top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Benjamin L, MD

13 Septemba 2025, 09:59:46

Vipele kwenye uume: Sababu, Vipimo na Matibabu
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Vipele kwenye uume: Sababu, Vipimo na Matibabu

Vipele kwenye uume ni hali inayopatikana mara nyingi kwa wanaume. Ingawa baadhi ya vipele vinaweza kusababishwa na magonjwa ya zinaa, mara nyingi huchangiwa na sababu zisizo hatarishi kama vile mabadiliko ya ngozi au maambukizi madogo. Kwa kuwa uume ni kiungo muhimu kwa afya ya uzazi na maisha ya kijinsia, mabadiliko yoyote katika muonekano wake huweza kuleta hofu au wasiwasi. Hata hivyo, si kila kipele au uvimbe ni ishara ya tatizo kubwa.


Makala hii inalenga kutoa mwongozo wa jumla kuhusu visababishi vya kawaida na visivyo vya kawaida vya vipele kwenye uume. Ili kupata utambuzi sahihi na matibabu yanayofaa, ni muhimu kumwona daktari au mtaalamu wa afya kila unapogundua mabadiliko yasiyo ya kawaida.


Dalili

Dalili zinazoweza kuambatana na vipele ni pamoja na;

  • Kuwasha au maumivu

  • Usaha au majimaji kutoka kwenye vidonda

  • Harufu isiyo ya kawaida

  • Uvimbe wa tezi za kinena

  • Homa, uchovu, au maumivu ya misuli


Visababishi

Vipele na uvimbe kwenye uume vinaweza kutokea kutokana na sababu nyingi, kutoka zile zisizo na madhara makubwa hadi zile zinazohitaji matibabu ya haraka. Mara nyingi hutokana na muwasho wa ngozi, maambukizi ya fangasi au bakteria, magonjwa ya zinaa, au hata msuguano unaosababishwa na nguo au shughuli za kimwili. Wakati mwingine, yanaweza pia kuashiria hali nadra kama ugonjwa wa ngozi sugu au saratani ya uume. Ili kuelewa vyema chanzo, ni muhimu kutambua dalili zinazofuatana na vipele na kumwona daktari kwa uchunguzi sahihi. Visababishi vikuu vya vipele na uvimbe kwenye uume ni;


Mole

Ni vijivimbe visivyo vya hatari vinavyotokana na ngozi kuzalisha pigmenti nyingi za rangi nyeusi kwenye eneo digo. Uvimbe wa aina hii unaweza kuonekana sehemu yoyote ule ya mwili ikiwa pamoja na kwenye uume. Kwa wastani watu huwa na takribani mole 10 hadi 40 sehemu mbalimbali za mwili


Picha chini inaonyesha aina za mole;



Wakati gani wa kuonana na daktari?

Mara nyingi uvimbe wa mole huwa hauna hatari, hata hivyo endapo unabadilika umbile, rangi, kuwa na umbile lisiloeleweka na kubadilika muundo, wasiliana na daktari haraka kwa uchunguzi ili kuchunguzwa kama ni saratani au la.


Maoteo ya vinyweleo ndani ya ngozi

Hutokea kama kipande cha nywele iliyokatwa kimezuliwa kutoka nje ya ngozi kutokana na kuziba kwa vishimo vya vinyweleo na hivyo kutengeneza uvimbe chini ya ngozi. Uvimbe huu unaweza kuleta dalili ya kuwasha au maumivu na wakati mwingine kutengeneza usaha au majimaji. Mara nyingi hutokea mara baada ya kunyoa nyweke za maeneo hayo hivi karibuni.


Ili kuondoa vipele hivi, vinyweleo vilivyootea chini ya ngozi vinapaswa kunasuliwa au kutolewa na mtaalamu wa afya.


Maambukizi ya bakteria au fangasi kwenye kinyweleo kilichojificha chini ya ngozi hupelekea ugonjwa wa ngozi wenye jina la folikilaitiz.


Angalia picha inayofuata kwa maelezo zaidi.


