Achillea millefolium
Imeandikwa na:
@ULY CLINIC
26 Juni 2021, 11:40:01
Utangulizi
Achillea millefolium ni mmea ambao una asili ya Ulaya, uwezo wake wa kutibu maradhi unafahamika kwa muda mrefu sana na umekuwa ukiwasaidia askari wakati wa vita kutibu na kukata damu inayotoka kwenye majeraha mbalimbali.
Dawa hii pia huweza kutibu homa ya hey, homa ya baridi na mafua. Hata hivyo huweza kutibu matatizo ya uzazi yanayohusiana na mzunguko wa hedhi
Maelezo ya mmea Achillea millefolium
Ni mmea unaostawi mwaka mzima kutoka katika familia ya Asteracea na hukuwa kwenye ukanda wa joto katika mabara tofauti duniani ambayo ni Ulaya, Asia, na Amerika kaskazini.
Mti wa mmea huwa na shina dogo na urefu wa sentimita 60 hadi 80 ingawa baadhi ya spishi huweza kufikisha mita mbili za urefu.
Shina la mti wake huwa limefunikwa na manyoya meupe na majani yake huwa marefu yenye rangi ya kijani iliyokolea
Maua ya mmea huu huwa na rangi nyeupe, pinki au zambarau ikitegemea spishi na hubonoa kati ya mwezi wa sita hadi wa tisa
Uwezo wa Achillea millefolium katika tiba
Matumizi ndani yamwili
Achillea millefolium huwa na uwezo wa;
• Kuzuia mijongeo ya misuli laini na hivyo huweza kuzuia matatizo ya maumivu wakati wa hedhi na mfumo wa chakula.
• Husaidia mmeng'enyo wa chakula na kutibu kiungulia
• Huongeza mzunguko wa damu kwenye kizazi na ogani zingine ndani ya nyonga na hivyo kuamsha hedhi au kufanya hedhi itoke kwa muda mrefu. Haitakiwi kutumika wakati wa ujauzito.
Matumizi nje ya mwili
• Hutumika kuharakisha uponyaji na kufanya jeraha liache kutoa damu endapo dawa itagandamizwa kwenye kidonda.
• Hupunguza michomo ya kinga kwenye ngozi
• Huzuia kupata maambukizi kwenye ngozi endapo itapakwa.
• Endapo mwenye maumivu ya hedhi atakalia maji yake, hupunguza maumivu ya hedhi
Namna ya kutumia Achillea millefolium kama dawa
Matumizi ya kunywa
Kwa tatizo la kukosa hamu ya kula, matatizo ya mmeng'enyo na maumivu ya hedhi, tumia maji yaliyovunwa kwa infushen kijiko kimoja au viwili kwenye mililita 150 za maji, kila baada ya masaa 8. Au dawa iliyovunwa kwa njia ya maji mililita 1 hadi 2 kila baada ya masaa 8.
Matumizi ya nje
Tumia kijiko kimoja au viwili vya infushen ya dawa kisha changanya kwenye mililita 250 za maji kisha funga kidonda kwa kitambaa kilichochovywa kwenye maji hayo.
Changanya kwenye lita ishirini za maji lita moja ya infusheni iliyotengenezwa na gramu 100 za mmea kisha kalia kwa dakika 15 kila baada ya lisaa mara nyingi jinsi utakavyokuwa unapata nafuu
Kukata damu inayotoka puani- weka majani mabichi kwenye pua inayotoa damu
Majina mengine ya dawa ya mmea Achillea millefolium
Mmea Achillea millefolium unafahamika na watu wengine kama kama;
• Dawa asili ya kukata damu inayotoka puani
• Dawa asili ya damu puani
• Dawa asili ya maumivu ya hedhi
• Dawa asili ya kiungulia
Namna ya kuandaa aina mbalimbali za dawa kutoka kwenye mmea
​
Namna ya kuandaa infusheni ya dawa asilia
​
Infusheni huandaliwa kwa kuzamisha sehemu ya mmea unayotaka kutumia kama dawa kwenye kiasi cha maji yaliyochemka. Baada ya kuzamisha kwenye maji yaliyochemka, maji hayo huchujwa baada ya dakika 15. Dozi ya dawa inayotakiwa kuandaliwa kwa wastani huwa ni gramu 1 kwa kila mililita 10 za maji.
​
Kuna dawa nyingi asilia zimeshatengenezwa na kufungwa kwenye vifungashio vya karatasi ambapo unaweza kutumia kirahisi kama majani ya chai ya kuchovywa. Dawa kwenye fomu hiyo zitapunguza muda wa kuandaa.
​
Namna ya kuandaa dikokshen ya dawa asilia
​
Dikokshen hutumika kuvuna kiini cha dawa ambacho hakiathiriwi na joto.
