Adansonia digitata
Imeandikwa na:
@ULYCLINIC
27 Juni 2021 13:02:36
Utangulizi
Mbuyu umekuwa ukiwashangaza watu wengi kwa jinsi ulivyo mkubwa wa umbo na umekuwa ukitumika kwa matumizi mbalimbali. Lichaya kutumika kama chakula toka enzi, sehemu mbalimbali za mbuyu zimekuwa zikitumika kama tiba ya kuharisha, kuondoa michomo na kuzuia au kutibu matege
Mbuyu hukua na kufikia urefu wa mita 20 hadi 25, shina lake linaweza kuwa kubwa sana kufikia kipenyo cha mita 3. Kikonyo cha jani lake huwa na majani 5 hadi 7.
Maua yake huwa na rangi nyeupe na huzaa matunda ambayo yanafunikwa na podo gumu na ndani ya matunda hayo huwa na mbegu nyeusi iliyo na karanga ndani yake na imefunikwa kwa unga mweupe.
Mti huu hupatikana sana katika ukanda wa tropiki .
Uwezo wa Adansonia digitate katika tiba
Majani ya mbuyu si sumu endapo yakiliwa kama mboga lakini endapo kiini cha dawa atachomwa panya, panya huyo hufa.
Tunda la ubuyu huwa na wanga aina ya kabohaidreti, viini vya pektiki, protini, mafuta, vitamin tindikali na madini mbalimbali.
Uwezo wa ubuyu kuzuia kuharisha hutokana wingi wa viini vya pektiki na kabohaidreti ambazo husaidai mfumowa umeng’enyaji wa chakula kufyonza maji.
Mizizi ya ubuyu ina kiwango kikubwa cha madini ya kalisiamu na ute ute ambao huvimba unapowekwa kwenye chakula na hivyo husaidia mmeng’enyo wa chakula uende vizuri.
Matumizi Adansonia digitate kama dawa
Chukua unga wa ubuyu kutoka kwenye tunda lililokauka baada ya kuuondoa tetele zake kisha changanya gramu 10 za unga wa ubugu kwa mililita 100 za maziwa au maji na kunywa.
Majina mengine ya Adansonia digitate
Majina mengine ya Adansonia digitate hufahamika kama;
• Dawa asili ya kuzuia kuharisha
• Dawa asili ya kuzuia matege
Namna ya kuandaa aina mbalimbali za dawa kutoka kwenye mmea
​
Namna ya kuandaa infusheni ya dawa asilia
​
Infusheni huandaliwa kwa kuzamisha sehemu ya mmea unayotaka kutumia kama dawa kwenye kiasi cha maji yaliyochemka. Baada ya kuzamisha kwenye maji yaliyochemka, maji hayo huchujwa baada ya dakika 15. Dozi ya dawa inayotakiwa kuandaliwa kwa wastani huwa ni gramu 1 kwa kila mililita 10 za maji.
​
Kuna dawa nyingi asilia zimeshatengenezwa na kufungwa kwenye vifungashio vya karatasi ambapo unaweza kutumia kirahisi kama majani ya chai ya kuchovywa. Dawa kwenye fomu hiyo zitapunguza muda wa kuandaa.
​
Namna ya kuandaa dikokshen ya dawa asilia
​
Dikokshen hutumika kuvuna kiini cha dawa ambacho hakiathiriwi na joto.
​
Ili kuandaa dikokshen ya dawa, chemsha magome au mizizi ya mmea kwa muda wa dakika 15 hadi 60 (hutegemea aina ya mmea au kiini cha dawa), kisha pooza na ongeza maji ya baridi ili kutengeneza kiasi cha dawa na wingi wa kiini unachohitaji.
​
Endapo dawa inatakiwa kuchemka kwa muda mrefu, unatakiwa ongezea kiasi cha maji yaliyopotea ili dawa isiungue.
​
Dozi ya dikoksheni ni sawa na infusheni yaani gramu moja ya mmea kwa mililita 10 za maji isipokuwa endapo dawa ina uteute mwingi, gramu moja inatakiwa kuchanganywa na mililita 20 za maji.