Kifuko maji

Ni uvimne usio wa hatari wenye ukuta wa epithelia na maji ndani yake pasipo kuwa na kitundu mtoleo cha maji hayo. Huweza kutokea sehemu yoyote ya mwili ikiwa pamoja na uume.

Kifuko maji mara nyingi hufanana na rangi ya ngozi na hakina maumivu na kutobadilia mwonekano licha ya kuweza kuwa kubwa.


Fodisi spoti

Fodisi spoti ni kiuvimbe kidogo chenye rangi nyeupe kinachoweza kuonekana kwenye ncha ya ulimu au ndani yam domo pamoja na meneo ya siri kama kwenye uume.


Viuvimbe hivi ni aina ya tezi ndogo za sebaceous zisizofanana na tezi za kawaida na huwa haziambatani maeneo yenye vinyweleo. Huhitaji matibabu kwenye aina hii ya vipele.


Angalia picha chini kwa maelezo zaidi.


Pearly penile papule


Ni vipele laini vinavyovyozunguka kwenye shingo ya uume na huzunguka uume wote kwenye mstari mmoja wa duara au mistari miwili. Vipele hivi huchukuliwa kuwa vya kawaida na havileti dalili totote wala kuhitaji matibabu.



Angiokeratoma


Ni vipele vidogo vinavyotokea katika mkusanyiko kwenye maeneo ambapo mishipa ya damu upo karibu na usawa wa ngozi au karibu na mshipa wa damu uliotanuka.


Angiokeratoma huweza kuwa na umbile lisiloeleweka na kuogezeka ukubwa. Huweza kumaanisha kuwa na ugonjwa wa mishipa ya damu kama vile shinikizo la juu la damu au varikosili. Unapaswa kuwasiliana na daktari kama ukipatwa na tatizo kama hili.


Ugonjwa wa Pironiaz


Ugonjwa wa Pironiaz hutokana na tishu za makovu za faibrazi kutengenezwa kwenye uume na kufanya ujikunje na kuwa na mwonekano usioeleweka au kutengeneza uvimbe.Uume unaweza kupata maumivu wakati wa kusimama na kupelekea pia madhaifu ya kusimamisha uume.


Ugonjwa Pironiaz huongezeka muda unavyokwenda, unapaswa kuwasiliana na daktari mara moja upatwapo na dalili hii.


Limfosil

Limfosil ni uvimbe mgumu unaoweza kuonekana kwenye uume baada ya kufanya ngono au punyeto. Hutokea kufuatiwa kuziba kwa muda kwa moja ya mshipa limfu. Mara nyingi limfosili huisha haraka bila matibabu yoyote.


Molluscum contagiosum

Ni ugonjwa wa ngozi unaosababishwa na uambukizo wa gozi na virusi. Huzalisha vipele vidogo, laini, vinavyong’aa na kujazwa na nta ndani. Huweza kuonekana sehemu yoyote ya mwili na hutokea sana kwa watoto


Herpes ya sehemu za siri

Vipele au uvimbe wa herpes husabaishwa na uambukizo wa sehemu za siri na kirusi herpes simplex 1 au 2 (HSV-1 au HSV-2).


Sifa zingine

Vipele hivi huwa vimejazwa na maji na huwa na maumivu au kuwasha. Vipele hivi huhitaji matibabu ya dawa za virusi na za maumivu ili kudhibiti dalili.


Sunzua

Sunzua au warts za shemu za siri husababishwa na uambukizo wa kirusi human papilloma (HPV).


Sifa zingine

  • Huzalisha kipele au uvimbe usio na maumivu maeneo ya kuzunguka uume au uke na njia ya haja kubwa.

  • Huweza kuwa laini, rangi ya kijivu nyeupe, pinki- nyeupe au kahawia na huweza kuwa mmoja au kwenye kundi na wakati mwingine huchanua na kuwa na umbile kama la uyoga uliosambaa.


Dawa mbalimbali zinaweza kutolewa kwa matibabu ya uvimbe au vipele vya namna hii na mtaalamu wa afya na baadhi ya nyakati mgonjwa hufanyiwa upasuaji kama tiba.


