top of page

Aloe vulgaris

Imeandikwa na:

@ULY CLINIC

27 Juni 2021 16:42:47

Utangulizi

Ni mmea wa ajabu ambao unatumika mpaka sasa kutibu magonjwa mbalimbali, magonjwa machache sana yameonesha usugu kwake. Mmea wa alovera umekuwa ukitumika kiimani na kwenye tiba toka zamani na hukua kufikia urefu wa sentimita 80, hauna shina na hutoka katika familia ya asphodelaceae.

Mmea huu asili yake ni kaskazini mwa Ulaya, Afrika kusini na kaskazini na kwa sasa umelimwa sehemu nyingi duniani.

Sifa za mmea Aloe vulgaris

Kuna spishi nyingi za mmea wa Aloe vulgaris lakini spishi inayofahamika na nzuri ni aloe vera ambao juisi yake huwa na uwezo mkubwa kwenye tiba na lishe.

Juisi ya aloe vera huwa na uwezo wa

• Kuamsha kinga ya mwili
• Kufanya kazi za antibayotiki
• Kuzuia shambulio binafsi la kinga
• Kuponya, kutuliza na kutakasa tumbo
• Huondoa sumu na kusafisha figo, ini na mapafu.
• Hupunguza maumivu ya tumbo,
• Hushauriwa kutumika kwa wagonjwa wa kisukari, mzio, konstipeshen, magonjwa ya moyo.
• Juisi ya alo vera huwa na vitamin A, B, C na E pamoja na madini kama phosphorus, potasiamu, kalisiamu, chlorine, chuma na zinki.

Ukitambua matumizi yake vema, mme huu hautakuangusha, popote ulipo unaweza kuupanda kwenye bustani au kwenye kopo la maua na kisha utakuwa wenyewe, kazi yako ni kuupa maji kidogo sana.

Uwezo wa Aloe vulgaris kwenye tiba

Maji ya majani yake yaliyokatwakatwa vipande vidogo kisha kulowekwa kwenye maji kwa dakika 2 hadi 3 huwa na uwezo wa;

• Kutumika kama losheni ya ngozi
• Kutibu majeraha ya kuungua kwa sababu ya mionzi
• Kuharakisha kupona kwa vidonda vya tumbo
• Kutibu magonjwa yote a ngozi
• Kutibu majeraha ya kuungua na jua, mikraruzo na maumivu ya varikosi
• Hutuliza mfumo wa chakula na kufanya kinyesi kipite kwa haraka

Kumbuka, Usitumie maji ya aloe vera baada ya siku moja kwa sababu hupoteza uwezo wake wa kitiba.

Namna ya kutumia Aloe vulgaris kama tiba

Vidonda

• Paka juisi yake kwenye kidonda isipokuwa kidonda cha kuungua na barafu
Haja ngumu/konstipesheni

• Loweka majani kiasi kwenye kikombe cha chai na changanya na resin kisha kunywa katikati ya milo yako mikubwa kila siku kwa wiki mbili mpaka

Kwa matibabu ya Kisukari, vidonda vya tumbo, uchovu mkali, magonjwa ya shambulio binafsi la kinga, haja ngumu, kutomeng’enwa vema kwa chakula, matatizo ya mzunguko wa damu, maambukizi ya herpes, maumivu ya tumbo, maumivu ya gastriki, saratani, magonjwa yasiyo na tiba nay a ngozi au magonjwa sugu ya tumbo fanya hivi

• Changanya vijiko viwili hadi vitatu kwenye bilauri ya maji au juisi kisha kunywa mara mbili hadi tatu kwa siku au kula kiini cha ndani ya jani baada ya kutoa maganda kwa siku.

Majina mengine ya aloe vulgaris

Mmea huu hufahamika kwa majina mengine kama;

• Dawa asili ya magonjwa ya ngozi
• Dawa asili ya vidonda vya tumbo
• Dawa asili ya kuungua na moto
• Dawa asili ya mikraruzo ya ngozi
• Dawa asili ya kulainisha kinyesi

Namna ya kuandaa aina mbalimbali za dawa kutoka kwenye mmea

​

Namna ya kuandaa infusheni ya dawa asilia

​

Infusheni huandaliwa kwa kuzamisha sehemu ya mmea unayotaka kutumia kama dawa kwenye kiasi cha maji yaliyochemka. Baada ya kuzamisha kwenye maji yaliyochemka, maji hayo huchujwa baada ya dakika 15. Dozi ya dawa inayotakiwa kuandaliwa kwa wastani huwa ni gramu 1 kwa kila mililita 10 za maji.

