.

  • Kati yake huwa na rangi nyeupe au ya manjano, kingo ni nyekundu.

  • Huenda vikawa kimoja au vingi kwa wakati mmoja.

  • Vidonda vidogo hupona ndani ya wiki mbili bila kovu, vikubwa huchukua muda zaidi na huweza kuacha kovu.

  • Kabla havijatokea, mtu anaweza kuhisi kuungua au kuchomachoma kwenye sehemu hiyo.


Dalili

Vidonda huwa na umbo la mduara na rangi nyeupe au njano katikati ya kidonda, kingo za kidonda huwa na rangi nyekundu. Vidonda hivi hufanyika ndani ya midomo, kwenye mashavu, fizi, au kwenye paa laini la kinywa.


Baadhi ya wagonjwa huwa na dalili za kuungua au kuchomachoma kabla ya kidonda kutokea

Vidonda vinaweza kuwa vidogo au vikubwa, vidonda vidogo hutokea sana na hupona ndani ya wiki mbili pasipo kuleta makovu wakati vidonda vikubwa huchelewa kupotea na huweza leta makovu ndani ya mdomo.


Visababishi


Visababishi vya vidonda mdomoni badi havifahamiki kimaanani, hata hivyo tafiti zimeonyesha kuwa kuna miunganiko ya mambo yanayopelekea kutokea kwa vidonda hivi kwa mtu.

Mambo yanayoweza kuamsha vidonda mdomoni ni pamoja na;

  • Mabadiliko ya homoni wakati wa hedhi kwa wanawake

  • Maambukizi ya H.pyrol anayesababisha vidonda vya tumbo

  • Msongo wa mawazo

  • Mzio na chakula au bakteria ndani ya kinywa mfano chocolate, kahawa, matunda forosadi, mayai, karanga, maziwa mtindi na vyakula vyenye viungo kwa wingi au pilipili

  • Kula chakula kinachokosa vitamin B12, madini ya zinc foleti na madini chuma

  • Majeraha kidogo kinywani kutokana na kupiga mswaki, kujing’ata, kutumia grili ya meno

  • Matumizi ya dawa na vimiminika vya kusafisha meno vyenye madini ya sodium sulfate

  • Magonjwa aina Fulani ya mfumo wa kinga kama ugonjwa wa seliak, inflamatori baweli, bahcet, autoimmune, UKIMWI.


Vihatarishi

Kila mtu anaweza kupata vidonda mdomoni uwe na umri mkubwa au mdogo endapo, hata hivyo vidonda hivi hutokea sana kwa wanawake.


Watu wenye vidonda vinavyojirudia rudia mara nyingi huwa na historia kwenye familia ya vidonda hivi kwa sababu ya kurithi vinasaba au kuishi Mazingira au mtindo wa maisha unaochochea (msongo, vyakula vyenye mzio). n.k



Kinga

Kula mlo kamili

Kula vyakula kutoka kwenye makundi matano ya chakula ili kupata virutubisho vyote na kujikinga kupata vidonda hivi


Safisha kinywa vema kila siku

Safisha kinywa kila unapomaliza kula chakula na kusukutua mdomo mara moja kwa siku. Hakikisha kinywa chako hakina mabaki ya chakula ambayo yanaweza kuamsha vidonda. Tumia mswaki laini ili kuepuka kujeruhi kinywa chako wakati wa kupiga mswaki. Mswaki ulioharibika haufai kwa matumizi, usitumie nguvu kubwa kusafisha kinywa ili kuepuka majeraha.


Linda kinywa chako

Kama unatumia vifaa tiba mdomoni hakikisha kama kuna ncha zilizochomoza zimefunikwa ili kuepusha kupata majeraja.


Chunga kinachoingia mdomoni mwako

Jaribu kujizuia kula vyakula vinavyokereketa kinywa chako. Vyakula hivi ni kama vile karanga, chipsi, viungo aina Fulani, vyakula vyenye tindikali, kama nanasi, zabibu, forosadi, machungwa na ndimu. Usitumie chakula ambacho kina kuletea mzio.


Punguza msongo wa mawazo

Endapo vidonda vyako vinatokana na msongo wa mawazo, tumia mbinu za kupunguza msongo huomfano kwa kuwa na kipindi cha kujitafakari kwa meditation.


Wakati gani uonane na daktari?