Kaswende

Vipele vya kaswende husababishwa na uambukizo wa bakteria Treponema pallidum anayeenezwa kwa kufanya ngono.


Sifa zake

Hutengeneza kidonda kigumu cha duara na kisicho na maumivu. Utahitaji matibabu mara moja kama utapatwa na dalili hii.


Tazama picha kwa maelezo zaidi

Sakabi


Hutokana na vimelea wadogo wanaochimba na kuingia chini ya ngozi hivyo kuonekana kama upele au uvimbe mdogo. Vimelea vya skabi huweza kutaga mayai chini ya ngozi na hivyo kupelekea muwasho mkali haswa wakati wa usiku.


Saratani

Ni kwa ndra sana upele kwenye ngozi ya uume unaweza kuashiria saratani.


Sifa zake

Upele wa saratani huweza kukua haraka, huwa na umbile lislilo na mipaka ya kueleweka na huweza kuwa na maumivu au la.


Wasiliana na daktari kwa uchunguzi kama unapata vipele vyenye sifa kama zilizotajwa hapo juu vilivyodumu kwa muda wa wiki nnje au zaidi kwa uchunguzi.


Chunusi

Ni vipele vidogo vinavyoweza kuwa na kichwa chenye mwonekao mweupe au mweusi vinavyosababishwa na kuziba kwa vitundu vya ngozi kutokana na mafuta, maambukizi ya bakteria, vinyweleo au uchafu kwenye ngozi.


Sifa zake

Huweza kuacha alama nyeusi au kovu kweney ngozi baada ya kupona na huchochewa sana na mabadiliko ya homoni au msongo wa mawazo.


Jedwali 1: muunganisho wa visababishi

Kisababishi

Maelezo

Dalili Kuu

Dalili za vipekee

Mole

Vijivimbe visivyo hatari vinavyotokana na ngozi kutoa pigmenti nyingi (melanin).

Uvimbe mdogo wenye rangi ya kahawia au nyeusi, laini au kidogo kigumu.

Kubadilika rangi au umbo, kingo zisizo sawa – ishara ya hatari ya saratani ya ngozi.

Maoteo ya vinyweleo

Nywele kuota chini ya ngozi kutokana na kuziba kwa vishimo vya nywele.

Uvimbe mdogo, wekundu au wenye maumivu.

Wakati mwingine huzalisha usaha au majimaji.

Folikulaitis

Maambukizi ya bakteria au fangasi kwenye vinyweleo.

Vipele vidogo vyenye wekundu au usaha.

Kuwasha au maumivu kwenye eneo lenye vinyweleo.

Kifuko cha maji (sisti)

Uvimbe wenye ukuta mwembamba na majimaji ndani.

Uvimbe laini bila maumivu.

Mara chache hukua lakini hubaki bila kubadilika.

Fordyce spots

Tezi ndogo za mafuta (sebaceous) zisizo na madhara.

Vipele vidogo vyeupe au vya njano kwenye shingo ya uume au ndani ya mdomo.

Havileti maumivu wala kuwasha, ni vya kawaida.

Pearly penile papules

Vipele vidogo vinavyozunguka kichwa cha uume.

Mistari ya vipele laini na vidogo kuzunguka shingo ya uume.

Havina maumivu, usaha, au dalili nyingine.

Angiokeratoma

Vipele vinavyotokana na mishipa ya damu iliyo karibu na ngozi.

Vipele vyekundu au zenye rangi ya damu iliyokauka.

Huongezeka ukubwa au kubadilika umbo, wakati mwingine kuhusiana na shinikizo la damu au varikosili.

Ugonjwa wa Peyronie

Makovu ya nyuzi (fibrosis) kwenye uume.

Uvimbe au mistari chini ya ngozi ya uume.

Uume kujikunja au maumivu wakati wa kusimama.

Limfosil

Kuziba kwa muda kwa mshipa wa limfu baada ya punyeto au ngono.

Uvimbe mgumu, bila maumivu.

Huisha haraka bila tiba maalumu.

Molluscum contagiosum

Virusi vya ngozi vinavyozalisha vipele vidogo.