​

Kuna dawa nyingi asilia zimeshatengenezwa na kufungwa kwenye vifungashio vya karatasi ambapo unaweza kutumia kirahisi kama majani ya chai ya kuchovywa. Dawa kwenye fomu hiyo zitapunguza muda wa kuandaa.

​

Namna ya kuandaa dikokshen ya dawa asilia

​

Dikokshen hutumika kuvuna kiini cha dawa ambacho hakiathiriwi na joto.

​

Ili kuandaa dikokshen ya dawa, chemsha magome au mizizi ya mmea kwa muda wa dakika 15 hadi 60 (hutegemea aina ya mmea au kiini cha dawa), kisha pooza na ongeza maji ya baridi ili kutengeneza kiasi cha dawa na wingi wa kiini unachohitaji.

​

Endapo dawa inatakiwa kuchemka kwa muda mrefu, unatakiwa ongezea kiasi cha maji yaliyopotea ili dawa isiungue.

​

Dozi ya dikoksheni ni sawa na infusheni yaani gramu moja ya mmea kwa mililita 10 za maji isipokuwa endapo dawa ina uteute mwingi, gramu moja inatakiwa kuchanganywa na mililita 20 za maji.

 

Namna ya kuandaa mmengenyo wa dawa

 

Kuandaa mmeng’enyo wa dawa kwa njia hii unatakiwa weka dawa yako kwenye chombo kisha ongeza maji yenye joto linalotakiwa, mara nyingi joto linatakiwa kuwa kati ya nyuzi za sentigrade 35 hadi 40 ikitegemea aina ya dawa. Lengo kuu la kuzingatia joto ni kutoharibu kiini cha dawa ambacho kinategemea joto.

​

Namna ya kuandaa masalesheni ya dawa

 

Ili kuandaa masalesheni ya dawa, saga au katakata dawa kwenye vipande vidodo vidogo sana kisha weka kwenye jaa ya kioo yenye kimiminika cha kufyonza dawa. Funika mchanganyiko na acha kwa muda wa siku tatu au zaidi kwenye joto la ndani ya nyumba.Baada ya kutimia kwa siku tatu, tikisa kwa nguvu mara nyingi ili dawa iingie kwenye kimiminika. Baada ya hapo chuja dawa na kamua unga au vipande ili dawa yote itoke. Baada ya hapo unaweza kuchuja dawa kwa ajili ya matumizi au kuifanyia dekatensheni ili kupata kiini safi cha dawa.

​

Namna ya kuandaa pakolesheni ya dawa

 

Hii ni njia maarufu ya kuandaa tinkcha ya dawa au kufyonza dawa kutoka kwenye kimiminika.  Njia hii inahitaji chombo maalumu chenye jina la pakoleta na unatakiwa kuwa mtaalamu zaidi kuandaa dawa kwa njia hii. Soma zaidi maelezo kwa kutumia linki chini ya tovuti hii.

 

Namna ya kuandaa dawa ya kufyonza kwa kimiminika

​

Njia hii huandaa dawa kutoka kwenye kimiminika chenye dawa au tishu za mnyama kwa kufyonzwa dawa hiyo kwa kutumia kimiminika kingine haswa pombe aina ya ehthanol  au maji.

 

Kiasi cha pombe na maji yanayowekwa hutegemea aina ya dawa. Njia hii inahitaji uwe mtaalamu wa kuandaa dawa, unaweza kujifunza zaidi namna ya kuandaa dawa kwa njia hii kupitia linki chini ya tovuti hii au tumia dawa ambazo tayari zimekwisha andaliwa.

​

Namna ya kuandaa tinkcha ya dawa

 

Tinkcha ya dawa huandaliwa kwa kufanya masalesheni au pakolesheni ya dawa kwa kutumia kimiminika cha pombe tu. Njia hii ni nzuri ya kuvuna kiwango cha kiini unachotaka kutoka kwenye mimea au mnyama. Soma zaidi kuhusu njia hii kupitia rejea chini ya Makala hii.

​​

KUMBUKA:

 

Kama kuna haja ya kuchemsha dawa, hakikisha unatumia chomo kilichotengenezwa na udongo au sufuria za stainless steel na usifunike wakati wa kuchemsha ili kutoa sumu na kutobadili kiini cha dawa.

 

Usitumie dawa zaidi moja na kutibu tatizo moja au mawili tofauti ili kuepuka madhara na mwingiliano

​

Endapo unatumia dawa za hospitali, wasilina na daktari wako kukushauri ili kuepuka mwingiliano wa dawa na madhara yanayoweza kutokea.

ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute msaada kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala hii

Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba kupitia kitufe cha 'Pata tiba' au 'Mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

27 Juni 2021 17:39:56

Rejea za mada hii;

bottom of page