top of page

Alchemilla vulgaris

Imeandikwa na:

@ULY CLINIC

27 Juni 2021 16:28:41

Utangulizi

Mmea huu ulikuwa ukitumika zamani kurudisha bikra na kusimamisha matiti yaliyokwisha lala na ulijulikana kama ladys mantle.

Miaka ya 1570 maji infusheni ya maji yake ilitumika kutibu mifupa iliyopasuka na iliyovunjika kwa vichanga na watoto wadogo

Dawa hii ilipoongezewa wine nyekundu ilitumika kutibu aina zote za vidonda.

Katika karne ya ishirini mwanzoni mmea huu uligundulika kuwa na uwezo wa kutibu maumivu ya hedhi na kumuandaa mwanamke kabla ya kujifungua.

Siza za mmea Alchemilla vulgaris

• Hustawi mwaka mzima, asili yake ni Ulaya na Amerika kaskazini. Huweza kustawi katika mazingira yoyote na kuna zaidi ya spishi 50 za mmea zinazojulikana kutumika katika matibabu asilia.

• Huwa na shina la kijani mpauko na urefu wake hufikia sentimita 10 hadi 30.

• Majani yake huwa ni mviringo na huwa na lobu 5 hadi 7

• Humea maua mwezi wa tano na kumi,maua yake huwa madogo yenye rangi ya njano na kubadilika kuelekea kijani.

• Katika tiba majani tu hutumika bila maua yake

• Huwa na gallic tannins ambyo hukata damu kutoka kwenye vidonda na flavonoids ambayo ni kiuasumu na huzuia michomo ya kinga ya mwili. Huwa pia na salicyclic acid, phytosterol, saponins, palmitic na stearic acid.

Uwezo wa Alchemilla vulgaris kwenye tiba

Matumizi ndani ya mwili

• Hutumika kutibu tatizo lisilo sugu la kuhara haswa kwa wanawake wajawazito
• Huzuia maumivu ya hedhi na matatizo ya mfumo wa umeng’enyaji wa chakula
• Hurekebisha mzunguko wa hedhi na kutibu dalili zinazotokea kabla ya kuona (PMS)
• Huzuia kutokwa na damu nyingi haswa kwa wanawake wanaoelekea koma hedhi

Matumizi ya nje ya mwili

• Hupakwa ukeni ili kutibu kutokwa na uchafu mweupe ukeni
• Kutibu miguu mizito na uvimbe wa kiwiko cha mkono au mguu
• Hutakasa kinywa na kutibu vidonda mdomoni

Namna ya kutumia Alchemilla vulgaris kama tiba

Matumizi ndani ya mwili

• Ili kutibu kuendesha au maumivu makali ya hedhi, tengeneza infusheni ya gramu 2 hadi 4.5 kwenye mililita 200 za maji kisha kunywa maji hayo kama chai mara mbili hadi tatu kwa siku
• Ili kuzuia matizo ya mfumo wa uzazi tumia dikoksheni inayotengenezwa kwa gramu 7 ya majani yaliyokauka kwenye mililita 200 za maji

Matumizi ya nje ya mwili

• Huweza kutumika kwa kukaliwa, kuloweka au kuoga kwa matatizo mfano uzito wa miguu.
• Tumia infusheni ya gramu 50 za majani yake kwenye lita moja ya maji.
• Kwa sababu kazi zake zinafanana na za homon progesterone, dawa hii inatakiwa kutumika kwa umakini kwa wanaotumia dawa za uzazi wa mpango.
• Dawa hii haipaswi kutumika kwa watu wenye gastraitizi au vidonda vya tumbo
• Endapo una ujauzito tafuta ushauri kutoka kwa daktari wako endapo dawa hii ni salama kwako.

Majina mengine ya alchemilla vulgaris

Alchemilla vulgaris hufahamika kwa majine mengine kama;

• Dawa asili ya kuharisha
• Dawa asili ya kurekebisha hedhi
• Dawa asili ya homon imbalance
• Dawa asili ya miguu mizito
• Dawa asilia ya kubana uke
• Dawa asili ya kusimamisha matiti yaliyolala

Namna ya kuandaa aina mbalimbali za dawa kutoka kwenye mmea

Namna ya kuandaa infusheni ya dawa asilia

Infusheni huandaliwa kwa kuzamisha sehemu ya mmea unayotaka kutumia kama dawa kwenye kiasi cha maji yaliyochemka. Baada ya kuzamisha kwenye maji yaliyochemka, maji hayo huchujwa baada ya dakika 15. Dozi ya dawa inayotakiwa kuandaliwa kwa wastani huwa ni gramu 1 kwa kila mililita 10 za maji.