Ongea na daktari wako endapo unapata vidonda hivi mara kwa mara na vyenye maumivu makali na dalili zilizoorodheshwa hapa chini;

  • Vidonda vinavyokua kuelekea kwenye midomo

  • Endapo unapaya maumivu makali ya kinywa usiyoweza kuvumilia

  • Kushindwa kula au kunywa

  • Homa kali inayoambatana na vidonda

  • Vidonda vikubwa mdomoni

  • Vidonda vinavyojirudia rudia, endapo kidonda kipya kinatokea kabla ya cha zamani kutoweka au kutokea kwa mlipuko wa mara kwa mara

  • Vidonda vinavyodumu zaidi ya wiki mbili


Matibabu

Vidonda vya apthous huwa havina tiba. Matibabu yaliyopo hulenga;

  • Kupunguza dalili unazopata za kuhisi maumivu makali

  • Kukuwezesha uweze kula chakula na kusafisha kinywa pasipo kupata maumivu

  • Kupunguza uvimbe kwenye kidonda ili kufanya kidonda kipone haraka


Maswali yaliyoulizwa mara kwa mara

1. Je, vidonda mdomoni vinaambukizwa kwa kubusu au kushiriki vyombo vya kula?

Hapana. Vidonda vya apthous havihusiani na virusi kama vya homa baridi (herpes). Hivyo havipitii kwa mguso, busu, au kutumia kikombe/visu vya mtu mwingine.

2. Vidonda vya homa baridi (herpes simplex) vinatofautianaje na aphthous ulcers?

Vidonda vya herpes hutokea nje ya midomo (kona za mdomo au juu ya midomo) na huambukiza. Aphthous ulcers hutokea ndani ya kinywa pekee, havihusiani na virusi na havipitii kwa mtu mwingine.

3. Kwa nini vidonda vinajirudia mara kwa mara kwa baadhi ya watu?

Mara nyingi husababishwa na mchanganyiko wa kurithi (vinasaba), mfumo wa kinga wenye ukinzani, pamoja na vihatarishi vya mazingira kama msongo, lishe duni au mzio wa vyakula fulani.

4. Je, vidonda mdomoni vina uhusiano wowote na saratani ya mdomo?

Hapana moja kwa moja. Aphthous ulcers siyo saratani. Hata hivyo, ikiwa kidonda hakiponi ndani ya wiki mbili au kinaonekana kinasambaa bila sababu, ni muhimu kupimwa kubaini kama kuna tatizo jingine, ikiwemo saratani.

5. Je, watoto wanaweza kupata vidonda mdomoni?

Ndiyo. Watoto pia hupata, hasa baada ya kujing’ata au kupata maambukizi madogo. Wengine hupata kutokana na mzio wa vyakula. Kwa watoto wadogo, vidonda vikubwa vinaweza kusababisha kukosa kula vizuri.

6. Je, kupungukiwa na vitamin pekee kunatosha kusababisha vidonda?

Mara nyingi si sababu pekee, lakini upungufu wa vitamin B12, folate, zinki au chuma unaweza kuongeza uwezekano wa vidonda kurudia. Ndio maana mlo kamili ni kinga muhimu.

7. Vidonda vikubwa au vingi vinapojitokeza mara moja, inamaanisha nini?

Hii inaweza kuashiria tatizo la kinga ya mwili (mfano Behçet’s disease, HIV, au inflammatory bowel disease). Hali hizi huhitaji uchunguzi na ufuatiliaji wa daktari.

8. Kuna tiba za asili zinazosaidia?

Baadhi ya watu hupata nafuu kwa kusukutua maji ya chumvi kidogo, kutumia asali au aloe vera kwenye kidonda. Hata hivyo, ushahidi wa kisayansi ni mdogo, na si mbadala wa matibabu rasmi iwapo vidonda ni sugu au vikubwa.

9. Je, vidonda vinaweza kuzuiwa kwa kutumia dawa kabla havijatokea?

Hakuna dawa ya moja kwa moja ya kuzuia. Hata hivyo, kwa watu wenye vidonda vinavyorudia mara nyingi, daktari anaweza kuandikia mouthwash maalum, corticosteroid topical, au dawa zinazodhibiti kinga (immunomodulators) katika hali maalum.

10. Ni lini vidonda huchukuliwa kuwa hatari?

Endapo vinadumu zaidi ya wiki mbili, vinaambatana na homa, kuvimba tezi shingoni, kupungua uzito bila sababu, au kuenea haraka bila kupona. Hapo lazima kufanyiwa uchunguzi wa kitaalamu.

11. Nimekuwa nikisumbuliwa na vidonda mdomoni vinavyorudia mara kwa mara, vikichochewa na vyakula fulani kama matunda yenye tindikali (nanasi, chungwa, limao), pilipili, chocolate na mboga fulani. Nimejaribu dawa za antihistamine kama Citrizine bila mafanikio. Nifanye nini?