Vipele vidogo, laini na kung’aa.

Huwa na kitu cheupe au nta ndani, mara nyingi huenea kwa kugusana.

Herpes ya sehemu za siri

Virusi vya HSV-1 au HSV-2.

Vipele vidogo vilivyojaa majimaji.

Maumivu au kuwasha, vidonda baada ya kupasuka.

Sunzua (warts za sehemu za siri)

Virusi vya HPV.

Vipele vidogo visivyo na maumivu.

Umbile kama uyoga uliosambaa au rangi ya kijivu/pinki.

Kaswende (syphilis)

Maambukizi ya bakteria Treponema pallidum.

Kidonda kigumu na duara.

Hakina maumivu, kinaweza kupona chenyewe lakini kuendelea ndani ya mwili.

Sakabi (scabies)

Vimelea wanaoingia chini ya ngozi.

Muwasho mkali, hasa usiku.

Mistari midogo ya ngozi yenye vipele vidogo.

Saratani ya uume

Ukuaji wa seli zisizo za kawaida kwenye ngozi ya uume.

Upele au uvimbe usio na mpangilio.

Kuongezeka ukubwa haraka, kingo zisizo sawa, unaweza kutoa damu au maumivu.

Kumbuka: Dalili zikipatikana kwa muda mrefu, zikiambatana na maumivu, usaha, au mabadiliko yasiyoelezeka, ni muhimu kumwona daktari mapema kwa uchunguzi na matibabu sahihi.

Vipimo vya Uchunguzi

Jedwali 2: Aina ya vipimo na lengo

Lengo

Uchunguzi wa mwili na historia ya mgonjwa

Kueleza mwonekano, eneo, dalili zinazohusiana

Swab ya kidonda kwa culture/PCR

Kutambua HSV, HPV, Treponema pallidum au bakteria wengine

Serolojia (VDRL/RPR, HIV test)

Kuchunguza kaswende na hali ya kinga

Biopsy ya ngozi/uvimbe

Kwa uvimbe usioeleweka au kushukiwa saratani

Dermatoscopy

Kwa mole, angiokeratoma na vidonda vya damu

Urinalysis na urethral swab

Kama kuna maumivu wakati wa kukojoa au usaha

Ultrasound ya uume

Kwa Peyronie’s au uvimbe unaoshukiwa cyst


Matibabu kulingana na kisababishi

Jedwali 3: Matibabu kulingana na kisababishi

Kisababishi

Vipimo vinavyopendekezwa

Matibabu / Ushauri

Maoteo ya vinyweleo / Folikulitisi

Uchunguzi wa ngozi, culture kama kuna usaha

Osha kwa sabuni nyepesi, antibiotic topical (mupirocin), toa nywele iliyoingia kwa uangalifu

Herpes simplex

Swab PCR/culture

Dawa za kuzuia virusi (acyclovir/valacyclovir), analgesics

Molluscum contagiosum

Uchunguzi wa macho

Curettage, cryotherapy au cream ya imiquimod ikiwa kuna kero

Sunzua (warts za HPV)

Uchunguzi wa macho, biopsy ikiwa haieleweki

Podophyllotoxin, cryotherapy, electrocautery

Kaswende

VDRL/RPR

Penicillin G benzathine (kulingana na hatua ya ugonjwa)

Angiokeratoma

Dermatoscopy/biopsy

Hakuna tiba kama haina dalili; laser/excision kama inavuja damu

Ugonjwa wa Peyronie

Ultrasound, historia

NSAIDs kwa maumivu, dawa (mf. pentoxifylline), upasuaji ikiwa kali

Sisti

Uchunguzi wa macho, ultrasound

Ufuatiliaji au excision kama kubwa/kero

Saratani ya uume

Biopsi

Upasuaji wa kuondoa uvimbe au uume

Chunusi

Hakuna vipimo maalum

Safisha mara kwa mara, benzoyl peroxide ya kupaka au clindamycin

Ushauri wa Jumla: Safisha uume kwa maji safi na sabuni isiyo kali. Epuka kujikuna au kubonyeza vipele. Tumia kinga wakati wa tendo la ndoa. Usitumie dawa za kupaka bila ushauri wa daktari.