Namna ya kuandaa mmengenyo wa dawa
Kuandaa mmeng’enyo wa dawa kwa njia hii unatakiwa weka dawa yako kwenye chombo kisha ongeza maji yenye joto linalotakiwa, mara nyingi joto linatakiwa kuwa kati ya nyuzi za sentigrade 35 hadi 40 ikitegemea aina ya dawa. Lengo kuu la kuzingatia joto ni kutoharibu kiini cha dawa ambacho kinategemea joto.
​
Namna ya kuandaa masalesheni ya dawa
Ili kuandaa masalesheni ya dawa, saga au katakata dawa kwenye vipande vidodo vidogo sana kisha weka kwenye jaa ya kioo yenye kimiminika cha kufyonza dawa. Funika mchanganyiko na acha kwa muda wa siku tatu au zaidi kwenye joto la ndani ya nyumba.Baada ya kutimia kwa siku tatu, tikisa kwa nguvu mara nyingi ili dawa iingie kwenye kimiminika. Baada ya hapo chuja dawa na kamua unga au vipande ili dawa yote itoke. Baada ya hapo unaweza kuchuja dawa kwa ajili ya matumizi au kuifanyia dekatensheni ili kupata kiini safi cha dawa.
​
Namna ya kuandaa pakolesheni ya dawa
Hii ni njia maarufu ya kuandaa tinkcha ya dawa au kufyonza dawa kutoka kwenye kimiminika. Njia hii inahitaji chombo maalumu chenye jina la pakoleta na unatakiwa kuwa mtaalamu zaidi kuandaa dawa kwa njia hii. Soma zaidi maelezo kwa kutumia linki chini ya tovuti hii.
Namna ya kuandaa dawa ya kufyonza kwa kimiminika
​
Njia hii huandaa dawa kutoka kwenye kimiminika chenye dawa au tishu za mnyama kwa kufyonzwa dawa hiyo kwa kutumia kimiminika kingine haswa pombe aina ya ehthanol au maji.
Kiasi cha pombe na maji yanayowekwa hutegemea aina ya dawa. Njia hii inahitaji uwe mtaalamu wa kuandaa dawa, unaweza kujifunza zaidi namna ya kuandaa dawa kwa njia hii kupitia linki chini ya tovuti hii au tumia dawa ambazo tayari zimekwisha andaliwa.
​
Namna ya kuandaa tinkcha ya dawa
Tinkcha ya dawa huandaliwa kwa kufanya masalesheni au pakolesheni ya dawa kwa kutumia kimiminika cha pombe tu. Njia hii ni nzuri ya kuvuna kiwango cha kiini unachotaka kutoka kwenye mimea au mnyama. Soma zaidi kuhusu njia hii kupitia rejea chini ya Makala hii.
​​
KUMBUKA:
Kama kuna haja ya kuchemsha dawa, hakikisha unatumia chomo kilichotengenezwa na udongo au sufuria za stainless steel na usifunike wakati wa kuchemsha ili kutoa sumu na kutobadili kiini cha dawa.
Usitumie dawa zaidi moja na kutibu tatizo moja au mawili tofauti ili kuepuka madhara na mwingiliano
​
Endapo unatumia dawa za hospitali, wasilina na daktari wako kukushauri ili kuepuka mwingiliano wa dawa na madhara yanayoweza kutokea.
ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute msaada kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba kupitia kitufe cha 'Pata tiba' au 'Mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
27 Juni 2021 13:02:36
Rejea za mada hii;
1. Infusion methods. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/infusion/#. Imechukuliwa 27.06.2021
2. Decoction extraction. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/decoction/. Imechukuliwa 27.06.2021
3. Extraction methods digestion. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/digestion/. Imechukuliwa 27.06.2021
4. Fluid extract. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extracts/fluid-extract/. Imechukuliwa 27.06.2021
5. Tincture. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extracts/tincture/. Imechukuliwa 27.06.2021
6. Perolation. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/percolation/. Imechukuliwa 27.06.2021
7. Maceration. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/maceration/. Imechukuliwa 27.06.2021