​
Ili kuandaa dikokshen ya dawa, chemsha magome au mizizi ya mmea kwa muda wa dakika 15 hadi 60 (hutegemea aina ya mmea au kiini cha dawa), kisha pooza na ongeza maji ya baridi ili kutengeneza kiasi cha dawa na wingi wa kiini unachohitaji.
​
Endapo dawa inatakiwa kuchemka kwa muda mrefu, unatakiwa ongezea kiasi cha maji yaliyopotea ili dawa isiungue.
​
Dozi ya dikoksheni ni sawa na infusheni yaani gramu moja ya mmea kwa mililita 10 za maji isipokuwa endapo dawa ina uteute mwingi, gramu moja inatakiwa kuchanganywa na mililita 20 za maji.
Namna ya kuandaa mmengenyo wa dawa
Kuandaa mmeng’enyo wa dawa kwa njia hii unatakiwa weka dawa yako kwenye chombo kisha ongeza maji yenye joto linalotakiwa, mara nyingi joto linatakiwa kuwa kati ya nyuzi za sentigrade 35 hadi 40 ikitegemea aina ya dawa. Lengo kuu la kuzingatia joto ni kutoharibu kiini cha dawa ambacho kinategemea joto.
​
Namna ya kuandaa masalesheni ya dawa
Ili kuandaa masalesheni ya dawa, saga au katakata dawa kwenye vipande vidodo vidogo sana kisha weka kwenye jaa ya kioo yenye kimiminika cha kufyonza dawa. Funika mchanganyiko na acha kwa muda wa siku tatu au zaidi kwenye joto la ndani ya nyumba.Baada ya kutimia kwa siku tatu, tikisa kwa nguvu mara nyingi ili dawa iingie kwenye kimiminika. Baada ya hapo chuja dawa na kamua unga au vipande ili dawa yote itoke. Baada ya hapo unaweza kuchuja dawa kwa ajili ya matumizi au kuifanyia dekatensheni ili kupata kiini safi cha dawa.
​
Namna ya kuandaa pakolesheni ya dawa
Hii ni njia maarufu ya kuandaa tinkcha ya dawa au kufyonza dawa kutoka kwenye kimiminika. Njia hii inahitaji chombo maalumu chenye jina la pakoleta na unatakiwa kuwa mtaalamu zaidi kuandaa dawa kwa njia hii. Soma zaidi maelezo kwa kutumia linki chini ya tovuti hii.
Namna ya kuandaa dawa ya kufyonza kwa kimiminika
​
Njia hii huandaa dawa kutoka kwenye kimiminika chenye dawa au tishu za mnyama kwa kufyonzwa dawa hiyo kwa kutumia kimiminika kingine haswa pombe aina ya ehthanol au maji.
Kiasi cha pombe na maji yanayowekwa hutegemea aina ya dawa. Njia hii inahitaji uwe mtaalamu wa kuandaa dawa, unaweza kujifunza zaidi namna ya kuandaa dawa kwa njia hii kupitia linki chini ya tovuti hii au tumia dawa ambazo tayari zimekwisha andaliwa.
​
Namna ya kuandaa tinkcha ya dawa
Tinkcha ya dawa huandaliwa kwa kufanya masalesheni au pakolesheni ya dawa kwa kutumia kimiminika cha pombe tu. Njia hii ni nzuri ya kuvuna kiwango cha kiini unachotaka kutoka kwenye mimea au mnyama. Soma zaidi kuhusu njia hii kupitia rejea chini ya Makala hii.
​​
KUMBUKA:
Kama kuna haja ya kuchemsha dawa, hakikisha unatumia chomo kilichotengenezwa na udongo au sufuria za stainless steel na usifunike wakati wa kuchemsha ili kutoa sumu na kutobadili kiini cha dawa.
Usitumie dawa zaidi moja na kutibu tatizo moja au mawili tofauti ili kuepuka madhara na mwingiliano
​
Endapo unatumia dawa za hospitali, wasilina na daktari wako kukushauri ili kuepuka mwingiliano wa dawa na madhara yanayoweza kutokea.
ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute msaada kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba kupitia kitufe cha 'Pata tiba' au 'Mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
27 Juni 2021, 12:45:43
Rejea za mada hii;
1. Infusion methods. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/infusion/#. Imechukuliwa 27.06.2021
2. Decoction extraction. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/decoction/. Imechukuliwa 27.06.2021
3. Extraction methods digestion. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/digestion/. Imechukuliwa 27.06.2021
4. Fluid extract. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extracts/fluid-extract/. Imechukuliwa 27.06.2021
5. Tincture. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extracts/tincture/. Imechukuliwa 27.06.2021
6. Perolation. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/percolation/. Imechukuliwa 27.06.2021
7. Maceration. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/maceration/. Imechukuliwa 27.06.2021