Mwandishi: ULY-Clinic
Mhariri: Dkt. Benjamin L, MD
06 juni 2018
Kutokwa na damu nyingi kwenye hedhi
​
Ni kiasi gani cha damu ni kawaida kutoka wakati wa hedhi?
​
Tafiti zinaonyesha kuwa wastani wa damu inayotoka kwenye hedhi kwa wanawake wengi huwa kati ya mililita 5 hadi 80 kwa hedhi nzima, kupoteza hedhi zaidi ya mililita 80 kwa kipindi kimoja cha hedhi huitwa kuwa na hedhi yenye damu nyingi.
Kiasi cha mililita 80 za hedhi hufananishwa kuwa sawa na vijiko 6 vya chakula.
​
Ni nini hupelekea kupata hedhi yenye damu nyingi?
​
Kwa kawaida mzunguko wa hedhi huchukua siku 21 mpaka 35 lakini wastani wa wanawake wengi hupata mzunguko wa siku 28.
Kama unapata mzunguko wa siku 21 basi katika mwaka wenye siku 365 utapata mizunguko 17 (365/21=17) na endapo una mzunguko wa siku 35 utakuwa na vipindi 10 vya hedhi( 365/35=10) katika mwaka
Hivo endapo hedhi inatokea katika wastani wa siku 28 utakuwa na mizunguko 13 katika mwaka na ikiwa unapata vipindi vya hedhi zaidi ya vipini 17 kwa mwaka au kuwa na mzunguko wa hedhi chini ya siku chini ya 21 katika kwa mwezi, basi utakuwa kwenye tatizo linaloitwa 'Mizunguko mingi ya hedhi' au 'polimenorea' (polymenorrhea).
Endapo mwanamke anaenda hedhi chini ya vipindi 10 katika mwaka au zaidi au kuwa na mzunguko unaochukua zaidi ya siku 35 kati ya mzinguko mmoja na mwingine,hili huwa ni tatizo ambalo linaitwa 'mizunguko michache ya hedhi' au 'oligomenorea'. Polymenorea huambatana husababisha kutokwa na damu nyingi kwenye hedhi na pia husababishwa na matatizo mbalimbali kama vile msongo wa mawazo, kufanya mazoezi makali, matumizi ya dawa mbalimbali na kuelekea koma hedhi, matatizo/magonjwa kwenye mfumo wa uzazi. Soma maelezo zaidi ya visababishi kwenye kurasa ya visababishi
​
Imeboreshwa 06 Juni 2021
​
Rejea za mada hii
​
-
I S Fraser, et al. Estimating menstrual blood loss in women with normal and excessive menstrual fluid volume. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/11704173/#:. Imechukuliwa 06.07.2021
-
Andra H. James, et al. Heavy menstrual bleeding: work-up and management. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC6142441/. Imechukuliwa 06.07.2021