Wakati wa kumwona daktari haraka?

  • Vipele vinavyoambatana na homa, kutokwa damu, au harufu mbaya.

  • Uvimbe unaoongezeka haraka au unaosababisha maumivu makali.

  • Kidonda kinachodumu zaidi ya wiki 2–4 bila kupona.

  • Dalili za kuvimba tezi za kinena au maumivu makali wakati wa kukojoa.


Hitimisho

Vipele kwenye uume vinaweza kusababishwa na sababu nyingi kuanzia zile zisizo na madhara hadi maambukizi makali au saratani. Uchunguzi wa kitaalamu ni muhimu ili kupata tiba sahihi mapema. Kudumisha usafi, kutumia kinga na kufanyiwa vipimo mapema hupunguza madhara na huimarisha afya ya uzazi wa mwanaume.



Maswali yalitoulizwa mara kwa mara

1 Je, vipele vyote kwenye uume vinaambukiza?

Jibu: Hapana. Vipele vingi kama mole, pearly penile papules au Fordyce spots havisababishwi na vijidudu, hivyo havienzi maambukizo. Vipele vinavyotokana na virusi (mfano herpes simplex, HPV, molluscum contagiosum) au bakteria (kaswende) vinaweza kuambukiza, hasa kupitia ngono isiyo salama. Ni muhimu kutofautisha kati ya hali isiyoambukiza na maambukizi kupitia uchunguzi wa kitaalamu.

2 Nifanye nini nikiona kipele kimoja pekee kwenye uume?

3 Vipele vya virusi kama HPV au herpes vikishatibiwa vinaweza kurudi?

4 Je, matumizi ya kondomu huzuia vipele vyote vya zinaa?

5 Vipele vya uume vina uhusiano gani na magonjwa ya kinga mwilini (mfano UKIMWI)?

6 Nifanye nini ili kuzuia vipele vinavyotokana na unyoaji?

 7 Je, lishe au mtindo wa maisha una mchango kwenye afya ya ngozi ya uume?

8 Je, kila kipele kwenye uume lazima kiondolewe?

9 Nawezaje kutofautisha kati ya saratani na vipele vya kawaida?

10  Nini madhara ya kuchelewa kutafuta tiba ya vipele kwenye uume?


ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeandikwa:

26 Oktoba 2021, 12:31:00

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

American Academy of Dermatology. Moles: Who gets and types [Internet]. Rosemont (IL): AAD; [imechukuliwa 2025-09-13]. Inapatikana: https://www.aad.org/public/diseases/a-z/moles-types

American Cancer Society. Signs and symptoms of penile cancer [Internet]. Atlanta (GA): ACS; 2021 [imechukuliwa 2025-09-13]. Inapatikana: https://www.cancer.org/cancer/penile-cancer/detection-diagnosis-staging/signs-symptoms.html

American Society of Clinical Oncology. Penile cancer: Symptoms and signs [Internet]. Alexandria (VA): ASCO; 2020 [imechukuliwa 2025-09-13]. Inapatikana: https://www.cancer.net/cancer-types/penile-cancer/symptoms-and-signs

Workowski KA, Bachmann LH, Chan PA, Johnston CM, Muzny CA, Park I, et al. Sexually transmitted infections treatment guidelines, 2021. MMWR Recomm Rep. 2021;70(4):1-187.

Buechner SA. Common skin disorders of the penis. BJU Int. 2002;90(5):498-506.

Edwards SK, Bunker CB, Ziller F, van der Meijden WI; European STI Guidelines Editorial Board. 2013 European guideline for the management of balanoposthitis. J Eur Acad Dermatol Venereol. 2014;28(5):617-26.

Gross GE, Tyring SK. Sexually transmitted infections and sexually transmitted diseases. 2nd ed. Berlin: Springer; 2011.

Kumar V, Abbas AK, Aster JC. Robbins & Cotran pathologic basis of disease. 10th ed. Philadelphia: Elsevier; 2021.

bottom of page