Jibu:Vidonda vya apthous havihusiani moja kwa moja na mziow wa kawaida unaoitikia dawa jamii ya antihistamines kama Citrizine, ndio maana huenda havijakusaidia. Kwa hali ya vidonda vinavyorudia:

  1. Kuzuia vichochezi

    • Kuepuka vyakula ambavyo umethibitisha vinaamsha vidonda (mfano matunda yenye tindikali, pilipili, chocolate).

    • Kuandika orodha ya vyakula ili kufuatilia vyakula vinavyosababisha mlipuko wa vidonda.

  2. Matibabu ya kupunguza maumivu na kuharakisha kupona

    • Mouthwash zenye dawa: chlorhexidine gluconate au tetracycline mouth rinse (kwa agizo la daktari).

    • Topical kortikosteroidi (mfano triamcinolone dental paste au hydrocortisone pellets) kuwekwa moja kwa moja juu ya kidonda. Hizi hupunguza uvimbe na maumivu.

    • Dawa za kupaka zenye benzocaine au lidocaine kusaidia ganzi na kupunguza maumivu wakati wa kula.

  3. Tiba ya ndani ya mwili kwa vidonda sugu au vikubwa

    • Wakati mwingine daktari anaweza kuagiza kortikosteroid za kumeza kwa kipindi kifupi (mfano prednisolone) au dawa zinazodhibiti kinga ya mwili kwa visa vigumu sana.

    • Uchunguzi wa damu unaweza kufanyika kuona kama una upungufu wa vitamini B12, folate, chuma au zinki na ukihitajika kupewa virutubisho.

  4. Mbinu za nyumbani

    • Kusukutua maji yenye chumvi kidogo au baking soda mara kadhaa kwa siku.

    • Kuepuka msongo wa mawazo, ambao mara nyingi huongeza mlipuko.


Kumbuka:

Kwa kuwa vidonda vyako vinarudi mara kwa mara kwa muda mrefu, ni busara kumwona daktari wa meno au daktari bingwa wa magonjwa ya kinywa na meno. Wataweza kuthibitisha kuwa siyo tatizo jingine linalofanana, na kukupa dawa maalum za kuzuia kurudi kwa vidonda.





ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeandikwa:

3 Juni 2020, 08:51:19

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

American Academy of Oral Medicine. Canker sores [Internet]. American Academy of Oral Medicine; c2020 [cited 2020 Jun 3]. Available from: http://www.aaom.com/index.php?option=com_content&view=article&id=82:canker-sores&catid=22:patient-condition-information&Itemid=120

American Dental Association. Canker sores [Internet]. Chicago (IL): American Dental Association; c2020 [cited 2020 Jun 3]. Available from: https://www.mouthhealthy.org/en/az-topics/c/canker-sores

American Academy of Family Physicians. Canker sores [Internet]. Leawood (KS): FamilyDoctor.org; c2020 [cited 2020 Jun 3]. Available from: http://familydoctor.org/familydoctor/en/diseases-conditions/canker-sores.html

Merck Manual Consumer Version. Recurrent aphthous stomatitis [Internet]. Kenilworth (NJ): Merck & Co., Inc.; c2020 [cited 2020 Jun 3]. Available from: http://www.merckmanuals.com/home/mouth_and_dental_disorders/symptoms_of_oral_and_dental_disorders/recurrent_aphthous_stomatitis.html

American Academy of Oral and Maxillofacial Pathology. Recurrent aphthous ulcerations [Internet]. American Academy of Oral and Maxillofacial Pathology; c2020 [cited 2020 Jun 3]. Available from: http://www.aaomp.org/public/aphthous-ulcerations.php

Merck Manual Consumer Version. Mouth sores and inflammation [Internet]. Kenilworth (NJ): Merck & Co., Inc.; c2020 [cited 2020 Jun 3]. Available from: http://www.merckmanuals.com/home/mouth_and_dental_disorders/symptoms_of_oral_and_dental_disorders/mouth_sores_and_inflammation.html

Mayo Clinic. Canker sore (aphthous ulcer) [Internet]. Rochester (MN): Mayo Foundation for Medical Education and Research; 2023 [cited 2025 Sep 23]. Available from: https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/canker-sore

Porter SR, Scully C, Pedersen A. Recurrent aphthous stomatitis. Crit Rev Oral Biol Med. 1998;9(3):306–321. doi:10.1177/10454411980090030301

Preeti L, Magesh KT, Rajkumar K, Karthik R. Recurrent aphthous stomatitis. J Oral Maxillofac Pathol. 2011;15(3):252–256. doi:10.4103/0973-029X.86669

Scully C, Porter S. Oral mucosal disease: recurrent aphthous stomatitis. Br J Oral Maxillofac Surg. 2008;46(3):198–206. doi:10.1016/j.bjoms.2007.07.201

bottom of page