Kuna dawa nyingi asilia zimeshatengenezwa na kufungwa kwenye vifungashio vya karatasi ambapo unaweza kutumia kirahisi kama majani ya chai ya kuchovywa. Dawa kwenye fomu hiyo zitapunguza muda wa kuandaa.

Namna ya kuandaa dikokshen ya dawa asilia

Dikokshen hutumika kuvuna kiini cha dawa ambacho hakiathiriwi na joto.

Ili kuandaa dikokshen ya dawa, chemsha magome au mizizi ya mmea kwa muda wa dakika 15 hadi 60 (hutegemea aina ya mmea au kiini cha dawa), kisha pooza na ongeza maji ya baridi ili kutengeneza kiasi cha dawa na wingi wa kiini unachohitaji.

Endapo dawa inatakiwa kuchemka kwa muda mrefu, unatakiwa ongezea kiasi cha maji yaliyopotea ili dawa isiungue.

Dozi ya dikoksheni ni sawa na infusheni yaani gramu moja ya mmea kwa mililita 10 za maji isipokuwa endapo dawa ina uteute mwingi, gramu moja inatakiwa kuchanganywa na mililita 20 za maji.

 

Namna ya kuandaa mmengenyo wa dawa

 

Kuandaa mmeng’enyo wa dawa kwa njia hii unatakiwa weka dawa yako kwenye chombo kisha ongeza maji yenye joto linalotakiwa, mara nyingi joto linatakiwa kuwa kati ya nyuzi za sentigrade 35 hadi 40 ikitegemea aina ya dawa. Lengo kuu la kuzingatia joto ni kutoharibu kiini cha dawa ambacho kinategemea joto.

Namna ya kuandaa masalesheni ya dawa

 

Ili kuandaa masalesheni ya dawa, saga au katakata dawa kwenye vipande vidodo vidogo sana kisha weka kwenye jaa ya kioo yenye kimiminika cha kufyonza dawa. Funika mchanganyiko na acha kwa muda wa siku tatu au zaidi kwenye joto la ndani ya nyumba.Baada ya kutimia kwa siku tatu, tikisa kwa nguvu mara nyingi ili dawa iingie kwenye kimiminika. Baada ya hapo chuja dawa na kamua unga au vipande ili dawa yote itoke. Baada ya hapo unaweza kuchuja dawa kwa ajili ya matumizi au kuifanyia dekatensheni ili kupata kiini safi cha dawa.

Namna ya kuandaa pakolesheni ya dawa

 

Hii ni njia maarufu ya kuandaa tinkcha ya dawa au kufyonza dawa kutoka kwenye kimiminika.  Njia hii inahitaji chombo maalumu chenye jina la pakoleta na unatakiwa kuwa mtaalamu zaidi kuandaa dawa kwa njia hii. Soma zaidi maelezo kwa kutumia linki chini ya tovuti hii.

 

Namna ya kuandaa dawa ya kufyonza kwa kimiminika

Njia hii huandaa dawa kutoka kwenye kimiminika chenye dawa au tishu za mnyama kwa kufyonzwa dawa hiyo kwa kutumia kimiminika kingine haswa pombe aina ya ehthanol  au maji.

 

Kiasi cha pombe na maji yanayowekwa hutegemea aina ya dawa. Njia hii inahitaji uwe mtaalamu wa kuandaa dawa, unaweza kujifunza zaidi namna ya kuandaa dawa kwa njia hii kupitia linki chini ya tovuti hii au tumia dawa ambazo tayari zimekwisha andaliwa.

Namna ya kuandaa tinkcha ya dawa

 

Tinkcha ya dawa huandaliwa kwa kufanya masalesheni au pakolesheni ya dawa kwa kutumia kimiminika cha pombe tu. Njia hii ni nzuri ya kuvuna kiwango cha kiini unachotaka kutoka kwenye mimea au mnyama. Soma zaidi kuhusu njia hii kupitia rejea chini ya Makala hii.

KUMBUKA:

 

Kama kuna haja ya kuchemsha dawa, hakikisha unatumia chomo kilichotengenezwa na udongo au sufuria za stainless steel na usifunike wakati wa kuchemsha ili kutoa sumu na kutobadili kiini cha dawa.

 

Usitumie dawa zaidi moja na kutibu tatizo moja au mawili tofauti ili kuepuka madhara na mwingiliano

Endapo unatumia dawa za hospitali, wasilina na daktari wako kukushauri ili kuepuka mwingiliano wa dawa na madhara yanayoweza kutokea.

ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute msaada kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala hii

Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba kupitia kitufe cha 'Pata tiba' au 'Mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

27 Juni 2021 16:28:41

Rejea za mada hii;

bottom of page